James Mbatia Anaua Upinzani Angalia Barua hii!

KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
864
Mwenyekiti wa NCCR Jemus Mbatia ametajwa kwa mara ya kwanza na Mwenyekiti wa Chadema Mh Freeman Mbowe na kuwakataa Wabunge wake waliiopewa Mashart na Rais Kikwete kuhakikisha kwamba Washambulia Chadema.

Hata hivyo David Kafulila alitamuka wazi kuwa Mbatia anafanya kazi ya CCM na kuua Upinzani kwa Ushahidi wa kumushitaki Mhe Halima Mdee.

CCM walimushauli Mbatia Kufuta Kesi ya Kawe huku Kikwete akijiandaa kumupa Ubunge viti Maalumu ambapo amejipenyeza urafiki kwa Chadema ilikuunga nguvu ya Shibuda na kuua Upinzani!!!
Angalia barua hii aliyo andika ili upate ukweli wa Mambo!!!!



NCCR – MAGEUZI
National Convention for Construction and Reform – Mageuzi

Kumb Na. NCCR-M/MM/BJMT/10/21 17 January, 2012
Mhe.Nee S. Makinda (mb)
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Ofisi ya Bunge,
S.L.P 9133,
DAR ES SALAAM.
Mheshimiwa Spika, Salaam.

YAH: TASWIRA DHALILI YA CHAMA CHA NATIONAL CONVENTION FOR CONSTRUCTION AND REFORM – MAGEUZI KWA OFISI YA BUNGE.
Tafadhali husika na somo hapo juu.Chama chetu cha National Convention for Construction and reform – mageuzi (NCCR-Mageuzi) ni miongoni mwa vyama vya siasa vinavyotambulika hapa nchini na chenye usajili wa kudumu kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, sura ya 258 ilivyoruhusiwa mwaka 2002.
Aidha unantaambua kwamba chama chetu kilishiriki uchaguzi mkuu wa Urais, Wabunge,Wajumbe wa baraza la Wawakilishi na Madiwani wa Mwaka 2010 ambapo tulifanikiwa kupata viti vya wabunge wane katika bunge Tukufu.
Mheshimiwa Spika, unatambua pia kwamba mnamo tarehe 21/12/2011, chama chetu kilikuandikia na kukufahamisha kuhusu hatua za kinidhamu alizochukuliwa aliyekuwa mmoja wa wanachama wake ndugu David Zacharia Kafulila na ambaye kwa tiketi ya chama hiki alichaguliwa kuwa mbunge jimbo la Kigoma Kusini. Barua yetu yenye Kumb. NA NCCR-M/MM/BJMT/10/20 iliyoandikwa na kukabidhiwa kwako kupitia kwa Katibu Mkuu wetu wa chama Ndugu Samuel AM. Ruhuza ya tarehe 21/12/2011 ikikufahamisha hatua hizo, na nina uhakika unayo ofisi kwako. Ni tegemeo letu kuwa hadi sasa ofisi yako ilitakiwa kuwa imeshachukua hatua zinazostahili kuhusiana na nafasi ya Mbunge ambaye amevuliwa uanachama wake na chama cha sias anachokiwakilisha Bungeni.
Tofauti na matarajio yetu, nasikitika kueleza kwamba ofisi yako imeamua kutoyatilia maanani matakwa ya kisheria yanayohusiana na nafasi ya Mbunge anayeacha au kuvuliwa uanachama na chama chake. Badala yake, ofisi yako imeendelea kumtambua ndugu David Zacharia Kafulila na kumpa fursa na nafuu zote za Mbunge bila kujali hatua za chama ambazo zilichukuliwa.

HEAD QUARTERS
P.O.BOX 72474, DAR ES SALAAM, TANZANIA​
Phone/Fax:+255-022-2862238/website:www.nccrmageuzi.or.tz/Email:info@nccrmageuzi.or.tz



All correspondence should be addressed to the Secretary General
Mheshimiwa Spika, kana kwamba hayo hayatoshi, nikiwa mbele yako na katika hafla ya kuaga mwili wa marehemu Regia Mtema (Mb), aliyeaga dunia kwa ajali ya gari tarehe 14/01/2012 na mwili wake kuagwa leo tarehe 17/01/2012 katika ukumbi wa Karimjee. Ofisi yako imefanya kitendo cha kutudhalilisha, kutunyanyasa, kutufedhehesha,kutuonea na kejeli kwa maamuzi halali ya Halmashuri Kuu ya Taifa ya Chama chetu, licha ya kwamba umetoa tamko na msimamo wako binafsi na wa ofisi yako kwamba, Watanznia tuwe na moyo wa upendo na ushirikiano na kuacha itikadi zetu za vyama na tofauti zetu ndogo ndogo ili tujenge taifa moja lenye umoja na Upendo. Hii ilikuwa ni kauli nzito na inayoonesha msimamo wa ofisi yako wa kutenda kazi zake bila kujali itikadi za watu wala tofauti zao,
Wakati huo huo, nimesikitika pia kuona ofisi yako ikitenda kinyume na kauli yako nzito kama ilivyoelezwa hapo juu kwa kutangaza majina ya wabunge watakaowasilisha vyama katika mmsafara wa maziko huko Ifakara mkoani Morogoro, katika namna ambayo ilitukejeli, kutudhalilisha na kushusha heshima ya chama chetu cha kijamii. Hii imetokana na kauli ya mwendeshaji wa hafla hiyo kutoka katika ofisi yako alipoueleza umma wa watanzania kwamba mwakilishi wa chama cha NCCR – Mageuzi katika maziko atakuwa ndugu David Zacharia Kafulia. Kauli hii imetolewa mbele yangu nikiwa Mwenyekiti wa Taifa, Msimamizi Mkuu wa Maslaihi ya Chama na msemaji mkuu wa chama cha NCCR – Mageuzi na bila kujali athari za kisiasa na kiitikadi ambazo kwa sasa zipo kufuatia hatua za kumvua uanachama ndugu David Zacharia Kafulia katika chama chetu.

Mheshimiwa Spika, nasikitika pia kuiarifu ofisi yako kwamba kwa kumtangaza ndugu David Zacharia Kafulia kuwa mwakilishi wa NCCR – Mageuzi katika msafara wa maziko ni kukiuka kanuni na misingi ya haki. Ni dhahiri kwamba chama chetu hakijakuandikia barua ya kumtambulisha ndugu David Zacharia Kafulia kuwa mwakilishi wetu katika hafla hiyo, mbali na kwamba tunao wabunge wengine. Naamini kwamba hekima ya ofisi yako ingelitafakari athari za kitendo hicho cha chama chetu. Ni kitendo ambacho kinatupa ujumbe kwamba ofisi yako imetumika kukidhoofisha chama chetu, kwanza kwa kutoweka bayana masuala ya msingi yanayotokana na hatua za kinidhamu tulizozichukua na sasa kuanza kumnadi hadharani ndugu David Zacharia Kafulia kuwa mwanachama wetu ilhali ofisi yako inafahamu kuwa siyo kweli. Hizi fedheha ambazo ofisi yako inaanza kuzijenga na kuwataka watanzania wamtambue hivyo na kumjengea utukufu ndugu David Zacharia Kafulia kuwa yeye yuko juu ya chama. Hakika kwa kitendo hicho, haki haijatendeka, hekima haikutumika na busara zinakataa kukubaliana na jambo hilo. Mtu ambaye amevuliwa uanachama kwa kufukuzwa na chama husika hawezi leo hii akaonekana ndiye mtu pekee aliyeteuliwa kukiwakilisha chama hicho, tena katika hafla ya kitaifa.

Ingelikuwa ndugu David Zacharia Kafulia alipovuliwa uanachama wake tayari ameshahamia chama kingine je?, ofisi yako ingeendelea kumtambua kuwa mwanachama na mwakilishi wa NCCR – Mageuzi? Hii ni sawa na kiongozi wa dini kubadili imani yake na kuendelea kuongoza ibada za dini alikotoka. Ni dhahiri jamii haitamuelewa kiongozi huyo wa dini na pia waumini wenzake katika dini alikotoka hawatakuwa na imani naye tena ya kuwangoza katika ibada zao.
Ibara ya 71(1)(a) na (f) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 imeweka bayana kwamba Mbunge ataacha kuwa Mbunge na kiti chake kubaki wazi endapo sifa alizokuwa nazo wakati wa kuchaguliwa zitabadilika na kumfanya akose sifa hizo za kuwa Mbunge. Sifa hizo ni kuacha kuwa mwanachama wa cham cha siasa. Aidha, sifa za kuchaguliwa zimetamkwa katika ibara ya 67(1)(b) kuwa ili mtu awe Mbunge ni lazima awe na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa
Katika kumbukumvbu za Bunge lako tukufu, mnamo mwaka 2003, Chama cha United Democratic Party (UDP) kiwafukuza uanachama wabunge wake wawili ambao ni ndugu Danny Makanga pamoja na ndugu Erasto Tumbo. Matokeo yake, ofisi yako ilitambua hatua hizo na kuwaondolea ubunge wao kwa mujibu wa Katiba. Uchaguzi mdogo uliitishwa kuhusiana na majimbo waliyokuw wakitokea.
Mheshimiwa Spika, inasikitisha na inafedhehesha sana kwamba ofisi yako haijatutendea haki. Pamoja na kuwapo shauri katika Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu uamuzi wa Halmashauri kuu ya Taifa ya
NCCR – Mageuzi, bado hakuna amri yoyote ile inayokuzuia wewe kutekeleza majukumu yako kama mhimili mmojawapo wa dola.
Ni dhahiri kwamba kam ofisi yako ingezingatia kutenda haki katika suala hili, tayari ungelikwishamsimamisha ubunge ndugu David Zacharia Kafulila na kushirikisha taasisi za umma zinazohusika katika kusimamia na kuitisha uchaguzi wa jimbo Kigoma Kusini. Kuendelea kukaa na kutofanyia kazi suala hili muhimu Kitaifa, ofisis yako imesababisha mgogoro mkubw katika chama chetu na kuendelea kupandikiza chuki, fitina na majungu miongoni mwa wanachama, wapigakura na Watanzania kwa ujumla.
Mheshimiwa Spika kwa baruq hii, ni imani yangu kuwa ofisi yako itachukua hatua zinazostahili ili kulinda maslahi ya Chama cha NCCR – Mageuzi na kutoendelea kufedheheshwa na kudhalilishwa mbele ya Watanzania kama ilivyotokea leo.
Pamoja na salamu za Democrasia na Maendeleo.
Ndimi mtumishi mtiifu,
…………………………..
James Francis Mbatia
MWENYEKITI WA TAIFA.

Nakala: Mhe. Mizengo K.P Pinda (Mb)
Waziri Mkuu wa JAMHURI YA Muungano wa Tanzania
Na Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni,
S.L.P. 3021,
DAR ES SALAAM.
 
Another episode,najiuliza sana Mbatia bungeni atakuwa anasimama upande upi sasa,kwa vyovyote ni mbunge wa upande wa ccm
 
Ataunganaje na chama cha spika aliyekuwa anamlaani kwenye issue ya Kaka David kumwakilisha.Siasa ni tata
 
upinzani kamwe hauwezi kufa kwa kufuata sheria na kanuni tulizojiwekea, vinginevyo itakua ni fujo, Upinzani si kupindisha sheria ama kuvunja katiba.
 
Mbunge wa kuchaguliwa anawajibika kwa wapigakura wake na chama chake.
mbunge wa viti maalum anawakilisha chama chake.
Je mbunge wa kutoka chama pinzani kama Mbatia anapoteuliwa na Rais hua anamuakilisha( anawajibika ) kwa nani?
 
Hii barua ilivyoandikwa inatia mashaka. Any unsigned letter to me mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh!!! Tunatakaa pdf letter yenye sign ya Mbatia. Hii barua full spelling errors na kiswahili kisichonyooka. Kumbuka wachanga hawana l but r. Sasa wewe mchanga gani anaandika balua badala ya barua!!! Bado not conviced japo mambo mengi umeweka jinsi story zenyewe zilivyo. But anyway umefanya vema kutukumbusha mambo mazuri!!
 
Ukiwa mtu wa kupenda feva sharti usiwe na neno HAPANA mdomoni mwako! Ni wapi na kwa lipi mwenyekiti huyu anaweza kuiambia ccm hapana?
 
Back
Top Bottom