Uchaguzi 2020 Jambo wanalopaswa kufahamu CHADEMA, ni kwamba muda wa kufanya siasa za kistaarabu umekwisha

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,581
11,658
Rais wa CCM na CCM yake, na polisi wake na wateule wake na vyombo vingine vya kisheria na dola, hawaamini katika demokrasia. Wao wakisikia Chadema wanachukulia kama ni waasi au magaidi. Kwa hiyo wanapambana kwa njia zote zisizo za kidemokrasia, bila kujali dhuluma wanayofanya kwa wananchi wanaotumia muda wao mwingi kwenye kwenye mikutano ya kampeni na kwenye foleni, wakisubiri kupiga kura. Mbaya zaidi, CCM wako tayari kufanya mauaji kwa viongozi na wafuasi wa Chadema, tena wakishirikiana na vyombo vya dola na viongozi wa serikali ya CCM.
Jambo wanalopaswa kufahamu Chadema, ni kwamba muda wa kufanya siasa za kistaarabu umekwisha.
Sikuwahi kukubaliana na wanaosema Watanzania hatuwezi kuheshimiana kwa sababu hatukuwahi kumwaga damu wenyewe kwa wenyewe, lakini sasa nakubaliana nawo. Sihamasishi kumwaga damu, lakini nakubali kwamba dhuluma inafanyika kwa sababu hatuheshimiani, na hatuheshimiani kwa sababu hatujatoana damu.
Dhuluma wanayofanyiwa Chadema itaendelea, kama wao wataendelea kusubiri siku ambayo CCM watakubali kukaa mezani, hiyo siku haiwezi kutokea. Hakuna mazungumzo kati ya mtu anayepoteza (looser) na mtu anayefaidika (beneficiary). Mazungumzo na suluhu vitakuja vyenyewe ikiwa wote mnapoteza.

Kila kukicha tunasikia kiongozi wa CDM amechinjwa, mara amepotea, mara amekatwa katwa mapanga na kutupwa mtaroni, mwingine ametiwa ndani kwa amri ya mkuu wa wilaya, wengine wanachomwa visu....hatusikii wa CCM wakifanyiwa hayo. Kwa hali hiyo, hakuna suluhu, kwa sababu anayepoteza (CDM) analialia, mnufaika (CCM) anafurahi. Lakini kama wote watalia, suluhu itakuja bila kuitwa.

Jambo wanalopaswa kufanya Chadema ni kujiandaa kifedha na kiintelijensia kabla ya 2020, la sivyo hawatapata jimbo hata moja.
Kujiandaa kifedha ni rahisi kuliko kujiandaa kiintelijensia. CCM hawana intelijensia zaidi ya kutegemea vyombo vya kiserikali. Lakini kama Chadema itawekeza kiuhakika kwenye intelijensia, ni Jeshi la wananchi pekee ndio litaweza kuidhibiti. "Jeshi" tu ndio chombo cha kogopa, na kuheshimu kiasi.
Idara ya usalama imejaa 'corrupts' na 'ignorant'. Wachache wanaojitambua hawawezi kufanya ujinga wa CCM, na hata wakirubuniwa hawawezi kufanya ujinga wa CCM kwa ufanisi wa kutosha. "Mtu anayefanya kazi kwa kurubuniwa au kulazimishwa hawezi kuifanya kwa ufanisi wa kutosha".
Zaidi wanaojitambua ndani ya vyombo vya dola, watakuwa radhi kutoa ushirikiano kwa Chadema kuliko CCM.
Na kwa hiyo, Chadema ikitaka kuunda intelijensia imara, itahitaji watu wa kujitolea. Ogopa mtu anayejitolea kupambana. Lakini pia anayejitolea anaweza kuwa 'ametumwa'.
Anyway! Jambo la msingi ndio hilo, kujiandaa. La sivyo, hakuna jimbo litaenda Chadema mwaka 2020. Kwanza hakutakuwa na uchaguzi zaidi ya vituko, na kama kweli Chadema wanataka kuirudisha nchi kwenye mstari, ni vema kujiandaa na vituko hivyo. Haipaswi hata kidogo kusubiri "Rais Mstaarabu" ili kupambana, hapana. Anayestahili "kupigwa" ni mtu asiye na ustaarabu. Mwaka 2020 unapaswa kuwa mwaka wa kukomesha vitendo visivyo vya kistaarabu tunavyofanyiana watanzania wenyewe kwa wenyewe. Na njia pekee iliyobaki ya kukomesha vitendo visivyo vya kistaarabu, ni kuwafanyia hao wahusika, vitendo visivyo vya kistaarabu.

Msimamizi anayetangaza matokeo ya uongo, halafu akaendelea kuishi kwa raha mustarehe, atarudia tena.

Mkuu wa polisi anayetuma polisi kutishia watu, kupiga raia na kusaidia CCM, akiachwa aendelee kula maisha kwa raha mustarehe, atarudia tena.

Kila kiumbe kinachofanya ujinga, kikaachwa kiendelee kuishi kwa raha mustarehe, kitarudia ujinga wake.

Kiongozi wa tume ya uchaguzi anayetumiwa na CCM kudhulumu demokrasia akiachwa aendelee kula maisha, atarudia tena.

Hao, wanatakiwa kukomeshwa, ili iwe funzo kwao na kwa wengine wenye tabia kama zao, na iwe funzo kwa anayewatuma.
Ukitaka kuua Nyoka, kata kichwa, ukishindwa, kata hata mkia, uwezekano ni kuwa atakimbia lakini tayari umempumguzia nguvu.

Nani mwenye uwezo wa kuwakomesha, bila kujiingiza katika mgogoro wa kisheria? Ndio hapo pa kuandaa intelijensia imara. Lawama ni bora kuliko fedheha, na katika hili anayestahili lawama ni CCM, na fedheha ni kwa Chadema. Mwaka 2020, Chadema ni vema walaumiwe kuliko kufedheheka.

Hata hivyo viongozi wakubwa wa Chadema hawapaswi kujiingiza katika hayo, kwasababu watakamatwa na kufungwa mara moja.
Na sisi wengine, tu waumini wa ubinadamu, ni rahisi zaidi kuachana na siasa kuliko kufanya hayo, hatuwezi hayo.

mr mkiki.
 
Kwani lini Hawa Malofa waliwahi kufanya Siasa Za kistaarabu?

Umesahau matusi Yao Kwa Rais Muungwana Kwa Kuwa tu alikuwa mstaarabu?

Sasa hivi wamepoa Kwa uoga Sio Kwa sababu ya ustaarabu wala hikma

Fursa ya kufanikiwa wameipoteza 2005-2015 Sasa hivi wavute subira Kwani Mvumilivu Hali mbichi
 
Hivyo Chadema ni chama cha upinzani? Hivyo Chadema ina Demokrasia? Acha mawazo potofu, mawazo yenye hoja za kubuni zisizo za msingi. Usitoe hoja za kubuni, za hisia zilizochoka. Tulia mzee unalialia ili uhurumiwe? Subiri kipigo kingine kinakuja hivi karibuni.
 
Haipaswi hata kidogo kusubiri "Rais Mstaarabu" ili kupambana, hapana. Anayestahili "kupigwa" ni mtu asiye na ustaarabu.
Kila kiumbe kinachofanya ujinga, kikaachwa kiendelee kuishi kwa raha mustarehe, kitarudia ujinga wake.
Hao, wanatakiwa kukomeshwa, ili iwe funzo kwao na kwa wengine wenye tabia kama zao, na iwe funzo kwa anayewatuma.
Ukitaka kuua Nyoka, kata kichwa, ukishindwa, kata hata mkia, uwezekano ni kuwa atakimbia lakini tayari umempumguzia nguvu.
Mkuu mr mkiki kwa hoja hizi inaonekana wewe unachochea vita itokee kati ya CHADEMA na Serikali ya CCM. Hii ni hatari sana ndugu kama imefika mahali mtu unaweza kuandika uzi wa kishari shari kama huu basi hali ni mbaya. Mkuu fahamu kwamba Serikali yoyote ile duniani haiwezi kukubali kirahisi kufanyiwa hujuma unazozipendekeza wewe na halafu ikakaa kimya tu bila kuchukua hatua.

Kuwa makini sana na vitu unavyoandika maana "shari" huzaa "shari". Ushauri wako kwa CHADEMA utawaletea matatizo makubwa kuliko suluhisho.
 
82 Reactions
Reply
Back
Top Bottom