James Mbatia amkingia kifua Spika Ndugai, kwenda mahakamani kuzuia mchakato wa kutafuta Spika mpya

Mkuu Sexless , japo sijabahatika kuiona charge sheet, lakini Mbatia has a point.
1. Katiba imetoa maelekezo Spika akijiuzulu barua anapeleka kwa nani?. Hili halijufanyika!. Why?. Mahakama itajibu.

2. CCM ndio imeliarifu Bunge, na Bunge likakubali!. Who is mightier kati ya Bunge na CCM?. I thought enzi za party supremacy are over!.

3. Kuna watu wamezuiwa kugombea Uspika, wametajwa mawaziri, manaibu mawaziri na viongozi wengine wanaotajwa na katiba. Tulia kagombea bila kwanza kujiuzulu unaibu Spika, kasema Naibu Spika hatatajwa!.
Mahakama itajibu.
P
Asante Sana mkuu Pascal Mayalla
 
Matusi si uungwana. Tuangalie hoja ya Mbatia. Je katiba yetu inasemaje juu ya kujiuzulu kwa spika. Ni lazima atangaze hivyo ndani ya bunge mbele ya wabunge na Siwa au anaweza kujiuzulu hata kwenye banda lake la kufugia kuku?
Wacha kuunga mkono Malaya wa kisiasa!! Huyu Mbatia anaishi kwa kujipendekeza na kusaliti upinzani
 
Kwa majaji wa wadanganyika watatafuta vifungu ili kesi ionekane haina mshiko.badala ya kuangalia sheria inasemaje.but one day ukweli utajulikana
 
Kesi ya Mbatia dhidi ya Ndugai kusikilizwa Januari 26 mwaka huu.

SPIKA wa zamani wa Bunge, Job Ndugai ambae ni mdaiwa wa kwanza katika kesi ya kupinga kujiuzulu kwake iliyofufunguliwa na Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia leo Januari 24,2022 ameshindwa kufika katika Mahakama Kuu wakati kesi hiyo ilipokuja kwa kusikilizwa.

Kufuatia kutoonekana kwa Ndugai na wakili wake, Jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Iohn Mgeta akisaidiana na Jaji Masoud na Jaji BenHaji Sanya limeagiza kuwa mujibu maombi (Ndugai) apelekewe hati ya kuitwa mahakamani hapo mkononi kwa sababu awali wito huo ulitumwa kwa email.

Jopo hilo limesema hati hiyo ya kuitwa mahakamani, inatakiwa imfikie Ndugai kabla ya saa nane na nusu leo mchana.Pia, jopo hilo llmeagiza mdaiwa wa pili na watatu ( Bunge na AG) wawasilishe majibu yao ya kiapo kinzani mapema na kesi itasikilizwa Januari 26,2022 saa tano asubuhi.

Jopo hilo limetoa maagizol kwa kuzingatia hoja za upande wa mdai na mdaiwa na kufikia maamuzi hayo. Wakati pande hizo zinawasilisha hoja zao jopo la mawakili wa Serikali wanne likiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Mussa Mbura alidai kuwa hawakuweza kuandaa majibu ya kiapo kinzani kwa sababu hati ya wito wa kwenda mahakamani waliipata jioni.

Amedai, tukio la kujiudhuru Spika liitokea Januari 6,2022 na kesi imefunguliwa Januari 21,2022, kwa hiyo Mbatia walipata siku 14 za kuandaa kesi yao, kwa hiyo hawaoni kama kuna dharura , tunaomba siku 14 kwa ajili ya kujiandaa.

Jopo na mawakili wa mdai, likiongonzwa na Wakili Mpare Mpoki wamedai kuwa dharura ipo kwa sababu kuna kitu wanachokiwahi ambacho ni uchaguzi wa Spika usifanyike , kwa sababu akichaguliwa Spika kutakuwa na Spika wawili, jambo ambalo ni hatari.

Mpoki anadai kuwa, busara ya Mahakama inatakiwa itoke kabla ya Januari 31,2022 na ni Mahakama pekee ndiyo inaweza kusimamisha uchaguzi huo, hati ya wito walipewa wadaiwa ili leo kesi isikilizwe, kwa hiyo walitakiwa wandae kiapo hicho.

Mbatia alifungua kesi hiyo kwa madai kuwa kuna vifungu Ndugai hakuvifuata wakati anajiuzulu uspika.


ndug.jpg
 
Kesi ya Mbatia dhidi ya Ndugai kusikilizwa Januari 26 mwaka huu.
SPIKA wa zamani wa Bunge, Job Ndugai ambae ni mdaiwa wa kwanza katika kesi ya kupinga kujiuzulu kwake iliyofufunguliwa na Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia leo Januari 24,2022 ameshindwa kufika katika Mahakama Kuu wakati kesi hiyo ilipokuja kwa kusikilizwa...
Imbombo ngafu
 
Kweli duniani hukosi mtetezi.

Hawa jopo la mawakili wa Serikali wanne likiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu mara nyingi huwa wanashindwa kesi.

Ngoja tuone job akirudi kwenye kiti chake tutajua kuwa alitembea kijijini cha Bwana Yesu
 
Back
Top Bottom