Jambo Usilolijua: Nyerere alipokea Taifa la namna gani? Mpango wa Kwanza wa Maendeleo 1961

UNCONCIOUSLY umeunga mkono hoja ya mwanzisha uzi kwa hoja nzito tuu!!!
RED: Inajieleza yenyewe vizuri
BULUU: Imagine challenge/mzigo uliokuwepo
KIJANI: Maana haswa ya kiongozi. Iliondoka na Sokoine na mwishowe Nyerere mwenyewe. Sijui kama itazaliwa tena!
ZAMBARAU: Contrast iliyopo kati yake na hawa "wapole" na "wasikivu" waliopelekea magenge ya wanyang'anyi kuhamia ikulu na kuwa ndio source ya inputs
Nyerere alikuwa na muda kuchange plan zote za economic, pale tu alipoona hazina maendeleo na Taifa. Kwa mfano, plan yake ya agriculture ilkuwa ni kuwahamisha Wananchi kwa nguvu, na kuwapeleka vijijini bila ya mpango maalum wa maendeleo. Utalima vipi wakati huna maji? nyenzo muhimu za kilimo, nk.

Pili, huwezi kusema kama Nyerere libebeshwa mzingo mkubwa wakati ni yeye mwenyewe Nyerere ndiyo alikuwa anataka kuimplement kila law ya nchi. Viongozi wengine hawakuweza kuinput chochote kwa Nyerere, kutokana na ubabe aliokuwa nao.
 
Nashukuru sana mkuu kwa taarifa muhimu kama hii, nimepitia kwa kweli hakuna blah blah , ni maendeleo na misingi ya mafanikio.
 
This is impossible!! You???

Mwanakijiji,

Nilishasema jina la Nyerere litajwapo wengi tu linawasumbua na wataibuka from nowhere! Brazamen!

Any tupatie nyanga. Ila nadhani unawakera sana na mipango "yao" na unawafanya wasilale

BTW una records zozote za Nyerere kwenda Malaysia pia?
 
Mwanakijiji kwa mara nyingine tena umewaweka mahala pao wale wote wenye kubeza mchango wa Mwalimu JK kwa taifa letu.

Uk 47 sec 8: Imenigusa maana leo Tanesco wamechukua umeme na bado wamekalia ma IPTL, SONGAS, RICHMOND, DOWANS na SYMBION ili kuganga njaa zao wakati hawa wazee wetu wanaotukanwa leo walikuwa na akili ya kujenga mradi wa Hale ili kupunguza utegemezi wa mafuta nakuokoa pesa za kigeni.

Nyerere alikuwa kiongozi kwa viwango vyovyote utakavyoweka (uwe bepari au mjamaa); bahati mbaya sana amefuatiwa na watawala wenye kukimbilia Ikulu huku hawana ndoto wala maono ya nini wafanye wakishafika ikulu.

Moja ya laana anayoweza kuipata mwanadamu ni pale atapomdharau mzazi wake aliyejinyima ili mtoto apate fursa ya maisha bora. Kina Nyerere walikuwa na hiari ya kuwa mafisadi lakini walichagua kujinyima ili kina Sam Sita, Lipumba na wengineo wasome. Si halali mbinguni wala duniani kuonyesha dhihaka kwa kiongozi wa kiwango cha Nyerere.
 
Nyamba usiwe na shaka, siku chache zinavyokwenda nitaweka hata barua za mawasiliano kati ya Kennedy na Nyerere.. nadhani unachosema kina ukweli sana.

Ila wewe Mzee lakini, una jambo unawatafua "hao". Hawajakubeep tu?

Thanks kwa nyanga, tumetoka mbali ila tuendako mh!
 
MMM Heshima mbele!
Sikuwepo enzi hizo lakini kwa habari chache nilizozikia na kuzisoma nilim-admire Mwalimu,lakini katika 'documentary' zako (kumhusu Mwalimu) za hivi karibuni zinazidi kunifanya niamini kwamba pamoja na mapungufu ya kibinadamu, hatujapata kiongozi wa aina ya Mwalimu.Na haya maandiko unayoyatoa naamini hawakutaka yatoke kwa umma hata kidogo..

Wacha niendelee kuupitia huu mpango...
 
MKJJ angalia usalama wako!

Hii plan inatofautisha sana kati ya wachapakazi na wachapa domo.

It is genuine no blah blah!



MKJJ kwani umesoma development plan ya Kikwete iliyotolewa juzi juzi?? tafadhali jibu hili ASAP......jibu yes or no!!!
 
Mwanakijiji naomba kutanguliza shukrani zangu kwa hii taarifa! Tunaugulia machungu ya kukatika umeme, nitaprint hii kitu umeme, ukirudi, niipitie kwa undani. Thanks once again!
 
MMM ahsante sana....and this is the best so far kwa sisi wa vizazi ambavyo havikushuhudia zama hizi...some people are just talking lakini hawatoi mielekeo sahihi kama ya aina hii

Ombi binafsi: Kuna ile second 5 yrs dvpt plan, Je tunaweza kuipata ukatupakulia hapa pia? Nimerjaribu fuatilia kama ilivyokuwa hii ya first 3 yrs dvpt plan bila mafanikio zaidi ya kupata za kuunga unga tu

Thanks and keep us informed
 
MKJJ angalia usalama wako!

Hii plan inatofautisha sana kati ya wachapakazi na wachapa domo.

It is genuine no blah blah!

MKJJ kwani umesoma development plan ya Kikwete iliyotolewa juzi juzi?? tafadhali jibu hili ASAP......jibu yes or no!!!

I like your post Engineer...

Nyongeza tu: Ningependa itokee zote ziambatanishwe ....ile First and Second Development Plans za Nyerere na hizi za sasa za Mkwe.re then tupime rasilimali tulizonazo sasa na za wakati ule alafu tuone kipi kiko kwenye position na muelekeo wa kimaendeleo zaidi ya porojo na ku-please wananchi tu kwa matumaini hewa
 
wengine wanasema eti kama mzalendo arudi hapa ...lakini hao waliopo hapa ndiyo wanafanya madudu yote na hata wakiambiwa hawataki kabisa kusikia. Sasa sijui MMJ akisema 1+1=2 akiwa huko ndio akija hapa itabadilika!? Ukweli ni Ukweli tu!
Mzee mwanakijiji nakupongeza sana kwa taarifa zako nzuri. Wewe ni mzalendo na mpenda nchi.....
 
hapa ndipo matatizo yote ya nchi hii yalipolala. ACTION ...VITENDO!!!! Nimemuona waziri Nyarandu jana kabanwa na Mh. Tindu Lissu, kaishia kutetea pumba zao kwa kutoa mfano wa USA wanavyosamehe kodi kuvutia uwekezaji, TZ na US wapi na wapi?. Cha kusikitisha budget/mswada umepita wakati kuna budget nzuri sana wa Mh. Zitto imekuwa imekataliwa!
Tuanzie wapu kutekeleza vinavyotekelezeka na kuacha upupu huu??
Kwa nini tusiiadopt sasa?
 
Mwanakijiji kwa mara nyingine tena umewaweka mahala pao wale wote wenye kubeza mchango wa Mwalimu JK kwa taifa letu.

Uk 47 sec 8: Imenigusa maana leo Tanesco wamechukua umeme na bado wamekalia ma IPTL, SONGAS, RICHMOND, DOWANS na SYMBION ili kuganga njaa zao wakati hawa wazee wetu wanaotukanwa leo walikuwa na akili ya kujenga mradi wa Hale ili kupunguza utegemezi wa mafuta nakuokoa pesa za kigeni.

Nyerere alikuwa kiongozi kwa viwango vyovyote utakavyoweka (uwe bepari au mjamaa); bahati mbaya sana amefuatiwa na watawala wenye kukimbilia Ikulu huku hawana ndoto wala maono ya nini wafanye wakishafika ikulu.

Moja ya laana anayoweza kuipata mwanadamu ni pale atapomdharau mzazi wake aliyejinyima ili mtoto apate fursa ya maisha bora. Kina Nyerere walikuwa na hiari ya kuwa mafisadi lakini walichagua kujinyima ili kina Sam Sita, Lipumba na wengineo wasome. Si halali mbinguni wala duniani kuonyesha dhihaka kwa kiongozi wa kiwango cha Nyerere.

... iko comment humu ndani ya JF kwamba wanaoendelea kuharibu Tanzania ya Mwalimu (RIP) ni pamoja na wale walioandamana kupinga JKT wakati ule. Otherwise, inasemekana kwamba wapo waliocharazwa viboko na Mwalimu na jamaa hao hao ndio vinara wa kuitafuna nchi hii sasa hivi as if to avenge their two year stint in JKT. Nafurahia sana article moja ya Jenerali Ulimwengu (RAI enzi zile) alipotumia msamiati wa Kihaya kuwaelezea jamaa hao ambao kwa kifupi mtazamo wao unaweza kufananishwa na kupendelea sana mapilau, mawali, mahela mengi, .. etc ili mradi kwao kila kitu kiwe in big quantities na extravagance.

Kudos MKJJ for the document.
 
Mkuu MM


I am down with this threat..


over the recently umekwua msaada sana..


Hii ndiyo JF tunayoitika...


Keep It up...
 
Unaweza kusema labda kwa vile enzi hizo kulikuwa na Wazungu kwenye Serikali ya Mzee ndo maana hata mipango ilikuwa imekaa vizuri! Sasa hawa akina M-Kula wetu wamekalia kula tu wakija na mipango yao utafikiri haikupangwa na wasomi! Aibuuuuuuu!!!

TZ Bila kuwatoa kafara hawa CCM hatutachomoka hapa tulipo!!
 
View attachment 32526

Mojawapo ya hoja ambazo hatuzikii mara nyingi kwa wale ambao wanambebesha Nyerere lawama na mzigo wa taifa letu kuwa ni yeye ndiye aliyelivuruga ni kuwa Nyerere alipokea taifa lenye hali gani ile Disemba 9, 1961. Tunapoelekea miaka hamsini ya Uhuru wa Tanzania bara na hasa baada ya kupitishwa kwa mpango wa "nane" wa maendeleo chini ya serikali ya CCM ni vizuri kurudi nyuma kabisa tuone tulipoanzia.

Wiki iliyopita niliwaletea sehemu tu ya mapokezi ya Rais Nyerere Ikulu ya Marekani wakati huo chini ya Rais J. F. Kennedy. Mkutano wao ulikuwa ni mwaka 1963. Hata hivyo kabla ya hapo viongozi hao wawili walikuwa na mawasiliano ya karibu sana. Kuelekea Uhuru serikali chini ya Nyerere ilikaa na kuandaa mpango wa miaka mitatu (ambao ndio mpango wa kwanza wa maendeleo) wa taifa huru. Mpango huu ulikuwa na mambo mengi na ulikuwa na lengo moja tu nalo ni kujaribu kuleta taifa hilo changa katika karne ya ishirini.

Uzuri wa mpango huu unatupa mwanga wa hali ilikuwaje 1961 katika Tanganyika na mzigo mkubwa ambao Nyerere alibebeshwa na wananchi wenzake. Tunapojaribu kumhukumu leo hii kuwa aliiacha nchi katika "hali mbaya" - kitu ambacho si cha kweli - ni lazima tujaribu kujibu swali pia nchi aliyoipokea ilikuwaje? Changamoto za taifa changa hilo ilikuwaje (wengine wanafikiria hali ilivyokuwa Dar ndivyo ilivyokuwa mikoani). Hivyo kwa kupitia mpango huu utaweza kupata mwanga kidogo wa hali yetu ya kiuchumi ilikuwaje, kijiografia ilikuwaje na raslimali watu ilikuwaje.

Ukishapitia mpango huu swali moja ni LAZIMA ujiulize: Watendaji wa kutekeleza mpango huu walikuwa watoke wapi? Na je walikuwepo?

Wiki ijayo, inshallah tutaangalia nyaraka za CIA kuhusu Nyerere. Yote hii ni katika kuelekea kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika. Please do Enjoy. Kama umepitia mpango "wao" wa maendeleo wa miaka mitano unaweza kulinganisha kitu ambacho naweza kukiita 'motivation' ya mipango hii miwili ni nini. Only then you'll glance (like from a far) the thinking and making of a great leader. Kumbuka hakukuwa na MKUKUTA wala MKURABITA kabla yake.

NB:
1. Nashauri uongeze ukubwa wa PDF wakati unaangalia kwa karibu 700% kuweza kusoma vizuri.
2. Mistari iliyopigwa kwenye kijitabu hiki ni reaction ya serikali ya Marekani walipopitia mpango huu.

Nakushukuru sana, kwa inaonekana una access ya mambo mengi ya wakati wa utawala wa Nyerere, itakuwa tunawatendea haki vijana wa kizazi hiki kama tutaelimisha kuhusu namna Mwalimu Nyerere alivoua "Enterpreneurship" iliyokuwepo hapa nchini kwa Sera za Azimio la Arusha. Nyerer alivyoua productivity katika viwanda, mashirika n.k kwa kuua "Supervision" kwa Mwongozo wa TANU unaokataza unyapara na ukaripiaji n.k.

Tusiandike mazuri tu ya Nyerere tuandike opia na mabaya yake ili vijana wa kizazi hiki waweze kujua mchawi aliyeturoga watanzania ndipo wataweza kupata tiba ya ugonjwa tulionao kama taifa.
 
hapa ndipo matatizo yote ya nchi hii yalipolala. ACTION ...VITENDO!!!! Nimemuona waziri Nyarandu jana kabanwa na Mh. Tindu Lissu, kaishia kutetea pumba zao kwa kutoa mfano wa USA wanavyosamehe kodi kuvutia uwekezaji, TZ na US wapi na wapi?. Cha kusikitisha budget/mswada umepita wakati kuna budget nzuri sana wa Mh. Zitto imekuwa imekataliwa!
Tuanzie wapu kutekeleza vinavyotekelezeka na kuacha upupu huu??

Mhe Nyarandu alivyobanwa kisawaswa na Mhe Mnyika kuhusu upotoshaji wake kuhusu viwango vua kidogo katika EAC na kufikia mbunge wa CCM Mhe Simbachawene kuunga mkono pendekezo la Mnyika kuwa kipindi cha msamaha wa kodi kiwe ni miaka 5 badala ya 10. Mhe Nyarandu alitumia maneno ya vitisho yafuatayo" kwa wale wabunge wa CCM wenzangu naomba mtambue kuwa Serikali ina dhamira njema katika hili" . Cha ajabu wabunge wote wa CCM baada ya kusikia maneo haya ya vitisho wakasahau kuwa wapo pale bungeni kwanza kwa mujibu wa kifungu cha 63 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndipo yanafuta masuala ya vyama vya siasa na hivyo wakanywea.
 
Back
Top Bottom