Jambo la muhimu kwa watanzania wote ni kuendelea kuchukua tahadhari zote zinazotolewa na Serikali pamoja na wataalam wa afya kuhusu Corona

Kagosi DJ

Member
May 5, 2020
19
69
HUU SIO USHAURI NI UCHONGANISHI​
Kwa wakati huu taifa linahangaiaka kupambana na janga la corona lililo ikumba dunia.

Watanzania waliowengi wanaelewa mambo ya msingi kuhusu ugonjwa huu hatari na hili haswa ndio jambo la msingi kwa wakati huu.

Lakini tusijisahaulishe hali yetu halisi kwamba watanzania walio wengi ni wale wa kipato kidogo, bodaboda, mama rishe, makondakta, madereva, wapigadebe na machinga ndio shughuli zetu za kila siku.

Hizi shughuri zote zinahitaji uwepo wa watu mitaani ili ziwe na uhai. Watanzania tulio wengi uwezo wa kukaa angalau Siku tatu bila kufanya kazi na maisha yakaenda ni mdogo sana.

Kuna baadhi ya watu wanaishauri serikali kufunga baadhi ya miji na hata kuwafungia watu ndani. Hili ni wazo zuri na lina lengo la kusaidia kupunguza maambukizi ya corona nchini lakini kama likiishia hapo, huo hautokua ushauri tena bali ni uchonganishi.

Serikali ikiamua kufunga miji na kufungia watu ndani hiyo ni amri haitokuwa na mjadala tena, kwahiyo lazima itekelezwe sasa ni watanzania wangapi wanaweza kukaa ndani na kwa siku ngapi wakiwa na chakula cha kutosha? Hapo atujagusia swala la kodi ya pango maana wengi ni wapangaji.

Watu tutaonekana tunakaidi amri ya serikali na mwisho wake serikali itatumia vyombo vya Dora tutaambulia kipigo na kurazimishwa kutii amri hiyo, wale watu walio ishauri serikali watakuwa wakwanza tena kuikosoa kwa kuvunja haki za binadamu. Huo utakuwa uchonganishi wa kwanza

Lakini hata tukikaa huko vizuizini tutahitaji chakula washauri walewale watakuja kuishauri serikali igawe chakula, sasa ni watanzania wangapi watahudumiwa na serikali na kwa muda gani? Huo ni uchonganishi wa pili.

Hawa washauli kama kweli wanayo nia nzuri kwa serikali na taifa hawapaswi kuishia katika kuishauri serikali kufunga miji na kufungia watu ndani Bali waoneshe muelekeo wa taifa na maisha ya watanzania ndani ya mazuio hayo.

Hali ya mataifa mengi duniani ni ngumu chini ya hatua hizi Kali, ndio maana mataifa mengi hivi sasa yanapunguza masharti licha ya maambukizi kuongezeka hivi bado hatujifunzi kitu hapo??

Jambo la muhimu kwa watanzania wote ni kuendelea kuchukua taadhali zote zinazotolewa na serikali pamoja na wataalam wa afya, lakini umoja na mshikamano ni moja ya njia muhimu za kupambana na hili janga.

Tuweke itikadi zetu pembeni na wala huu sio wakati wa kutafuta umaarufu wa kisiasa. Kwapamoja tuendelee kumuomba MUNGU atuepushe na madhara zaidi.

MUNGU IBARIKI TANZANIA,
MUNGU IBARIKI AFRIKA,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom