figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,890
Salaam Wakuu,
Kuna kipande kidogo cha video kinasambaa Mtandaoni, James Mbatia Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi akielezea kusikitishwa kwake na wanaomuona kwamba anavunja nguvu upinzania.
Hapa chini nmenukuu kile alichokiongea na kukiandika hapa chini.
Ameanza kwa kusema:
"Mimi ni Mbunge wa Vunjo, umewahi kunisikia nalalamikia labda CHADEMA kwanini wameweka Mgombea kule Vunjo?
Niwe mkweli tu. Uchaguzi mkuu mwaka 2015 vyama Vingine viliweka Wagombea na wao tumo ndani ya UKAWA tukagawana zile kura za Madiwani CCM ikashinda, ulisikia nmelalamika?
Mwaka juzi nlimwambia Naibu Katibu Mkuu Bara Elizabeth kawaulize Washirika Wenzetu kwanini wanafanya fujo kule Vunjo? Alipowauliza wakasema Mbatia amezoea kudekadeka sana. Ulisikia nalalamika popote?
Ni haki yao na ni haki ya chama kilicho sajiliwa kina haki ya kufanya kazi mahali popote pale.
Mwasisi namba moja wa NCCR Mageuzi mwenye chama Mabere Nyaucho Marando alihamia CHADEMA ulisikia nalalamika popote? Kwanza nliulizwa nikawambia namtakia kila la heri, ni haki yake. Mwesigwa Baregu, ni haki yake.
Nakuhakikishia ukweli wa Mungu Chacha Wangwe akiwa Diwani wa NCCR Mageuzi Tarime Mjini 2003, walienda Viongozi wa CHADEMA wakamchukua wakamfanya Mwenyekiti wa Mkoa wa CHADEMA na wakati yupo NCCR Mageuzi na hatukumfukuza chama. aliendelea kuwa DIWANI"
Mwisho wa kumnukuu.
MY TAKE:
Vya vya siasa vya Tanzania vimetawaliwa na UBINAFSI, KIBURI, KUJIONA BORA na JICHO KWENYE FEDHA ZA BURE.