Jambo Unalolipenda na Kulitumikia Lina Uhusiano wa Moja Kwa Moja na Kifo Chako

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
Jambo Unalolipenda na Kulitumikia Lina Uhusiano wa Moja Kwa Moja na Kifo Chako




MUNGU ni wa ajabu. Ajabu yake inakamilishwa na yaliyomo ulimwenguni, ikiwemo yanayoonekana na yale ya kusadikika. Uwepo wa uhai umekamilisha pande mbili za shilingi ambazo ni uhai na kifo/mauti.

Upo uhusiano wa moja kwa moja kati ya kile unachokipenda na kifo chako. Wazungu wanaita “hobby”, hivyo hobi yako inaweza kuwa njia kuelekea safari ya mwisho wa maisha yako.

Mpenzi wa kuogelea anaweza kuyapoteza maisha yake katika maji, mwanamuziki anaweza kufa kwa kuanguka jukwaani ama chumba cha rekodi, mwanamasumbwi anaweza kufa akiwa na mpenzi, mwendesha gari anaweza kufikwa na mauti akiwa katika usukani vivyo hivyo kwa tasnia zingine na watendaji wake.

paul-walker.jpg


Paul William Walker.

Hii inaonyesha kifo kinaweza kusababishwa na mfumo wa maisha unayoishi kupitia jambo lile ulilolipenda. Starehe unayoipenda zaidi, ile yenye kuufurahisha moyo wako inaweza kuwa tiketi ya kuelekea safari yako ya mwisho. Ipo mifano hai ya watu maarufu na mashuhuri ambao mapenzi yao dhidi ya jambo fulani yamekamilisha safari yao ya kurejea kwa Mwenyezi Mungu.

Tumrejelee Paul William Walker aliyekuwa muigizaji mashuhuri ulimwenguni aliyezaliwa mwezi Septemba 12, 1973 huko Glendale, Califonia, na kufariki dunia Novemba 30, 2013 huko Santa Clarita katika jimbo la Califonia kwa ajali ya gari. Walker alifariki akiwa na rafiki yake Roger Rodas.

Kifo cha Paul Walker kiliibua simanzi kwa wapenzi wa filamu ulimwengu. Hisia hizo zilisindikizwa na wimbo wa Wiz Khalifa “See You Again” uliotumika katika filamu ambayo alishiriki Furious 7 (2015) lakini hakushiriki mpaka mwisho hivyo baadhi ya vipande walimtumia mdogo wake kukamilisha filamu hiyo.

Aliyekuwa nguli wa muziki wa dansi mwenye uraia wa Jamhuri ya Kidemodrasia ya Kongo, Papa Wemba, alifariki dunia kwa kuanguka jukwaani akitumbuiza. Janga hili linathibitisha mada yetu ya uwepo wa mahusiano ya kifo katika kile unachokipenda au kazi unayoifanya.

marc-vivien-foe.jpg


Marc-Vivien Foé .

Papa Wemba alianguka jukwaani akifanya shoo huko Abdjan, Ivory Coast, na mitandao mingi ikaripoti kuwa ameuawa baada ya kuwa na hali ya utata kwa mtu asiyefahamika kuoneka kukatiza jukwaani.

Bondia wa ngumi za kulipwa maarufu kama Thomas Christopher Malifedha Mashali, alishambuliwa na silaha za jadi na watu wasiojulikana, ni baada ya kushindwa kuelewana na kuleta ubabe wa ulingoni mtaani. Zipo stori tofauti-tofauti mtaani ambazo zinaongelea kifo ambacho bado kina majonzi mabichi.

Ni Jumapili ya wiki iliyopita maeneo ya Kimara, Bonyokwa, jijini Dar es Salaam, ndipo pumzi za Mashali ilipouacha mwili. Jambo alilolipenda zaidi Mashali ni masumbwi na ndiyo sababu ya mauti yake ambapo inasemekana baada ya kuleta ubabe akaitiwa kelele za mwizi.



Thomas Mashali.

Tuhitimishe na mchezaji wa mpira wa miguu kiungo wa zamani wa Cameroon, Marc-Vivien Foé ambaye alifariki dunia kwa kuanguka uwanjani na kudhaniwa kazimia lakini taarifa zikathibitika kuwa amekufa baada ya kufikishwa hospitali.

Foé alianguka wakati wa mechi ya nusu fainali katika mpambano wa Kombe la Mabara dhidi ya Colombia mjini Lyon, Ufaransa, Juni 2003. Enzi za uhai wake marehemu aliwahi kuichezea West Ham United, Manchester City na mauti yalimfika akiichezea Lyon.

Salum Milongo

GPL
 

Attachments

  • papa-wemba.jpg
    papa-wemba.jpg
    148.4 KB · Views: 83
  • paul-walker.jpg
    paul-walker.jpg
    20.9 KB · Views: 86
  • marc-vivien-foe.jpg
    marc-vivien-foe.jpg
    18.3 KB · Views: 104
  • mashali.jpg
    mashali.jpg
    43.7 KB · Views: 87
Kweli inawezekana kabisa,mf:kuna ndugu yetu alipoteza maisha akiwa shambani kwake,haijulikani aligongwa na nyoka au la ila alipenda sana kazi za shambani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom