James Lembeli atoboa siri kuhama CHADEMA na kurudi CCM

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
1073040

Mbunge wa zamani wa Kahama, James Lembeli amesema alihamia CHADEMA kujibanza tu ila kurudi CCM kulitokana na kushauriwa na Rais Magufuli na familia yake.

Akizungumza kwenye kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV amesema kuwa tangu aliporejea CCM amekuwa mtu mwenye amani na furaha.

"Rais Dkt. John Magufuli alikuwa kwenye ziara Kahama nilikwenda kwenye mkutano wake wananchi wakaniambia nirudi nyumbani, lakini pia Rais aliniambia nirudi tuijenge Tanzania, nikaamua kurudi, nilikwenda CHADEMA kujibanza kwenye mvua," amesema.

Amendelea kwa kusema, 'Mama yangu anaheshimika sana, kuhama kwangu CCM ilimkwaza sana aliniambia chama ambacho baba yako alikipigania wewe umeondoka, akaniambia nirudi kwa sasa nina amani na furaha,'.

Alipoulizwa ni kwanini kwa sasa hivi amekuwa kimya kwenye siasa za Tanzania, alijibu, 'Nimekuwa kimya kwa sababu za harakati za maisha zamani ilikuwa rahisi kuniona kwa sababu nilikuwa kwenye siasa kwa sasa nipo Kahama nafanya shughuli zangu" James Lembeli, Mbunge wa zamani wa Kahama'.
 
Nikikumbuka zile drama zake alipokuwa eti anahamia chama kinachojizika.. nacheka tu haswa siku moja alipokuwa stejini 🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Ukae utulie sasa Mzee.. tusumulie basi pia juu ya chama cha familia..
 
Mwanasiasa wa kitanzania katika ubora wake wa kufikiria kwa tumbo badala ya akili zake. Ni Tanzania tu unaweza mpata professor Lipumbavu

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Hapo ana watoto na watoto wana watoto Yaani kiufupi anaitwa baba, babu na mme................. kweli ?
 
Kinachojulikana na kilichosemwa kwenye mkutano wa hadhara mh Rais alipotoa ushauri kwa Lembeli kurudi CCM, Lembeli alikataa hapohapo, Lembeli awe mkweli na aseme ukweli wake kuwa misalaba ya upinzani imemshinda kwa kuwa unapoamua kubeba misalaba ya upinzani unatakiwa uvumilie na mijeredi yake inayoambatana na misalaba ya wapinzani wanayochapwa na CCM.
 
Wapo watu wengi ambao wanatamani sana kurejea CCM, ila wanaogopa kuchekwa. Suala kubwa hapa ni kumuunga mkono Rais MAGUFULI kwa ngivu zote ili kulijenga taifa

Watu wanarudi kujiunga ccm ili wawe salama kwenye mali zao. Na wanajua ukiwa upinzani ni hatari kwa shughuli zako, huruhusiwi kufanya siasa na hata risasi ni nje nje. Hawarudi ccm kwenye siasa bali kusaka usalama.
 
View attachment 1073040
Mbunge wa zamani wa Kahama, James Lembeli amesema alihamia CHADEMA kujibanza tu ila kurudi CCM kulitokana na kushauriwa na Rais Magufuli na familia yake.

Akizungumza kwenye kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV amesema kuwa tangu aliporejea CCM amekuwa mtu mwenye amani na furaha.

"Rais Dkt. John Magufuli alikuwa kwenye ziara Kahama nilikwenda kwenye mkutano wake wananchi wakaniambia nirudi nyumbani, lakini pia Rais aliniambia nirudi tuijenge Tanzania, nikaamua kurudi, nilikwenda CHADEMA kujibanza kwenye mvua," amesema.

Amendelea kwa kusema, 'Mama yangu anaheshimika sana, kuhama kwangu CCM ilimkwaza sana aliniambia chama ambacho baba yako alikipigania wewe umeondoka, akaniambia nirudi kwa sasa nina amani na furaha,'.

Alipoulizwa ni kwanini kwa sasa hivi amekuwa kimya kwenye siasa za Tanzania, alijibu, 'Nimekuwa kimya kwa sababu za harakati za maisha zamani ilikuwa rahisi kuniona kwa sababu nilikuwa kwenye siasa kwa sasa nipo Kahama nafanya shughuli zangu" James Lembeli, Mbunge wa zamani wa Kahama'.
Zee zima halioni aibu kusema linashikiwa akili na mwanaume mwenzake?

Sent using Jamii Forums mobile app
Huo ndio mfano dhahiri wa wanaccm. Umewahi ona wapi MTU anahama chama mbadala, anakitukana weee kisha anarudi tena?
Lakini ccm watu wanahama wanatukana weeeee, Mara chama cha nyeti za kuku nk lakini wakurudi wana pokewa kama wafalme na ndio utajua ni chama cha misukule.
Wabishe kidogo hapa kuwa wao sio misukule tuwape mifano halisi, wanyooshe tuu mkono waone!

Chama Cha Majuha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baba yake ndiyo nani,kwanza hayupo hata kwenye historia ya HARAKATI ZA UKOMBOZI.
Mwalimu Nyerere alisema MBOGAMBOGA si baba wala mama yake,na alikuwa tauari kuondoka,iwe Lembela?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lembeli kama hajalitaja jengo lake lenye Kahama FM kutaka kupigwa mnada kama sababu kuu ya yeye kurudi ccm basi ni muongo
 
Labda sijaelewa kitu hapa. Kwamba kujibanza kwake kule CHADEMA nani sasa alikuwa mvua aliyoikimbia? JK?
 
Mtu na mvi zake mpaka kwenye meno anajiunga chama cha siasa kwa msimamo wa mama yake.....
Wonder shall never end...
Sijui mke wake anamchukuliaje
yule hata akiambiwa na mama yake chepuka mwanangu kwani hata baba yako alikuwa anachepuka atachepuka,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom