Jambo hili ni la kuzingatia: Ukiona mtu amenusurika kufa katika tukio la kufyatuliwa risasi zaidi ya thelathini ujue liko jambo la Mungu linaendelea

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Mimi kwa uzoefu wangu mdogo wa kusoma maandiko matakatifu kwa habari ya mambo ya rohoni, nimekutana na visa kadhaa vya watu ambao shetani alitaka/alitamani kuwaangamiza kwa sababu shetani aliona watu hao wakiwa wamebeba kusudi kubwa la Mungu, hivyo ibilisi huwa anataka kulifutilia mbali kusudi la Mungu.

Kwa uchache niwataje wachache.

YUSUFU - huyu shetani aliwatumia ndugu zake na Yusufu kutaka kumwangamiza. Lakini kwa vile Yusufu alikuwa amelibeba kusudi la Mungu, ndugu zake hawakufanikiwa kumuua, waliishia kumuuza Misri ambapo baadaye alikuja kuwa mtu mkubwa sana na kufanyika msaada mkubwa si kwa ndugu zake tu, bali kwa taifa zima la Israeli kwa ujumla. Huyu ndiye alieendeleza ma-Agano kati ya Mungu na Ibrahimu, Isaka na Yakobo.

MUSA - Huyu alipozaliwa tu, shetani alimuwinda amuue kupitia mfalme wa Misri (Farao). Shetani aliandaa mpango mzima wa kumuangamiza Musa kwa kutangaza kuuawa kwa watoto wote wa kiume wa Kiebrania, lakini kwa muujiza mkuu Musa alipona na kupata hifadhi katika Kasri la mfalme na akakulia kwa waliotaka kumuua. Huu ni muujiza wa Mungu. Ndiye baadaye aliyekabidhiwa Torati, na pia alipewa na Mungu jukumu la kuwatoa wana-Israeli utumwani Misri.

YESU MNAZARETI - Mara tu baada ya Yesu kuzaliwa huko Bethlehemu, shetani kama kawaida yake alitaka amwangamize Yesu kabla mpango wa Mungu juu yake kutimia. Ibilisi alimtumia Herode na akatangaza kuwaua watoto wote wa kiume wa chini ya miaka miwili. Lengo likiwa ni kumwangamiza Yesu. Jaribio hili pia lilishindikana kwa kuwa shetani hana uwezo wa kulizuia kusudi la Mungu. Na hivyo mpango wa Mungu wa kumleta Yesu ulitimia, na ulipotimia ndipo akaondoka zake.

UKIONA MTU ANAKOSWAKOSWA KUUAWA KATIKA HALI YA KUMIMINIWA RISASI NYINGI VILE UJUE SHETANI AMESHINDWA KUTIMIZA KUSUDI LAKE LA KUTAKA KUPINGANA NA KUSUDI LA MUNGU. MIPANGO YA MUNGU NI ZAIDI YA MIPANGO YA SHETANI. Ibilisi ni wa kushindwa tu siku zote.
Ukiona mtu kanusurika tukio la kuchapwa risasi nyingi kama hizi kuna uwezekano huyo mtu ni msaliti wa nchi ama alitaka kuwatapeli mabwana zake waliokuwa wanamfadhili. Siku zote mzungu atatumia waafrika wasaliti, atakutunza na kukupa msaada ili afaidike huko mbeleni...akikuona unamzingua anakutungua.
 
Vipi akina chifu mkwawa nao, vipi machifu walionyongwa,hebu niambie kuhusu wao, hapa Kuna darasazuri

Not related. Hao walikuwa vitani, anayemuwahi mwenzake anamfanyia chochote. Of course vita haikuwa halali but it was a war.
 
Not related. Hao walikuwa vitani, anayemuwahi mwenzake anamfanyia chochote. Of course vita haikuwa halali but it was a war.
Unasemaje kuhusu lissu? Ukiweka siasa na upenzi wa vyama huezi ona lissu anafanya nini, na Ukiweka upenzi wa vyama mbele, huezi ona serikali inafanya nini, huezi ona madaraja, huezi ona umeme, huezi ona elimu bure kwa hiyo ugonjwa huohuo unaowasumbua hao wanaoitwa wapinzani ndo unaokusumbua wewe, lissu anachoongelea ni sawa na serikali mambo inayoyafanya kwa ajili ya maendeleo ni sawa, hawa wote wako katikati harakati za kufanya nchi iwe bora zaidi, sema wanatofautiana katikati mitazamo, sasa wewe ambaye siyo mwanasiasa, kaa kati uwaangalie wakipambana kwa ajili ya nchi
 
Ingekuwa unayoyasema yangeuwa na uwiano wenye usawa hats usingekuwa hapa kutetea hoja hizi.
 
Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom