Jambo limezua Jambo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jambo limezua Jambo.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by uporoto01, Aug 24, 2010.

 1. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wakuu muda flani hapo nyuma nilikuwa na GF ambaye tulipendana, tukakosana kwa mambo ya kitoto tu, sasa kuna muda akapata mtu wa kumuoa kwakuwa bado tulikuwa marafiki wa kawaida akaja kwangu na jambo la ajabu kidogo.Huyo jamaa anaetaka kumuoa alishapima akajua hawezi kuzaa yaani mbegu zake zina matatizo,wakawa wameelewana apatikane mtu wa kumpa mimba ili aolewe na mimba ndogo jamaa ijulikane anaweza.Alinionyesha picha ya jamaa ambaye kwa mbaali tumefanana kidogo.
  Nikamwambia nitafikiria na pia nikikubali nataka nisikie kauli ya jamaa na pia sitaki kuhusika na kitu chochote baada ya hapo.Zoezi lilifanyika mimba ikapatikana na mtoto wa kike kuzaliwa tukapoteza mawasiliano kama tulivyoelewana.Juzi kati bibie kanifata(baada ya miaka mitano) mumewe alifariki mwanzoni wa mwaka huu na yeye hana uwezo wa kumtunza mtoto peke yake,mtoto ana matatizo ya kiafya kibao asthma,tumbo nk kwa kifupi ni high maintenance kila wiki hospitali.Familia ya mumewe wamechukua kila kitu na hana nguvu wala muda wakupigania mali.Kapata kazi Zambia anadai hawezi kwenda na mtoto na kwakuwa mimi ni baba nimchukue.
  Nimemweleza wife kila kitu kasema hana tatizo la mimi na yeye kumsaidia kifedha lakini swala la kubwagiwa mtoto mgonjwa hataki kulisikia na maelewano si yalikuwa tusijuwane tena?Tusaidiane mawazo wakuu.
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...yaani hapa itakubidi tu ufungue account ya mtoto tumchangie.
  Malaika wa mungu hana kosa huyo jamani nyie wazazi wa kileo.
  5yrs old mama hamtaki, ndugu hawamtaki, baba mzazi hamtaki...
  mnh!
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wacha kukimbia majukumu bro.
   
 4. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Asante Mkuu tatizo sio uwezo,wife anadai bibie hamtaki mtoto kwa sababu ya ugonjwa,naye hayuko tayari kuchukua dhamana hiyo.Wife pia kasema yuko tayari kumtafutia kazi hapa hapa ili aendelee kumtunza mtoto wake na tumsaidie atakapokwama.Mama wa mtoto anadai kazi aliyopata Zambia ni ya hela nyingi na akifanikiwa atamfata mtoto jambo ambalo wife haliamini anasema akiondoka na kumuacha mtoto imetoka hiyo na hatutamuona tena.
   
 5. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mimi niko tayari kumtunza mtoto lakini niko kwenye wakati mgumu ukizingatia maelewano yetu kabla na wife kukubali kumsapoti mtoto kwa mama yake na sio kubwagiwa na bibie kukimbilia Zambia.
   
 6. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,835
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Binafsi dhamira ingenishtaki kwa kuwa huyo ni mtoto wangu. Sahau hayo mengine focus kwenye kuokoa maisha ya mtoto wako! There is no way you will be peace at yourself, na wala hakuna mtu mwenye akili timamu ata hoji kitendo chako wewe kuokoa maisha ya mtoto wako! Men go get her!
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Sasa hapo ndio unatakiwa utumie uanaume wako, uanaume sio kuvaa suruali tu..Ina maana maiwaifu wako akikataa utakatelekeza hako kamalaika?
   
 8. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,835
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Sio lazima ukae nae hapo kwako! Maana ukweli ni kwamba hata ukimleta hapo kwa mama wa kambo hatapendwa na unaweza mpoteza kabisa! Kama unakubali kuchukua jukumu la kutunza hata akiwa Zambia it doesnt matter. Cha msingi awe mahali you can reach her na apate huduma inayostahili.
   
 9. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kaka ukirejea maelezo yangu pale juu nilikuwa 'sperm donor' tu na bibie na mumewe walinihakikishia sitahusika tena,sawa yametokea matatizo namsifu wife kwa kunielewa nilipo mueleza na hata sasa anahusika kumpeleka mtoto hospitali na kukidhi mahitaji yao kwa kuwatembelea kila wiki.Uanamme gani unataka niutumie kwa mtu muelewa hivo?
   
 10. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huyu mama wa mtoto nahisi lengo lake kuu ni mtoto afike kwangu manake msaada wa fedha au kumtafutia kazi hapa haridhiki na hili linampa wife wasiwasi.
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  U-sperm donor ni huko Ughaibuni, bongo you are a sole father muzee. Nazungumzia from moral point of view, kisheria sijui. Nachojaribu kuelewa hapa ni wewe kama unasubiri kuambiwa kutimiza wajibu wako, yaani unasubiri uambiwe kuchukua uamuzi. Uamuzi wa kuchukua upo mikononi mwako, u can't compromise maisha ya hicho kiumbe kwa sababu yeyote ile, kama wife hataki kuachiwa huyo mtoto amtunze tafuta slot yeyote iliyo wazi, kama upo na dada au akina bibi shangazi etc, wewe mwenyewe unajua utafanya vipi..ikishindiakana sana itabidi uforce kingi mbanane hapohapo na wife.
   
 12. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu wanamjua huyu mama wa mtoto kwa sababu alikuwa GF wangu zamani na wanajua aliolewa na kuzaa mtoto sasa leo nitaanzaje kuwaeleza mimi ndio baba wa huyo mtoto? nitaanzaje kuwaambia nilimpa mimba huku mumewe akijua na kuafiki kwa mazingira yetu?
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu, mi nilidhani mtu wa kwanza wa kumuogopa alikuwa mkeo, kama amekuelewa sielewi kwa nini ndugu uwaogope.
   
 14. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ndio maana niko macho saa hizi,sina amani na mtoto anajua babake kafariki ni dilemma!
   
 15. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wife ni mtu mwenye exposure ana maduka yake kariakoo alianzishiwa na baba yake nilimkuta tayari ana maisha yake,familia ni watu conservative nikiwaambia wataniona mchafuzi na kunitenga.
   
 16. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #16
  Aug 24, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hapo mwambie akiwaachia mtoto mwende kwa lawyer, mtoto mumchukue nyie moja kwa moja.

  mke wako haonekani kuwa atamchukia huyo mtoto (si dhani kama kuna mtu anachukia mtoto wa ready made), tafuteni lawyer hakikisheni mtoto anakuwa wenu moja kwa moja.
   
 17. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Gaijin mtoto nilizaa na my EX while she was married to another man(now dead) with his knowledge/approval.
   
 18. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #18
  Aug 24, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  ndio ......sasa tatizo kitu gani?

  mama mtoto si yuko tayari kuthibitisha kuwa mtoto ni wako? na kuna dna tests ambazo zitathibitisha kuwa mtoto ni wako?

  kama mama mtoto anataka kuwatupia mtoto na yeye ende zambia, basi mumu adopt kabisa kabisa na asiwe na uwezo wa kurudi na kudai mtoto wake.
   
 19. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #19
  Aug 24, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ubini wa mtoto hauna tatizo mimi na wife hatuoni sababu ya yeye kwenda Zambia kama tutamsaidia kupata kazi hapa na kumpa msaada wowote atakaohitaji amtunze mtoto wake ambaye ni mgonjwa na anahitaji kuwa karibu naye na anafahamu matatizo/mahitaji ya mtoto.Pia wife ana mimba ya miezi kadhaa anatapika tapika hawezi kuchukua jukumu hilo kwa sasa.
   
 20. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Bro, naona unasitasita..tafuta namna ya kumsitiri huyo mtoto kwanza, huyo mamaye si mali kitu tena na ameshaonesha anabwaga manyanga..Kama Gaijin alivyokushauri wewe fanya taratibu za kisheria uangalie ustaarabu mwingine...hata kama wife wako hayupo tayari kwa sasa anaonesha ana roho nzuri basi angaza macho angalia kwene empty slot kokote umsitiri huyo mtoto..tatizo ulilipanda mwenyewe pengine kwa nia njema, lakini sasa huezi kumuadhibu huyo malaika tena. Cha msingi ni kufikiri kwa undani utamleaje huyo mtoto...kwa muda huu, halafu baadae wife anaweza kubadili mawazo taratibu pale utakapoonesha nia ya kumlea.
   
Loading...