scramble
JF-Expert Member
- Nov 29, 2012
- 1,593
- 256
kwanza nimpongeze mbatia kwa kazi nzuri anayo ifanya kuhusu suala la elimu hapa nchini. amekua msitari wa mbele kuonesha madudu yaliyomo ktk sekta ya elimu hapa nchini. ikumbukwe kuwa wadau kama hakielimu na wengineo, pamoja na wabunge wengine wamekua wakilalamikia baadhi ya mapungufu yaliyomo ktk sekta ya elimu. mbatia amejikita sana katika kukosoa mitaala na vitabu vinavyo tumika mashuleni. hapo zamani, seriklai ilikua ikiandika vitabu kupitia taasisi ya elimu na vilikua vikisambazwa na Tanzania elimu supplies. ubadhuirifu pale taasisi na Tanzania elimu supplies, ulikua unaisababishia serikali hasara kubwa na vitabu vilikua vinapungua au kukosekana mashuleni. ilibidi serikali iruhusu kampuni binafsi ziandike vitabu na maduka binafsi ya vitabu yalishamiri. kiliundwa chombo cha kupitia vitabu vya kampuni binafsi kwa kuvihakiki kabla havijachapishwa kwa wingi na kupelekwa mashuleni. chombo hicho maarufu kwa jina la EMAC kilianza vizuri lkn siku zilipozidi walianza kuomba rushwa ili wapitishe kitabu. baada ya rushwa kushamiri, wenye vitabu walilazimisha vitabu vyao vipitishwe haraka iwezekanavyo. RUSHWA NI ADUI WA HAKI. hali hiyo iliwafanya EMAC wasipitie vitabu kwa umakini. najua vitabu vinaweza kuwa na makosa madogomadogo ya hapa na pale khasa ya imla (spelling). ktk kitabu kizima linapotokea kosa moja sidhani kama ni suala la kupigia kelele na kukiita kitabu sumu. makampuni binafsi yamefanya kazi kubwa sn ktk tasnia ya uandishi wa vitabu. suingi mkono kuwa na kitabu kimoja kinacho andikwa na serikali. tukirudi kwenye kitabu kimoja tumekwisha. dunia ya leo ni ya kusoma vitabu vingi na kutafiti hapa na pale. inaelekea mbatia anatumwa kupambana na baadhi ya kampuni za uzalishaji vitabu. kama kitabu kina maswali zaidi ya elfu moja lkn swali moja likakosewa kwa kusema 7x2=15, sidhani kama ni sahihi kwa mbatia kukiita kitabu hicho SUMU. kote ulimwenguni makosa madogo hutokea ktk vitabu. kama mwalimu ni mweledi, akibaini kosa hulirekebisha papo hapo. sidhani kama ni sahihi kubeza kazi kubwa inayofanywa na kampuni binafsi zinazo chapisha vitabu. mbatia asivuke mipaka kwa kupoteza watu kuwa vitabu vyote hapa nchini ni sumu. kinacho nishangaza ni kwamba, nilikwenda wiki iliyo pita ktk ofisi za umoja wa wachapisha vitabu. niliwauliza kama walishawahi kutembelewa na mbatia au kuandikiwa barua inayo onesha baadhi ya makosa vitabuni? WALIJIBU HAPANA. nilishangaa sana kusikia hivyo. ni hayo tu wadau