James Mapalala: Mwanzilishi wa mageuzi aliyeishia kwenye mikosi

Wapinzani wa sasa hivi wanalia lia tu bila vitendo, hawa wa zamani sheria zilikuwa haziruhusu lakini wanafanya na wananchi wanawaunga mkono
 
Namfahamu fika Mzee James Mapalala, sisi tulikuwa tukiishi Driver In Flats, Mafleti yeye akiishi Morocco pale Polisi walipojenga, ile 1984 aliandaa petition na kuipitisha home kwa dingi ili isainiwe, dingi alisaini, mtiti ulipoanza signatories wote wa ile petition cha moto walikipata!. Wanaomjua Nyerere jamani mwacheni tuu apumzike kwa amani!, Huyu Mwalimu alikuwa no nonsense man, hana mchezo kabisa! . Dingi aliopolewa na Murtaza Lakha alijenga hoja waliosaini hawakujua wana saini nini, ili jinai iwepo lazima kuwepo kwa actus reus na mens rea!
Wengine waachiwa Mapalala akaendelea kushikiliwa.
Walishindwaje ku prove nia ovu ya mzee wako i.e. mens rea? Alikuwa hajui kusoma? Kama ni msomi atasaini kitu bila kuelewa maana yake? Mimi ningeweza ku prove both actus reus and mens rea early in the morning during the hearing session of the court
 
Mi nadhani sahihi HAKUANZISHA MAGEUZI, bali alikuwa moja ya waanzilishi wa chama cha CUF. Hicho chama hakikuleta mageuzi na hakuna mageuzi mpaka sasa, hivyo siyo sahihi kusema eti alianzisha mageuzi.
Mageuzi gani anayozungumzia mleta mada. Ameeleza vizuri na inaonekana vyama vya siasa vilianza kabla ya uhuru wa Tanganyika. Nisahihi kusema TANU ilileta mageuzi, kutoka utawala wa kizungu na kuleta utawala wa wazawa. Lakini vyama vingi vilipoanza, CUF haikuwa peke yake, na kama vyama vingi ndio mageuzi, basi ni sahihi kusema alikuwa miongoni mwa waanzililishi.
Fitina za watawala dhidi ya mahasimu wao, hazikuanzia kwake. Na hazikuishia kwake, ile ni roho ya ubinafsi tuliyonayo binadamu wote. Hakuna kati yetu anayetaka kunyang'anywa alicho nacho, iwe mke au mume, kiwanja, gari na ndivyo ilivyo kwa madaraka/vyeo huko maofisini.
Hata katibu tarafa hawapendi wapinzani wake, na hata wanaoteuliwa yaani vyeo vya kupewa hudhani wanawapinzani na utasikia nitapambana na wote wanaotaka kuniharibia. Hivyo Mzee Mapalala alipaswa apambane ashinde, lakini yeye alishindwa. Sasa iweje aonekane ni shujaa/hero wakati alishindwa?! Siasa ni vita ukiingia unaanza kupigana ndani na nje. Kuna kushinda vita na kushindwa, lakini sioni kwanini ushindwe halafu uwe shujaa/hero.
Mi naweza kusema Mzee James Mapalala alijaribu na aliweka historia hiyo ya kujaribu kama ilivyokuwa kwa kina Chief Fundikira, Kasanga Tumbo, Christopher Mtikila, Emanuel Makaidi, Alec Chemponda, Kambona na wengine wengi.
Mpaka leo kuna vyama vya siasa vinajaribu na havijaweza, chama pekee kilicholeta Mageuzi kilikuwa TANU, lakini vingine bado vinajaribu. Huo ni mtizamo wangu kulingana na mada iliyopo na muhusika alivyozungumziwa.
 
Mzee mapalala nae wakati mwingine haeleweki!
Ilikuwaje advct maira alimuingiza kingi!
Naona kiwanja chke watu wmeki subdivide sahv anatokea nyumaa ya obay police....
Wkt mwingine mzee huyu anajichanganya mwenyewe kwenye mambo anayofanya

Ova
 
Walishindwaje ku prove nia ovu ya mzee wako i.e. mens rea? Alikuwa hajui kusoma? Kama ni msomi atasaini kitu bila kuelewa maana yake? Mimi ningeweza ku prove both actus reus and mens rea early in the morning during the hearing session of the court
Enzi hizo ilikuwa ni kwa mwendo wa presidential preventive detention orders, hakuna kesi na kwa wengine hakuna hata kuambiwa kosa, wakati huo Nyerere, alionekana kama mungu fulani and no lawyer dared to challenge Mwalimu isipokuwa Murtaza Lakha, kwanza ndiye aliyemchomoa Mzee wangu kwenye Kesi ya Mauaji Mwanza, kisha kwenye hilo la Mapalala, alimchomoa kwa Habeas Corpus.
The signing sheet ya petition ilikuwa na majina tuu bila covering letter ni petition ya nini, Lakha akatumia legal technicalities na sio matters of law, dingi akachomoka haswa kwa kuzingatia kabla ya hapo alikuwa RSO wa Mwanza, hivyo it was easy.
P
 
Huyu Murtaza Lakha nilimfaidi kwenye kesi ya uhaini ya mwaka 1984! Wakati huo nilikuwa mdogo lakini nikisoma uendeshaji wa kesi hiyo kwenye magazeti ya Uhuru na Mzalendo. Kuna maswali alikuwa akimuuliza shahidi X hadi wakati nasoma kwenye gazeti nikawa naogopa!! Kama unavyosema enzi hizo ilikuwa hatari hata wakati unasoma gazeti unadhani wale jamaa wa co cabs wapo wanakuchungulia.

Kumbe mzee wako alikuwa na vi element vya kaupinzani ka Serikali ya Mwalimu. Naamini alisaini perition ile akijua wazi ilikuwa na maana gani kwa kuwa ex RSO hawezi kuletewa karatasi akasini bila kujua anasaini kwa ajili ya nini; huenda yangekuwa majina ya wanaojitolea kunyongwa angesemaje!!!!
 
Namfahamu fika Mzee James Mapalala, sisi tulikuwa tukiishi Driver In Flats, Mafleti yeye akiishi Morocco pale Polisi walipojenga, ile 1984 aliandaa petition na kuipitisha home kwa dingi ili isainiwe, dingi alisaini, mtiti ulipoanza signatories wote wa ile petition cha moto walikipata!. Wanaomjua Nyerere jamani mwacheni tuu apumzike kwa amani!, Huyu Mwalimu alikuwa no nonsense man, hana mchezo kabisa! . Dingi aliopolewa na Murtaza Lakha alijenga hoja waliosaini hawakujua wana saini nini, ili jinai iwepo lazima kuwepo kwa actus reus na mens rea!
Wengine waachiwa Mapalala akaendelea kushikiliwa.
Pascal hapa umeniacha njia panda. Ninavyoelewa Mzee wako Mzee Mayalla (May His Soul Rest In Eternal Peace) alikua mtu wa 'Kitengo" kwa ngazi ya RSO.

Kumbukumbu zangu zaniambia jambo lililomletea msukosuko mkubwa mpaka wenzake kufukuzwa kazi na kuishia mahakamani kama sikosei huku yeye akiponea kwenye tundu la sindano ni yale mateso waliyoyatoa kwa washukiwa wa mauwaji ya vikongwe walikokua wanashutumiwa na kutuhumiwa na wananchi kwa uchawi

Huo msukosuko alioupata kwa ku sign petition ya Mapalala ndio kwanza nausikia. Na kama Murtaza Lakha alihusika inamaana issue ilifika mahakamani. Sasa unaweza kutufungua macho zaidi maana kama jambo lilishawahi kua mahakamani sio siri tena

Wasiwasi wangu ni kua yawezekana marehemu Mzee Mayalla alikua anajua fika mchezo woote kuhusiana na hiyo petition ya Mapalala, na kwamba yeye kushiriki kwake ku sign alikukua yupo "kazini" kuhakikisha hilo halifanikiwi na kama usemavyo moto uliwaka na hatimaye wahusika wote kutiwa mbaroni. Hilo la Wakili Lakha kuwaokoa ilikua ni kiini macho tu

Mwalim Nyerere alikua bingwa na mahiri wa intelijensia. Aliwaficha watendaji wa kitengo kwa namna ambayo wengine hushiriki katika jambo fulani mwanzo mwisho lakini kumbe kuna wanaotafutwa. Siku hizi mambo yameparaganyika na kila mtu anawajua kuanzia mkuu wa kitengo, naibu wake viongozi hasa wa wilaya na watendaji wengine
 
Mkuu jamaa kasema mzee alitiwa ndani na Lakha akaenda mahakamani kuomba mtuhumiwa aletwe mahakamani kwa ile kitu inaitwa Habeus Corpus. Hii hutumika kuiomba mahakama iamuru mtu anayeshikiliwa na vyombo vya dola afikishwe mahakamani ili asomewe shitaka ama kama hakuna shitaka basi aachiwe huru.
 
Oooh hapo sawa mkuu ingawa pia kipindi hicho sheria ya Presidential Preventive Detention Order ilikua in force na pia kama kweli Mwalimu angekua amejiridhisha pasiposhaka uhusika wa ex spy wake kwenye hiyo petition Lakha angepata tabu sana kumchomoa
 
Hao ndio wanamapibduzi wa kweli. Akina mbowe ni untivirus wa mageuzi
Mbowe ndio mwana mageuzi aliyefanikiwa kupita wote.Fundikira , Mtikila na Mapalala hawakuwa na msukumo katika saisa za nchi. Ata Mrema ni sufuri.Mbowe kupitia kambi maalumu ya upinzani ameweza kuibana serikali na kuchochea maendeleo.Bila upinzani kamwe hatuwezi kupata maendeleo Chanya.Nyerere alitawala bila upinzani kwa miaka 30 na hatukupata maendeleo yoyote.
 
Hawa wa Kanda ya ziwa huwa wanafafana wakiongoza nchi huwa masikini sana,wanachukia matajiri, wana nyota za kimasikini,nyota za kushindwa kwenye uchumi,naona kombe lisiwe linaenda huko.
 
Mapinduzi gani ya kweli aliyofanya Mapalala?!Au hilo neno Mapinduzi halina maana yoyote kwako?!
Mkuu huwezi kuongelea harakati za mageuzi katika nchi hii ukaacha kuwataja watu kama akina Mzee Kasanga Tumbo, Mzee James Mapalala na Mzee Chifu Fundikira. Hawa wamekuwa wanamageuzi tangia miaka ya 60! Kassanga Tumbo amefariki akiwa ni mwanamageuzi.
 
Mageuzi ya nini?! Wamegeuza nini?! Siasa za vyama vingi haukuwa utashi wao binafsi bali ni KATIBA ya nchi. Hao uliowataja ni wachache waliochangamkia fursa hiyo.
Si wabezi ila nakataa kuwaita wana mageuzi. Majina mazuri ni waasisi wa vyama vyao.
 
Back
Top Bottom