Jambo hili limenishangaza sana tuwe makini na malezi ya watoto wetu

pancho boy

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
4,019
2,000
Wakuu,

Majuzi kati nilienda kumsalimia kaka yangu. Kaka huyu anaishi na mkewe na watoto wawili wa kike. Hawajafika miaka kumi.

Kwa bahati mbaya wakati nafika mkewe braza (shemeji) naye alikuwa anasafiri kwenda kwao kwani kutakuwa na sherehe, hivyo braza na watoto watakuja kesho kutwa yake.

Sasa kimbembe kilianzia hapa.
Tupo wote sebleni, vibinti vile vikamuuliza baba yao "Baba, leo utalala na nani mama hayupo?"

Baba (kwa Upendo) akajibu."nitalala na nyie wanangu "

Ghafla vibinti vile vikaropoka.
"eeh ili utu....? "

Nilishtuka mithili ya mwanamke aliefumaniwa...!
Baba yao na vile vibinti (kaka yangu) alibaki kuangalia chini utadhani kajamba ukweni na domo lake Kama kipimio cha njegere..!

Mwisho wakuu tuwe makini na malezi ya watoto wetu...
 
Top Bottom