Jambo Usilolijua: Kambona -"Nyerere... Baba wa Taifa"; Hotuba yake tuliyoisahau

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
attachment.php


Ifuatayo ni sehemu ya hotuba maarufu aliyoitoa Bw. Oscar S. Kambona ambaye alikuwa ni Katibu Mkuu wa Chama cha TANU na Waziri katika Baraza la Nyerere. Hotuba hii ilitolewa Bungeni (Dar) na ilihusu kile ambacho kimebeba jina la kijitabu hiki yaani "UONGOZI WETU". Wakati hotuba hii inatolewa ni lazima tutambue maudhui ya kihistoria ya wakati ule tayari kulikuwa na tetesi za migongano ndani ya TANU (kama tunayoiona leo) na tayari kulikuwa na hisia ya msuguano kati ya Nyerere na Kambona. Tukumbuke ni hotuba imekuja baada ya maasai ya 1964.

Kambona anajaribu kujenga hoja kuwa uongozi ni kukosoana na kusahihishana bila kuoneana aibu. Ni katika sehemu ya hotuba hii tunaweza kuona kabisa kuwa Nyerere alikuwa ni kiongozi miongoni mwa viongozi na kulikuwa na nafasi ya kukosoana. Lakini vitu viwili vimenigusa kwa sababu nimeandika kwenye MwanaHalisi ya leo juu ya jaribio la baadhi ya watu kumvua Nyerere hadhi yake ya "Baba wa Taifa" kwa kujaribu kumuona kama ni "Mzee Nyerere" au "Mmoja wa Waasisi".

Kwa baadhi ya vijana wa leo wanaweza kufikiria kuwa hadhi ya "Baba wa Taifa" ni hadhi ambayo Nyerere amekuja kuipata baada ya kustaafu au hata baada ya kufa kwamba katika mapenzi ya watu basi ndio wakaanza kumuita "Baba wa Taifa". Hotuba hii (na nyingine nyingi za wakati wake) zinatupa ushahidi wa karibu miaka 45 iliyopita kuwa wazee wa wakati wake walitambua nafasi na mchango wa Nyerere katika historia na hawakuwa na utata kuwa walimuita ni "Baba wa Taifa". Kambona ni mmoja tu wa viongozi ambao walitambua nafasi na mchango huo wa Nyerere.

Katika kazi yangu nyingine huko mbele tunapoelekea maadhimisho ya miaka 50 nitakuja na pendekezo ambalo naamini watawala wetu (wa CCM na Upinzani) watalipokea na kulifanyia kazi.

Pamoja na suala la Baba wa Taifa, tunaweza kuona katika hotuba hii kuwa Kambona alitambua kile alichokiita kuwa ni "Demokrasia yetu ya Chama kimoja". Mara nyingi tumekuja kusikia kuwa Nyerere na Kambona walitofautiana sana kuhusu suala la chama kimoja. Tofauti hizi tukumbuke zimekuja kukua zaidi baadaye na siyo mwanzo wake namna ambavyo wengi wameaminishwa. Maneno ya Kambona ni sehemu ndogo tu ya ushahidi wake; nimatumaini yangu maandishi mengine ya Kambona yatawekwa bayana na wazi kwa Watanzania waweze kupata ufahamu wa fikra za kiongozi mwingine muhimu sana katika historia yetu. Ukisoma vizuri utaweza kuviona pia vijembe vya kisiasa ambavyo Kambona hakukwepa kuvirusha dhidi ya Nyerere...

Ukiondoa mambo hayo, hotuba hii inatupa fikra za Kambona kuhusu uongozi na ukisoma kwa utulivu unaweza kuona ni jinsi gani CCM ya leo na hata vyama vingine vinaweza kujifunza kuhusu "uongozi wetu"! Ni hazina ya fikra. Enjoy!
 

Attachments

  • kambonaspeech1966.pdf
    474.1 KB · Views: 1,131
  • kambona1.png
    kambona1.png
    152.2 KB · Views: 2,350
Sasa kama Kambona aliwapa heshima wenzie kwa kuwaita "Baba", mbona yeye hakupewa heshima hiyo na kuishia kuitwa "Mwanamke" kinyume na jinsia yake, rejea wimbo huu wa jeshini, taasisi ya umma, na mchakamchaka mashuleni!

"Kambona kaolewa, wapi?, ulaya...... wivu wamkereketa?
 
Sasa kama Kambona aliwapa heshima wenzie kwa kuwaita "Baba", mbona yeye hakupewa heshima hiyo na kuishia kuitwa "Mwanamke" kinyume na jinsia yake, rejea wimbo huu wa jeshini, taasisi ya umma, na mchakamchaka mashuleni!

"Kambona kaolewa, wapi?, ulaya...... wivu wamkereketa?

Si kweli, Kambona hakuwapa heshima wenzie kwa kuwaita "baba". Labda usome vizuri hotuba yake.
 
Mkuu haujatutendea haki sisi tunaotumia mobile tena za kihindi. Hatuwezi kusoma hiyo hotuba. Kama unaweza kuipesti tutaenda sawa!
 
Shukrani Mzee MM!

Much respect !

Nakijumuisha katika maktaba yangu.

Ahsante na Mungu akupe nguvu zaidi na hekima zaidi na ujasiri zaidi!
 
Penye ukweli uongo utajitenga. Mwanakijiji umesema kweli kabisa kuhusu nia ya baadhi ya wanasiasa ambao kwa ajiri ya uovu wa matendo yao na kushindwa kuthubutu, wanataka kumfuta Nyerere kama kiongozi mahiri wa Taifa letu
 
Huyo mzee zake zimeisha sasa anakabiliana na "Baba" wa kila kiumbe. Ana kazi kubwa kujibu jinsi gani aliwatawala wa Tz. Msitulazimishe kumuabudu huyo mzee...wakati umefika wa Tz kuangalia mbele. Kama kuchelewa yeye "Nyerere " ndio alituchelewesha... huo ubaba mnaompa ni kwenu nyinyi msihusishe kila mtz.
 
Namuunga mkono mtu mmoja aliyesema kuwa wewe unafaa kuwa kiongozi wa Chadema huko mbeleni. Huwa nina enjoy sana makala zako.
 
Una sources nzuri sana! very impressive and keep it up!
Hicho kitabu ni 'Uongozi Bora' na sio 'Uongozi Wetu' kama ulivyoandika hapo juu.
 
Mwanakijiji eti nasikia ww ni mahaarufu sana wa kuchomoa nakala katika vitabu katika maktaba ya Taifa. Paste hiko kitu sioni kitu.
 
mzee mwanakijiji una mchango mkubwa sana si Jf peke bali taifa zima,una mkakat gani nje ya janvi hili? Naendelea kusoma kisha nitauliza maswali.
 
Una sources nzuri sana! very impressive and keep it up!
Hicho kitabu ni 'Uongozi Bora' na sio 'Uongozi Wetu' kama ulivyoandika hapo juu.

yeah.. kwenye cover kinasema Uongozi Bora... nadhani nilifikiria cha Nyerere.. Uongozi Wetu... (Nyerere alipoandika cha kwake alikuwa anafikiria hiki???)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom