James Mapalala; Rais Mwinyi alimfanya Kashaju kufa maskini ila tajiri wa watoto

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,368
Habar zenyu wanajamvi?

Nianze kwa kutoa shukrani za dhati kabsa kwa uongozi wa jf kwa kuniweka kolokoloni kwa siku nyinyi sana hakika nmeteseka na ninaidi kuto rudia kosa nililo lifanya.

Baada ya hapo niseme leo,nime bahatika kukutana na Mzee wetu James Mapalala na tulipokutana swali la kwanza alironiuliza ni kuhusu watoto wengi walio achwa na MJOMBA WANGU yeye alipenda kumuita mwanaharakatibmwenzake.

Nilimjulisha kuwa,watoto wake wapo tena mmoja wa kiume amemaliza chuo kikuu cha Dsm.

Ndipo nilipoona Mzee James Mapalala akishikwa na bumbuwazi kama kweli nikamwambia ni kweli.
Baada ya hapo akanipeleka kwenye Mkasa ambao nilikuwa siujui.

Alianza kwa kuniuliza swali,hivi kijana wangu unamjua Rais Mwinyi?nikamjibu ndio namjua ila nilizaliwa kwenye utawala wake, na sikuweza kuufahamu saa utawala wake.

Akacheka,akasema nyie watt wa siku hizi sjui mnakula nini yani wajua mtu akikuona anajua nimekutana na libaba lenye miraba minne lilizaliwa miaka ya 70 kumbe loh,anacheka kidgo.alafu anaendelea kunielezea.

Mjomba wako alikuwa rafiki yangu sanaa,tulifanya wote siasa nchini Tanzania kupitia vyama vya upinzani.

Ila alikuwa miongoni mwa vijana wa Tanzania waliopata fursa ya kwenda kusoma nje ya nchi miaka hiyo ya utawala wa Nyerere.

Aliporejea nchini Tanzania alikuta Nyerere kaisha toka madarakani na nchi inaongozwa na mzanzibari ambaye alikuwa ni Mzee Mwinyi sasa.

Bahati mbaya mjomba wako,hakupendezwa kabsa yule mzanzibar kwanza kuwa rais wa TANZANIA NZIMA.

Yeye na wenzake waliporejea Tanzania wakawa wamepata kazi za kuwa walimu katika shule za serikali.

Bahati mbaya sanaa, kipindi kile hata wale baadhi ya wanafunzi walikuwemo na mashushu.

Basi mjomba wako alikuwa mwalimu.mmoja mzuri sana wa siasa siku hiyo aliingia Darasani kufundisha katika kufundisha siasa na utawala akawa amemchora Rais wa wakati huo ubaoni na kuandika maneno ambayo yalionesha kumdhaki Rais.

Hayakuwa ya kumdhaki,ila mjomba wako alielezea jinsi alivyokuwa na elimu kubwa kuliko Rais wa wakati huo,lakini yeye yuko Darasani anafundisha alafu mwenye elimu Aliyosema ni ndogo yuko ikulu ya magogoni.

Basi ndani ya dakika 20 tu yule bwana alikamatwa na kuwekwa kizuizini katika ofisi za vijana wetu hapo karbu na kanisa la St peter ostabey.

Baada ya kutolewa ndani, alinyanganywa vyeti vyake vyote na hakuruhusiwa kufanya kazi pahala popote pale nchini na nje ya nchi.

Mjomba wako, KASHAJU akatangazwa kuwa alikuwa amemtukana Rais,alipo rudi kijijini babake yake nae hakumpokea alimfukuza kwa madai kuwa alikuwa ametangazwa kumtusi omukama.

Yuel bwana hakufanya kazi mpka utawala wa mwinyi ulivyokarbia kuisha akawaita ikulu na kuwasamehe yeye na wenzake ila yeye hakwenda kusameheana nae.

Lakini Rais mwinyi sasa akatangaza kuwasamehe ndipo alipo anza siasa na mimi miaka ya 1995 alinipokea mkoani Kagera pale nshamba akanitembeza vijiji vyote. Baadae aliungana na mrema wakapeleka NCCR mageuzi .baada e akaach siasa na kuomba kufundisha siasa mashuleni.

Moja ya shule aliyofundisha ni Makongo,baadae aliacha baada ya Mzee Kipingu kumwambia aandae Ripoti yeye alisema hawezi kutumwa na mtoto kama kipingu na ndevu zake zile.

Baadae akaenda Makongo Juu,ndiko na umauti ulimkuta.

Mungu amlaze kijana wangu mahala pema peponi. AMINA

JE uliwai kusoma historia ya James Mapalala?tukutane next wkend.
 
Kwani mzee mapalala amefariki, mbona leo mnaamuongelea sana humu
 
alijisemea Ndungai, wasomi wa nchi hii wakishapata elimu wanawaona wenzao 'mbuzi' tu!, nadhani chakujifunza kutoka kwenye hiyo story ni kuwa wanyenyekevu pale tunapo bahatika kupata elimu, mali au hata madaraka.
 
alijisemea Ndungai, wasomi wa nchi hii wakishapata elimu wanawaona wenzao 'mbuzi' tu!, nadhani chakujifunza kutoka kwenye hiyo story ni kuwa wanyenyekevu pale tunapo bahatika kupata elimu, mali au hata madaraka.
Huwezi kumkoti huyo.mgogo nikaona umasait yeye mwenyewe nadhan anaumwa simwelew mm
 
Back
Top Bottom