Mchunguzi J. Namala
Member
- Oct 31, 2013
- 14
- 13
CHADEMA tunavyotaka kuchukua dola hili ni muhimu lifanyiwe kazi.CHADEMA tumetegemea sana watu binafsi na hili linaweza kutugharimu.Mfano sio jambo la kujivunia kusema ofisi ya mkoa ya CHADEMA ilikuwa sebuleni kwa mtu.Viongozi jitahidi kwa hekima muhakikishe chama kina ofisi zinazoeleweka kuanzia ngazi ya chini mpaka juu. Lakini pia tuangalie suala lingine mfano wilaya ninayokaa mimi CHADEMA ni k.m inaendeshwa na mtu mmoja kwa sababu yeye mara nyingi ndio mfadhili mkuu wa chama.Kwa hiyo hilo linampa nguvu ya kuweza kuamua lolote na viongozi wakatii kwa sababu ya nguvu ya pesa.Je siku ikitokea naye akaasi?Kwa hiyo tuangalie vizuri misaada ya watu binafsi isikigharimu chama. Pia ni kweli kabisa tumewasahau viongozi wetu wa ngazi za chini na nahisi ndio maana wanatumiwa na C.C.M na watu wengine wenye masilahi yao.Viongozi wengi wa ngazi za chini wanajituma sana lakini wana njaa sana.Mfano C.C.M haiwalipi viongozi wake wa ngazi za chini lakini imewajengea mazingira ya rushwa ambayo wameridhika nayo.Mfano ukienda mahala una shida na balozi anataka umpe hela ndipo akuhudumie. Mimi nina rafiki yangu ambaye ni kiongozi wa CHADEMA Ambaye anajituma sana kukitumikia chama.Lakini juzi kakimbiwa na mke wake kisa maisha magumu.Nawaomba kama tunavyopigania haki za walimu,madaktari,polisi na wengine pia tuwaangalie viongozi wa chama kuanzia ngazi ya chini.Hii itatutofautisha na vyama vingine. MAWAZO YANGU NI KWA AJILI YA KUBORESHA NA SI KUBOMOA.