James Mapalala: Mwanzilishi wa mageuzi aliyeishia kwenye mikosi

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
james_mapalala.jpg

HARAKATI za mageuzi nchini zina historia ndefu, zikianza kabla ya uhuru ambapo wa wananchi kupitia vyama na vuguvugu za aina mbalimbali waliungana ili kuwaondoa wakoloni.

Hadi mwaka 1961 chama cha Tanu kilichokuwa kikiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere kilishinda uchaguzi na kuunda Serikali.Vyama vingine vilivyokuwepo ni pamoja na AMNUT, ANC na UTP.

Baada ya Mwalimu kuunda Serikali, alifanya mabadiliko kadhaa ambapo mwaka 1965 alifuta mfumo wa vyama vingi na kukifanya chama cha Tanu kushika hatamu za uongozi.

Mbali na kufutwa kwa mfumo huo, pia uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa asasi za kiraia ulidhoofishwa huku jumuiya mbalimbali za kiraia zikichukuliwa na kuwa jumuiya za Tanu.

Hata hivyo, hatua hiyo haikuwafurahisha baadhi ya watu akiwemo James Mapalala ambaye kwa wakati huo alikuwa ni mwalimu.

Mapambano yalipoanza
Akizungumza maisha yake hivi karibuni, Mapalala anasema aliamua kupambana na mfumo huo kutokana na ukandamizwaji wa haki za binadamu uliokuwa ukifanywa na Serikali tangu ngazi za juu hadi chini.

“Nilianza mapambano yangu rasmi mwaka 1968 wakati huo nikiandika makala katika Gazeti la Kiongozi wakati huo nikiwa naishi Tabora. Nilieleza kutoridhishwa na mateso wanayopata wananchi wakati huo ingawa kwa kweli Mwalimu Nyerere alikuwa na nia njema tu,” anasema Mapalala na kuongeza:
“Viongozi wa vijiji wakati ule walikuwa wakitesa wananchi na mimi niliandika kila kilichotokea.”

Kutokana na hali hiyo Mapalala alijikuta matatizoni na kufungwa jela katika gereza la Uyui na huo ulikuwa ni mkasa wa kwanza.

“Mkuu wa mkoa wakati huo akiitwa Makinda ambaye ni baba wa spika wa sasa, Anna Makinda, aliniweka jela.

Nilikaa kwa muda fulani hadi maaskofu na mashehe wa mkoa huo waliponihurumia na kumwandikia barua Mwalimu Nyerere kumwomba nitolewe,” anasema.

Anasema ombi hilo lilikubaliwa na Mwalimu Nyerere na hivyo kutolewa.
Hapo alifungua ukurasa mwingine ambapo kutokana na taaluma yake ya ualimu, aliomba na kupata kazi katika Shirika na la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) mwaka 1971.

“Nilitakiwa kwenda kufundisha Nigeria, hivyo nikaenda kuripoti kisha nikarudi ili niichukue familia yangu. Niliporudi, Jumapili moja nikiwa kanisani pale St. Peter, Oysterbay nikakutana na Nyerere akaniita na kuniuliza, ‘nasikia unataka kuondoka?’ nikamjibu ni kweli. Akaniambia nisiondoke kuna kazi atanipa, hivyo niripoti ofisi za Tanu pale Lumumba siku iliyofuata,” anasema.

Anasema siku hiyo alipofika ofisini hapo, aliwakuta maofisa wa chama ambao walimpangia kazi ya kununua na kuuza ng’ombe kutoka mikoani.

“Niliifanya kazi ile kwa shingo upande kwa miaka miwili kisha nikaiacha. Hapo tena ile kazi yangu ya Unesco ikaota mbawa,” anasema.

Anasema tangu wakati huo alianza kufanya kazi zake binafsi ikiwa ni pamoja na kuwa mkandarasi wa majengo ambapo anasema aliwahi kupata zabuni ya kujenga maghorofa ya bandari.

Hata hivyo anasema ilipofika mwaka 1983, mapambano yake yakaanza tena ambapo wakati huo kulikuwa na mkutano wa wanasheria jijini Dar es Salaam ambao pia walimkaribisha.

“Wakati huo kulikuwa na wanasheria kutoka katika Chama cha Tanganyika Law Society walinialika kwenye mkutano uliokuwa ukizungumzia matatizo ya demokrasia nchini. Walizungumzia matatizo ya mfumo wa chama kimoja, lakini hawakutoa suluhisho. Mimi nilipendekeza uanzishwe mfumo wa vyama vingi nchini,” anasema Mapalala.

Hata hivyo, pendekezo hilo halikutiliwa maanani hadi mwaka 1984 wakati Chama Cha Mapinduzi kikiwa na mkutano mkuu ambapo Mapalala alifanya tena ‘uchokozi’ wake.

“Mwaka 1984 nilimwandikia barua Mwalimu Nyerere wakati wa mkutano mkuu wa CCM nikimtaka kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi. Hapo ndipo matatizo yakaanza kwani niliwekwa kizuizini.

Nilikuwa nikihamishwa kutoka kituo kimoja cha polisi hadi kingine kwa karibu mwaka mmoja. Lakini sikufunguliwa kesi yoyote,” anasema.

Anaongeza kuwa mwaka 1986, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Muhidin Kimario alimkamata na kumfunga minyororo na kumpeleka kizuizini mkoani Lindi ambako alikaa hadi mwaka 1990 na wakati huo nilikuwa nikihamishiwa kisiwani Mafia.

Licha ya matatizo yote hayo Mapalala anasema hakukata tamaa na mawazo yake ya kuanzisha mfumo wa vyama vingi.

“Baada ya kutoka kizuizini, nilirudi tena na mawazo ya kuanzisha chama cha siasa. Nilikuwa na wenzangu ambapo tulianzisha chama wakati hakukuwa na sheria ya vyama vingi,” anasema na kuongeza.

“Hatukuogopa, tulikwenda kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, wakati huo Augustine Mrema na kumweleza haja yetu hiyo. Mrema alikuwa mkali sana akatufokea na kutufukuza.”

Baada ya kuona hivyo anasema waliamua kuandamana wakidai haki ya kuanzisha chama cha siasa,

“Tulikuwa watu 35 hivi, wakati maandamano yetu yanaanza. Tulipokuwa tukikaribia Kariakoo, watu waliongezeka na kufika hadi 1,000. Polisi wakaingilia kati na kuwakamata watu 25, mimi nikakimbilia Ubalozi wa Sweden kujificha.”

Anaendelea kusema kuwa, wale wanachama waliokamatwa na kupelekwa mahabusu waligoma kula kwa siku kadhaa na kuanza kuitisha Serikali.

“Ilibidi Serikali ije kuniomba niwasihi wale chakula. Ikabidi kitolewe chakula kizuri tena kutoka Kilimanjaro Hotel na kupelekwa gerezani na kuwabembeleza kula,” anasema.

Wakati mivutano hiyo ikiendelea, tayari kulishaanza kujitokeza mabadiliko ya kisasa na kiuchumi ulimwenguni ambapo mfumo wa ukomunisti ulianza kuanguka.

Kuanzisha, kufukuzwa CUF

Baada ya misukosuko ndipo walianzisha chama chao rasmi kikitwa Chama cha Wananchi (CUF) mwaka 1991.

Baada ya Serikali kupitisha sheria ya vyama vingi mwaka 1992, Mapalala anasema wanaharakati wengine wa mageuzi walikutana ukumbi wa Diamond Jubilee mwaka huo na kuanzisha chama cha NCCR-Mageuzi.

Hata hivyo, anasema mwaka huo kulikuwa na chama kingine huko Zanzibar cha ZUF (Zanzibar United Front) ambacho kilitaka kuunganisha nguvu na chama cha bara ili kiwe cha kitaifa.

“Walipokuja bara kuangalia chama chenye nguvu, wakaridhika na chama chetu na kuomba tuungane. Halmashauri kuu za vyama vyetu zikakaa kujadili suala hilo na hatimaye kukubaliana. Mwaka 1993 niliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CUF iliyoungana,” anasema.

Baada ya hapo anasema alifanya ziara katika mikoa karibu yote ya bara na Zanzibar kwa ajili ya kukitangaza chama hicho.

Hata hivyo, bahati haikuwa yake, anasema ilipofika mwaka 1994 mambo yakabadilika kwani wenzake hasa viongozi wa Zanzibar wakamgeuka na kuanza kumtuhumu kuwa anakisaliti chama.

Lakini mwenyewe anasema ilikuwa ni sababu za kidini pamoja na mkono wa Serikali uliokuwa ukiendelea kumwandama.

“Nilifukuzwa CUF kwa sababu za kidini tu. Ilikuwa mwaka 1994 baada ya kukijenga chama hicho nikashangaa mambo yamebadilika na viongozi wenzangu wamenigeuka. Wakawa wananishutumu kuwa natumiwa na CCM, mara nimechana bendera za chama, na tuhuma nyingi tu. Lakini nilipata hadi nyaraka zilizothibitisha sababu za udini,” anasema na kuongeza.

“Wakati huo CUF ilikuwa ikifadhiliwa na nchi za kiarabu, kwa hiyo wakasema ‘mtatakaje msaada wakati chama kinaongozwa na kafiri?’ Ndipo vituko vikaanza.

Lakini hata Serikali pia ilichangia, nakumbuka siku ya mkutano wa kunifukuza kule Tanga, Msajili wa vyama vya siasa wakati huo, George Liundi alikuwepo hadi saa tisa za usiku akishadadia kufukuzwa kwangu.”

Baada ya kufukuzwa Mapalala akaanza upya tena mikakati ya kuanzisha chama kingine. Hata hivyo ilimchukua muda mrefu hadi mwaka 2003 ambapo alianzisha Chama cha Haki na Ustawi alichonacho hadi sasa.

Tangu alipokianzisha alifanikiwa kupata diwani mmoja tu mkoani Mara mwaka 2005 ambaye hata hivyo hakuendelea baada ya kumaliza miaka yake mitano.

Mapalala anazungumzia pia tukio la kunyang’anywa nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya Morocco jijini Dar es Salaam kwa amri ya mahakama mwaka 2010, na kulihusisha na misukosuko aliyoipata katika harakati za kuleta mageuzi nchini.

“Hapa unapoona ninaishi kwenye mabanda ya ng’ombe, baada ya nyumba yangu kubomolewa kwa amri ya mahakama, yaani ni misukosuko tu. Chama changu kinanitegemea kifedha lakini kwa hali hii inaniwia vigumu kukisaidia,” anasema.

Anazungumziaje upinzani wa sasa?

Akizungumzia vyama vya upinzani vya sasa, Mapalala anasema kuwa vimejikita zaidi kwenye kutafuta madaraka badala ya kueleza sera zao kwa wananchi.

“Tofauti kati ya upinzani tuliokuwa tukiupigania miaka ile na wa sasa, ni watu kuwa na mawazo ya kwenda Ikulu tu bila kusema watawafanyia nini wananchi baada ya kufika huko.

Hata kwenye chama tawala, CCM, hali ni hiyo hiyo, watu wanalilia tu Ikulu. Sisi tunasisitiza sera tu… sera nzuri ndiyo zitakazouza chama, chema chajiuza kibaya chajitembeza,” anasema.
 
Aliponivunja mbavu ni pale aliposhindwa Kujua hadaa ya Nyerere, kutoka kukataa kazi ya UNESCO hadi kwenda kuuza ng'ombe! Kweli Nyerere alikuwa anajua jinsi ya kuwadhibiti waliokuwa wanaonekana kuleta upinzani! Yaani uende nje ukapate mbinu za kuendesha mapambano wewe, alifikiri Nyerere boya!
 
Namfahamu fika Mzee James Mapalala, sisi tulikuwa tukiishi Driver In Flats, Mafleti yeye akiishi Morocco pale Polisi walipojenga, ile 1984 aliandaa petition na kuipitisha home kwa dingi ili isainiwe, dingi alisaini, mtiti ulipoanza signatories wote wa ile petition cha moto walikipata!. Wanaomjua Nyerere jamani mwacheni tuu apumzike kwa amani!, Huyu Mwalimu alikuwa no nonsense man, hana mchezo kabisa! . Dingi aliopolewa na Murtaza Lakha alijenga hoja waliosaini hawakujua wana saini nini, ili jinai iwepo lazima kuwepo kwa actus reus na mens rea!
Wengine waachiwa Mapalala akaendelea kushikiliwa.
 
Cha kufurahisha ni kua wote waliomtendea ndivyo sivyo walishatangulia mbele ya haki wakamwacha na wengine afya zao ni dhoofu kweli.

Sijui unapomtendea binadamu mwenzio ndivyo sivyo hapa duniani unategemea nini, kisa cheo!
 
Namfahamu fika Mzee James Mapalala, sisi tulikuwa tukiishi Driver In Flats, Mafleti yeye akiishi Morocco pale Polisi walipojenga, ile 1984 aliandaa petition na kuipitisha home kwa dingi ili isainiwe, dingi alisaini, mtiti ulipoanza signatories wote wa ile petition cha moto walikipata!. Wanaomjua Nyerere jamani mwacheni tuu apumzike kwa amani!, Huyu Mwalimu alikuwa no nonsense man, hana mchezo kabisa! . Dingi aliopolewa na Murtaza Lakha alijenga hoja waliosaini hawakujua wana saini nini, ili jinai iwepo lazima kuwepo kwa actus reus na mens rea!
Wengine waachiwa Mapalala akaendelea kushikiliwa.
Msalimie sana Bernard mapalala

Ova
 
Hili la Udini CUF limewanyofoa nyadhifa Lwakatare na Mtatiro.
 
N
Aliponivunja mbavu ni pale aliposhindwa Kujua hadaa ya Nyerere, kutoka kukataa kazi ya UNESCO hadi kwenda kuuza ng'ombe! Kweli Nyerere alikuwa anajua jinsi ya kuwadhibiti waliokuwa wanaonekana kuleta upinzani! Yaani uende nje ukapate mbinu za kuendesha mapambano wewe, alifikiri Nyerere boya!
DA JK ALIKUWA NOMA SANA
Nimecheka sana
 
Namfahamu fika Mzee James Mapalala, sisi tulikuwa tukiishi Driver In Flats, Mafleti yeye akiishi Morocco pale Polisi walipojenga, ile 1984 aliandaa petition na kuipitisha home kwa dingi ili isainiwe, dingi alisaini, mtiti ulipoanza signatories wote wa ile petition cha moto walikipata!. Wanaomjua Nyerere jamani mwacheni tuu apumzike kwa amani!, Huyu Mwalimu alikuwa no nonsense man, hana mchezo kabisa! . Dingi aliopolewa na Murtaza Lakha alijenga hoja waliosaini hawakujua wana saini nini, ili jinai iwepo lazima kuwepo kwa actus reus na mens rea!
Wengine waachiwa Mapalala akaendelea kushikiliwa.
Sasa naamini mzee wako alikuwa mtu asiyejulikana Dah nimefurahi
 
Namfahamu fika Mzee James Mapalala, sisi tulikuwa tukiishi Driver In Flats, Mafleti yeye akiishi Morocco pale Polisi walipojenga, ile 1984 aliandaa petition na kuipitisha home kwa dingi ili isainiwe, dingi alisaini, mtiti ulipoanza signatories wote wa ile petition cha moto walikipata!. Wanaomjua Nyerere jamani mwacheni tuu apumzike kwa amani!, Huyu Mwalimu alikuwa no nonsense man, hana mchezo kabisa! . Dingi aliopolewa na Murtaza Lakha alijenga hoja waliosaini hawakujua wana saini nini, ili jinai iwepo lazima kuwepo kwa actus reus na mens rea!
Wengine waachiwa Mapalala akaendelea kushikiliwa.
Pascale ulishasoma kitabu kinaitwa Candid to my Country by anonymous writer? Kilielezea mambo mengi. Nilikisoma early 80s' Nahisi kiliandikwa na Mzee Mapalala. Kulikuwa na mama mmoja ambaye alikuwa ameolewa na mme mmoja ambaye alikuwa mpinzani, 1992 alibadili dini tena kurudi ukatoliki. Mwalimu, mama Maria na Mzee Ndejembi walihusika. Sisemi zaidi.
 
Namfahamu fika Mzee James Mapalala, sisi tulikuwa tukiishi Driver In Flats, Mafleti yeye akiishi Morocco pale Polisi walipojenga, ile 1984 aliandaa petition na kuipitisha home kwa dingi ili isainiwe, dingi alisaini, mtiti ulipoanza signatories wote wa ile petition cha moto walikipata!. Wanaomjua Nyerere jamani mwacheni tuu apumzike kwa amani!, Huyu Mwalimu alikuwa no nonsense man, hana mchezo kabisa! . Dingi aliopolewa na Murtaza Lakha alijenga hoja waliosaini hawakujua wana saini nini, ili jinai iwepo lazima kuwepo kwa actus reus na mens rea!
Wengine waachiwa Mapalala akaendelea kushikiliwa.
Kumbe uliishi flats za Drive in, kweli dunia ni ndogo.
 
Aliponivunja mbavu ni pale aliposhindwa Kujua hadaa ya Nyerere, kutoka kukataa kazi ya UNESCO hadi kwenda kuuza ng'ombe! Kweli Nyerere alikuwa anajua jinsi ya kuwadhibiti waliokuwa wanaonekana kuleta upinzani! Yaani uende nje ukapate mbinu za kuendesha mapambano wewe, alifikiri Nyerere boya!

Sasa, unadhani alikuwa na ujanja hapo? Si ajabu angekwama airport tu.Achana na mzee yule.
 
Alichofanya maalim Seif kwa mzee Mapalala ndio kinamtafuna na yeye
Lipumba anamfyekerea mbali
Malipo duniani
Lipumba mwenyewe si hao hao waarabu waliomtoa alikokua akagombee Urais? Udini mbaya; na ukabila pia huko Chadema.
 
Back
Top Bottom