Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
JAMES Mbatia, Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha NCCR-Mageuzi, ametoa ushauri kwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa kujiuzulu ili kumfanya Rais wa nchi hiyo, Samia Suluhu Hassan kuunda baraza jipya.

Mbatia amesema, hatua hiyo itamsaidia Rais Samia kuunda Serikali yake.

=====

Ni baada ya Samia aliyekuwa Makamu wa Rais, kuapishwa tarehe 19 Machi 2021, kuwa Rais, kuchukua nafasi ya Dk. John Pombe Magufuli, kufariki dunia.

Dk. Magufuli, alifariki dunia tarehe 17 Machi 2021 na mwili wake kuzikwa Ijumaa ya 26 Machi 2021.

MwanaHALISI TV, limefanya mahojiano na Mbatia kuhusu mabadiliko hayo ya uongozi na jinsi anavyomfahamu Rais Samia na matarajio yake.

Kufahamu zaidi, fuatilia mahojiano yake.

NB:
TLS walisema Rais anatakiwa kuvunja Baraza la Mawaziri

Waziri wa Katiba na Sheria akasema Rais halazimiki kuvunja Baraza hilo.

Je, Mwanasheria Mkuu wa Serikali anasemaje kuhusu hili?

1616863871709.png
Source:
 
ha ha haa

Mbona president anayo mamlaka ya kuvunja Baraza?

Hapa Mbatia anataka tuone Rais na Waziri mkuu Wana mgogoro. Kwamba Rais anashindwa kuunda Baraza jipya kwa vile Waziri Mkuu Majaliwa hajajiuzuru.

Wapi Kikwete, za kuambiwa tuchanganye na zetu.
 
Majaliwa anatakiwa aonyeshe njia, anapaswa kujiuzuru ili kumpa nafasi mama Samia kuunda baraza lake la mawaziri.

Kitendo cha Majaliwa kung'ang'ania madaraka ni kitendo cha aibu kwa taifa na kinaweza kutoa ishara kuwa huenda Majaliwa ni mmoja ya wahusika wa lile genge lililohisiwa kuwa linataka kumpora mama madaraka ya kiti cha urais.

Majaliwa onyesha njia sasa.
Jiuzuru haraka iwezekanavyo.
 
Hivi mnafikiri ni Rahisi ki hivyo..!?
Madaraka matam bhanaa..
Majaliwa anatakiwa aonyeshe njia, anapaswa kujiuzuru ili kumpa nafasi mama Samia kuunda baraza lake la mawaziri.

Kitendo cha Majaliwa kung'ang'ania madaraka ni kitendo cha aibu kwa taifa na kinaweza kutoa ishara kuwa huenda Majaliwa ni mmoja ya wahusika wa lile genge lililohisiwa kuwa linataka kumpora mama madaraka ya kiti cha urais.

Majaliwa onyesha njia sasa.
Jiuzuru haraka iwezekanavyo.
 
Mama Samia kazi anayo hii nchi ina watu vichwa ngumu!
Sio vichwa vigumu bali ni wajuaji. Ndio maana ili utawale vyema ni muhimu kuwaziba midomo wapuuzi maana watakuyumbisha katika mission yako! Hiki ndio alikifanya Magufuli akaonekana katili ila dhamira ilikua njema kabisa.

Yani kuongoza Tanzania ni sawa na kufundisha darasa la wanafunzi 200 ukitarajia kutakuwa na hali ya utulivu na ustaarabu katika kuuliza maswali na majibu ila badala yake kila mtu ananong'ona na kuropoka ovyo bila utaratibu halafu kuadhibiwa hawataki.

Wana expect wafanyiwe ustaarabu ambao wao hawana, hao ndio watanzania bana.😁
 
Yani kuongoza Tanzania ni sawa na kufundisha darasa la wanafunzi 200 ukitarajia kutakuwa na hali ya utulivu ila badala yake kila mtu ananong'ona na kuropoka ovyo bila utaratibu halafu kuadhibiwa hawataki.
Yani wabongo wajuaji juaji na wambea ndio maana TISS wanafanikiwa kirahisi kugather intelligence information kwa umbea wa wabongo.
 
Majaliwa anatakiwa aonyeshe njia, anapaswa kujiuzuru ili kumpa nafasi mama Samia kuunda baraza lake la mawaziri.

Kitendo cha Majaliwa kung'ang'ania madaraka ni kitendo cha aibu kwa taifa na kinaweza kutoa ishara kuwa huenda Majaliwa ni mmoja ya wahusika wa lile genge lililohisiwa kuwa linataka kumpora mama madaraka ya kiti cha urais.

Majaliwa onyesha njia sasa.
Jiuzuru haraka iwezekanavyo.
Mbona mnamlazimisha sana wazee, mnataka mama abaki pekeake ili mumpelekeshe jinsi mnavyojiskia 😁😁😁!!?

Sasa kwa taarifa yenu atajiuzulu kisha atateuliwa upya acheni utoto!
 
Sio vichwa vigumu bali ni wajuaji. Ndio maana ili utawale vyema ni muhimu kuwaziba midomo wapuuzi maana watakuyumbisha katika mission yako! Hiki ndio alikifanya Magufuli akaonekana katili ila dhamira ilikua njema kabisa.

Yani kuongoza Tanzania ni sawa na kufundisha darasa la wanafunzi 200 ukitarajia kutakuwa na hali ya utulivu na ustaarabu katika kuuliza maswali na majibu ila badala yake kila mtu ananong'ona na kuropoka ovyo bila utaratibu halafu kuadhibiwa hawataki.

Wana expect wafanyiwe ustaarabu ambao wao hawana, hao ndio watanzania bana.😁
Safii
Hata ukivaa viatu vya Serikali unaona kabisa Wakati mwengine inawabidi wawe wakatili ili Mambo yaende

Maskini Nchi yangu
 
Back
Top Bottom