James mbatia asichanganye elimu na siasa

scramble

JF-Expert Member
Nov 29, 2012
1,593
256
kwanza nimpongeze mbatia kwa kazi nzuri anayo ifanya kuhusu suala la elimu hapa nchini. amekua msitari wa mbele kuonesha madudu yaliyomo ktk sekta ya elimu hapa nchini. ikumbukwe kuwa wadau kama hakielimu na wengineo, pamoja na wabunge wengine wamekua wakilalamikia baadhi ya mapungufu yaliyomo ktk sekta ya elimu. mbatia amejikita sana katika kukosoa mitaala na vitabu vinavyo tumika mashuleni. hapo zamani, seriklai ilikua ikiandika vitabu kupitia taasisi ya elimu na vilikua vikisambazwa na Tanzania elimu supplies. ubadhuirifu pale taasisi na Tanzania elimu supplies, ulikua unaisababishia serikali hasara kubwa na vitabu vilikua vinapungua au kukosekana mashuleni. ilibidi serikali iruhusu kampuni binafsi ziandike vitabu na maduka binafsi ya vitabu yalishamiri. kiliundwa chombo cha kupitia vitabu vya kampuni binafsi kwa kuvihakiki kabla havijachapishwa kwa wingi na kupelekwa mashuleni. chombo hicho maarufu kwa jina la EMAC kilianza vizuri lkn siku zilipozidi walianza kuomba rushwa ili wapitishe kitabu. baada ya rushwa kushamiri, wenye vitabu walilazimisha vitabu vyao vipitishwe haraka iwezekanavyo. RUSHWA NI ADUI WA HAKI. hali hiyo iliwafanya EMAC wasipitie vitabu kwa umakini. najua vitabu vinaweza kuwa na makosa madogomadogo ya hapa na pale khasa ya imla (spelling). ktk kitabu kizima linapotokea kosa moja sidhani kama ni suala la kupigia kelele na kukiita kitabu sumu. makampuni binafsi yamefanya kazi kubwa sn ktk tasnia ya uandishi wa vitabu. suingi mkono kuwa na kitabu kimoja kinacho andikwa na serikali. tukirudi kwenye kitabu kimoja tumekwisha. dunia ya leo ni ya kusoma vitabu vingi na kutafiti hapa na pale. inaelekea mbatia anatumwa kupambana na baadhi ya kampuni za uzalishaji vitabu. kama kitabu kina maswali zaidi ya elfu moja lkn swali moja likakosewa kwa kusema 7x2=15, sidhani kama ni sahihi kwa mbatia kukiita kitabu hicho SUMU. kote ulimwenguni makosa madogo hutokea ktk vitabu. kama mwalimu ni mweledi, akibaini kosa hulirekebisha papo hapo. sidhani kama ni sahihi kubeza kazi kubwa inayofanywa na kampuni binafsi zinazo chapisha vitabu. mbatia asivuke mipaka kwa kupoteza watu kuwa vitabu vyote hapa nchini ni sumu. kinacho nishangaza ni kwamba, nilikwenda wiki iliyo pita ktk ofisi za umoja wa wachapisha vitabu. niliwauliza kama walishawahi kutembelewa na mbatia au kuandikiwa barua inayo onesha baadhi ya makosa vitabuni? WALIJIBU HAPANA. nilishangaa sana kusikia hivyo. ni hayo tu wadau
 
Siku hizi bungeni wanamwita Engineer, huu ni u-KIHIYO mwingine. tunajua alisomea Uhandisi na akafukuzwa chuo muhula mmoja kabla ya kumaliza, na muda wote huo amekuwa mwanasiasa wala hiyo fani hajawahi kuitumikia.
 
Mkuu kidogo nimeshindwa kuelewa mantiki ya hoja yako hapa.Unasema Mbatia asichanganye siasa katika mambo ya elimu hivi wa kulaumiwa kwa kuingiza siasa katika elimu ni Mbatia au Serikali?Mara ngapi Serikali imeshindwa kufanyia kazi ushauri kutoka kwa wadau mbali mbali wa ELIMU na Wananchi wa kawaida juu ya namna gani Serikali inapaswa kufanya ili kuokoa sekta ya elimu lakini wakapuuza?Mara ngapi Serikali hii imekuwa ikuchukua hatua au kufanya maamuzi yaliyopelekea matokeo kuwa mabaya zaidi katika sekta hii ya elimu ukiwemo huu uamuzi wa kuunda Tume ya Pinda kuchunguza matokeo mabovu ya kidato cha nne wakati sababu zilikuwa zinafahamika,Si ndio kuingiza kwenyewe siasa katika mambo ya msingi yaliyokuwa yakihitaji tiba sahihi ya kuyashughulikia?Mbatia alikuwa sahihi kabisa kuviita vile vitabu ni sumu maana vinapandikiza vimelea hatari vya elimu bandia katika akili za watoto wa kitanzania.Siku ya siku hutaweza kuwatofautisha hawa waliosoma na wale wasiosoma kabisa kiuelewa labda watofautiane ktk kusoma na kuandika
 
EMAC kilianza vizuri lkn siku zilipozidi walianza kuomba rushwa ili wapitishe kitabu. baada ya rushwa kushamiri, wenye vitabu walilazimisha vitabu vyao vipitishwe haraka iwezekanavyo. RUSHWA NI ADUI WA HAKI. hali hiyo iliwafanya EMAC wasipitie vitabu kwa umakini.

Inaelekea wewe ama ni mmiliki wa kampuni ya uchapaji vitabu na ulitoa rushwa kwa EMAC ili vipitishwe. Sasa unaona Mbatia kawashika pabaya vitabu vyenu vitawadodea unaanza kutetea kuwapo na makosa kwenye vitabu halafu unasema hiyo siyo sumu kwenye elimu. Basi nachukua nafasi hii kukuunga mkono kumpongeza jwa dhati mwandishi aliyeandika 2x7=15; 0/0=0. Naomba waandishi wote wa vitabu muige mfano wa bingwa huyo kama anavyopendekeza mleta hoja yaani watanzania wanafunzishwa kusifia ujinga kiasi hicho! Hivi nani anayechanganya elim na siasa, ni mleta mada hii uchwara au ni Mbatia alivyoanika uozo na kuonesha jinsi gani rushwa ina nguvu kuliko hata uzalendo katika masuala muhimu kwa taifa. Bila hata aibu watu wanapitisha vitabu vyenye makosa na wengine mchana kweupe wanaleta thread ya kuwatetea.

Basi waambie waongeze na hesabu ziuatazo ili vitabu vyao vipate wateja zaidi|
2+3 = 23; 3+3=33
 
sina maslahi yoyote na uandishi. suing mkono makosa kuonekana ktk vitabu hapa nchini. kilio change ni kwamba jambo hili limekuzwa sana. haiwezekani kitabu chenye maswali zaidi ya elfu moja swali moja likosewe jibu lake kasha kiitwe sumu. hapo ndipo ninapo palalamikia. mbatia nahisi ametumwa na hiyohiyo serikali ili taasisi waturudishe miaka ya nyuma kwa kuwa waandishi pekee wa vitabu vya shule. kampuni binafsi kwa mfano oxford, macmilan, longman, educational, ben, mture na mkuki na nyota wamefanya kazi kubwa sana. mimi ni mwalimu kwa kipindi cha miaka 10. vitabu vingi vinaleta changamoto na ni msaada mkubwa kwa walimu
 
scramble yupo scrambled kichwan... anasema mbatia asilete siasa halaf yeye ndo analeta siasa za ajabu kabisa...ndugu umeamua na wewe kukalia akil zako? 7+7 =15 we unaona kosa dogo? maskin scramble.hiv uliisoma kwanza post yako au uliandika tu usingzn au ukisukumwa na hila ndan ya moyo wako. hiv mtoto akiandika hilo jib kwa hiyo hesab ukamkosesha akaleta kitab utafanyaje? au wewe ulidhan emac walipaswa kuhariri machapisho ya vitab vyote vya toleo hilo? acha uvivu wa kufkir unalaza ubongo ili uwe bado mpya? tumia ubongo.
 
sina maslahi yoyote na uandishi. suing mkono makosa kuonekana ktk vitabu hapa nchini. kilio change ni kwamba jambo hili limekuzwa sana. haiwezekani kitabu chenye maswali zaidi ya elfu moja swali moja likosewe jibu lake kasha kiitwe sumu. hapo ndipo ninapo palalamikia. mbatia nahisi ametumwa na hiyohiyo serikali ili taasisi waturudishe miaka ya nyuma kwa kuwa waandishi pekee wa vitabu vya shule. kampuni binafsi kwa mfano oxford, macmilan, longman, educational, ben, mture na mkuki na nyota wamefanya kazi kubwa sana. mimi ni mwalimu kwa kipindi cha miaka 10. vitabu vingi vinaleta changamoto na ni msaada mkubwa kwa walimu
Kwanza si kazi ya Mbatia kufanya kazi ya kurekebisha makosa ya kizembe kwenye vitabu! Kwanini kitabu muhimu kama kinachotumiwa kwenye kazi nyeti kama hii kisihakikiwe? Hujui kwenye sayansi kosa moja dogo linaweza kuleta maafa! Makosa madogo madogo namna hiyo yangekuwa yanaoneka si kitu ndege zisingerua
 
Huyu jamaa ana ufikiri finyu sana..
Hivi kama leo mwanafunzi unamjenga kuona makosa ni swala la kawaida hata kesho atakapokuja kuwa daktari atakosa umakini kwenye kutoa tiba, pia hata engineer atakosea ratio katka materials matokeo yake yatakuwa maafa matupu... Mtoa mada huo ualimu wako wa miaka kumi haujakusaidia lolote. Kwanza nakushangaa sanaa unapotoa povu ukitaka kuhalalisha makosa katika vitabu ionekane ni kitu cha kawaida
 
Mleta mada, kitabu ili kipitishwe, inatakiwa kisiwe na kosa.
Hizo kampuni kama Oxford, Longman, Penguin, Mkuki na Nyota .... ni publishing companies amabazo huzipa printing presses order za vitabu. Publishers wanakuwa na files, zinawekwa kwenye plates (pre-press) baada ya kuhakikiwa, zinakuwa printed, zinakaguliwa pages not only for spelling , also color inconsistencies, pagination, etc ...

Zikimalizwa pages zote kukaguliwa, wanapewa ok ya kubind pages, wakisha-bind vinakaguliwa kuangalia pagination, gluing au stitching errors depending on the binding style, halafu baada ya hapo wanapeleka copy check kuhakiki tena kama kipo sawa ...

Baada ya hapo copies zinatumwa kwa publisher, ana approve halafu anaagiza copy kadhaa zitengenezwe, zinatengenezwa halafu randomly, board of education zinakagua tena hivyo vitabu kabla ya kuvipitisha.

Mimi hii ndiyo field yangu for the past 12yrs, it's painful na huwezi kumuhonga mtu kwa sababu inainvolve watu wengi sana, na kwa huku nilipo the process is digital with human eyes involved na hiyo ni kama kukuelezea juujuu tu..... hapo sijakueleza jinsi targeted readers wanavyokuwa invoilved.

USISEME KOSA MOJA SIO BIG DEAL!!!, KOSA MOJA LINAWEZA KUSAMBARATISHA BOARD OF EDUCATION!!
 
sina maslahi yoyote na uandishi. suing mkono makosa kuonekana ktk vitabu hapa nchini. kilio change ni kwamba jambo hili limekuzwa sana. haiwezekani kitabu chenye maswali zaidi ya elfu moja swali moja likosewe jibu lake kasha kiitwe sumu. hapo ndipo ninapo palalamikia. mbatia nahisi ametumwa na hiyohiyo serikali ili taasisi waturudishe miaka ya nyuma kwa kuwa waandishi pekee wa vitabu vya shule. kampuni binafsi kwa mfano oxford, macmilan, longman, educational, ben, mture na mkuki na nyota wamefanya kazi kubwa sana. mimi ni mwalimu kwa kipindi cha miaka 10. vitabu vingi vinaleta changamoto na ni msaada mkubwa kwa walimu

Kama wewe ni Mwalimu basi nina hakika shule yako ni miongoni mwa shule ambazo wanafunzi wengi kama si wote wametaga mayai. Una mawazo ya kimburula mno na inaonekana una ujauzito wa kufikiri mchumia tumbo mkubwa wewe. Ni wazi kuwa unatumiwa na hayo makampuni binafsi unayoyasifia kwa kuwaandalia watoto wa kitanzania vitabu vyenye hesabu za uongo. Eti tuwapongeze kwa kufanya kazi kubwa ya kuwaelekeza watoto wa kitanzania kuwa 2x7=15. Ondoa njaa yako huku ni kwenye jamvi la great thinkers ambao kwao ni rahisi sana kutambua mchele ni upi na chuya ni ipi. Kama hayo makampuni unayasifia, kwa nini yameshindwa kubaini makosa ya wazi kiasi hicho.

KAma kweli wewe ni mwalimu acha kabisa kutudhalilisha walimu wenzako hatupendi kabisa kuona vitabu vyenye makosa vikiwa sokoni. Kumbuka kuwa kuna shule zenye uhaba wa walimu wanafunzi wanajisomea wenyewe. Toka hapa wewe ndiye unayetaka kuleta siasa kwenye elimu. Hatuwezi kukubali vitanu vyenye makosa vitumike shuleni hiyo ni sumu kali kwenye elimu.
 
Siku hizi bungeni wanamwita Engineer, huu ni u-KIHIYO mwingine. tunajua alisomea Uhandisi na akafukuzwa chuo muhula mmoja kabla ya kumaliza, na muda wote huo amekuwa mwanasiasa wala hiyo fani hajawahi kuitumikia.

Mkuu,
Mbatia kasoma uhandisi katika Chuo Kikuu cha Hanze, nchini Uholanzi
 
sina maslahi yoyote na uandishi. suing mkono makosa kuonekana ktk vitabu hapa nchini. kilio change ni kwamba jambo hili limekuzwa sana. haiwezekani kitabu chenye maswali zaidi ya elfu moja swali moja likosewe jibu lake kasha kiitwe sumu. hapo ndipo ninapo palalamikia. mbatia nahisi ametumwa na hiyohiyo serikali ili taasisi waturudishe miaka ya nyuma kwa kuwa waandishi pekee wa vitabu vya shule. kampuni binafsi kwa mfano oxford, macmilan, longman, educational, ben, mture na mkuki na nyota wamefanya kazi kubwa sana. mimi ni mwalimu kwa kipindi cha miaka 10. vitabu vingi vinaleta changamoto na ni msaada mkubwa kwa walimu

Kama umesoma kwa makini nadhani wakuu humu wamekupa majibu ya size yako, kwa hiyo kama ulikuwa umetumwa nakwambia ukumbuke kuwa akili ya kuambiwa changanya na yako na kama ulikuwa unajaribu kuganga njaa basi nadhani unejifunza kuwa kwenye elimu siyo sehemu ya kugangia njaa ni sehemu ya kuhakikisha mambo mazuri yanaandaliwa kwa manufaa ya kiZazi cha sasa na cha baadaye
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom