Jambo Leo: Zitto na Dr. Slaa wachuana urais 2015, Zitto kama Ngasa na Dr. Slaa kama Messi

Ujinga ni ugonjwa mbaya mithili ya ukoma. Hivi mmeshawahi kufikiri kama CDM ingekufa leo, Zitto akaanzisha chama chake na Dk.Slaa akaanzisha chake nani ana uwezo wa kubakia mchezoni akiwa juu?

Nina mashaka hii ni mipango ya CCM na ni namna ya kuwatumia ndugu zetu wanaowatumiaga kushinda kwa kuwaaminisha kuwa fulani ana sifa ila sababu tu ya nanii yake ndio maana hapewi nafasi
 
Ngassa(Mh.Zitto) Vs Lionel Messi(Mh.Dr.Slaa) halafu wanaita ni mchuano mkali,kivipi?! Mwandishi lazima atakuwa na tatizo la msingi si bure.
 
kwangu mimi sidhani kama ipo busara ya kuwapambanisha wakati muda muafaka bado haujafika ingawa si vibaya kuonyesha nia. Hivyo nadhani haya yote yanaweza yakaleta athari kubwa mbele ya safari kama bado hayajaanza kuleta.
 
zitto anakubalika kwa WATANZANIA wote, Dk SLAA anakubalika kwa WAKRISTO tu.

Mkuu mbona unajipiga chenga mwenyewe na kushangilia! Wakristo hawapo miongoni mwa watu wote? Basi unataka kumaanisha kwamba Zitto anakubalika na Waislam na Wahindu basi.
 
magazeti mengine yaani ni kichefuchefu hata kusoma pengine hata kuyasikia tu unaona kinyaa tuweni makini na magazeti kama haya na wahariri waliochoka kimaisha na wanaotumiwa kundanganya umma wa tanzania
 
watu makini hawawez kumshindanisha zito na dr slaa. kwanza kwan chadema hakina watu zaid ya huyu?
 
Zito aache papara. Ana akili na uwezo wa kuchanganua mambo ila papara na haraka zake zitamuharibia mambo mengi. Awache kichwa ( dr slaa) awanyoe ccm kwa chupa. Wakati wake ukifika atapewa bila kulazimisha anachokitaka. Akileta ubishi na kujua kwingi atakosa vyote. Tulia kama Lisu na Mnyika. Nyakati zenu zaja
hata mie nyakati yangu yaja...sio hao tu kwakuwa wametangulia tupo majembe pia huku...tumechilii tunamalizia masomo kwanza
 
well said mkuu zzk kagaragazwa vibaya na dr. Slaa huwezi sema 85% na 15% (approx.) ni mchuano mkali, huo ni mzaha wa hali ya juu!
,

Madam, inawezekana imetumika sayansi nyingine, kwamba hayo matokeo ni draw: Dr. Slaa amebakiza 15% kupata 100% wakati ZZK amebakiza 15% kupata 0%, so kwa kufuata hesabu hiyo ya kiasi kilichobakia kufikia target, na kuwa wote wamebakiza 15% tu, so wako sawa, PLEASE ACCEPT THIS CALCULATION !
 
Tuko busy kujenga taasisi imara.Tunaijenga Chadema.Hatujengi watu na tufahamu kuwa Chadema imara ndiyo itakayotoa candidates imara kwenye uchaguzi wowote.Hatujengi familia au makundi maslahi....

Hakuna Dr.Slaa anayetisha bila Chadema imara,hakutakuwepo na Zitto anayetisha bila Chadema Imara

Leo hii kila candidate wa Chadema (subiri matokeo ya udiwani kata zote leo jioni) anatisha na wananchi wanaona wazi kwa kuwa wako juu ya mwamba,wapo juu ya Chadema inayotisha.
 
Messi ni gwiji la mpira....kala tuzo mara kibao ya mchezaji bora.....too shame kuwaweka kundi moja na Ngassa...ni kama tembo na sisimizi.
 
zitto anakubalika kwa WATANZANIA wote, Dk SLAA anakubalika kwa WAKRISTO tu.

kwa hiyo hao wakristo sio watanzania au ni wakenya? talkin ballocks....2015 i feel its too early for zzk...2020 should b jus the right time...
 
zitto anakubalika kwa WATANZANIA wote, Dk SLAA anakubalika kwa WAKRISTO tu.
JAMBOLEO LIMEANDIKA LIKITAKA WATU WENYE MTAZAMO KAMA HUO, HAWANA NIA NJEMA NA HAWAFIKIRII KUINDIKA CDM VIZURI NIA NI KUWAGDWA WATANZANIA ILI TUENDELEE KUTAWALIWA NA MAFISADI, PIA ILI KATIBA IENDELEE KUMWONA RAISI WA TZ MUNGU, KAMA SI MUNGU KWANINI AWEJUU YA SHERIA? Na ukilisema kwa wajinga watakuambia kwa sababu raisi ni kikwete, tuna tatizo habari leo inawataka wajinga na wajinga wanajitokeza
 
hiki si kijigazeti cha vihiyo. ukisoma habari utazani kuna lolote kumbe ni udaku tu, kwa nini wasijiunge na uwazi, ijumaa na kiu?
 
watu makini hawawez kumshindanisha zito na dr slaa. Kwanza kwan chadema hakina watu zaid ya huyu?

wapo kazini wametumwa kukisambaratisha cdm. Hivyo wajinga wenzao tu ndio watakaoamini ujinga huu, nchi masikini hii mpaka ubongo ni masikini nae anajiita mwandishi, misingi ya uandishi 0 ndio maana hata mauzo ya gazeti ni ovyo
 
For me NEVER EVER ZZK huwezi kumpambanisha na Dr. Slaa....

But if we aim to compare though are uncomparable politically..... Here is their equivalency.....

Dr. Slaa ----- USAIN BOLT

ZZK ---------- Cripple...
 
Smart boy ZItto, amefananishwa na Mrisho Khalfan Ngassa mchezaji wa timu ya Simba ya TAnzania na DR SLAA amefananishwa na Messi wa Barca , haya ZITTO tayari wewe ni mchezaji hatari unayeweza kulisaidia taifa hili ukiwa kama rais na utapokea misaada toka mataifa mbalimbali ikiwemo Spain na ARGENTINA anakotokea na kufanya kazi mchezaji nguli wa soka MESSI
 
Back
Top Bottom