Jambo gani umewahi kusingiziwa likakudhalilisha kwenye jamii?

baada ya kumaliza chuo rafiki yangu mmoja aliniita nije nimsaidie kazi ya kuuza electronic devices pande za chuo, jamaa alikua mjasiriamali toka tupo chuoni. Kwa kuwa sikuwa na mishe nikakubali.

nikafikia kwake ambapo pamoja na mimi pia alikua amemuita ndugu yake mmoja ili tusaidiane nae kutembeza devices kwenye hostels, sasa siku moja nikapokea simu niende kijijini kwetu, kwa iyo nikaondoka.Nikakaa kama siku nne hivi.

Siku narudi tu Nikaulizwa Swali : Hivi wakati Unaondoka Ulichukua Calculator Mbili..? Nikasema hapana. Jamaa akasema huenda walijichanganya wakati wa kufunga Hesabu. Nikadhani yameisha kweli, Kumbe wenzangu wamelihifadhi Vichwani mwao.

Siku ya siku ikatokea tumepishana kwenye mazungumzo ya biashara ndo wakalikumbushia lile tukio huku wakisema Wana Uhakika zile Calculator zilipotea Siku ile Nilipoondoka mimi.

Waliniaibisha sana yaani mpaka majirani zetu walikua kimya kutusikiliza mpaka mwisho, wakaonekana wao ndo washindi.
Mie Nilikua Kawaida tu, ikabidi palepale nianze kukusanya kila kilichokua changu taratiiiibu, nakavaa nguo zangu, nikabeba begi langu Mgongoni, nikawafuata wale majirani waliokua wakisikiliza, Nikawaaga.

Nikajisemea Moyoni: "Ukweli wa Jambo Hili Utajulikana Tukifika Mbinguni"
Mbinguni tena...
 
Kuwa mkweli ,huyo mwanamke hujawahi kulala nae hata Mara moja ,kwanini ukubali kwenda kupima DNA na hujawahi lala nae hata Mara moja.

Duuuh nshawahi kusingiziwa mambo mengiii ila katika yoote haya ya wanawake yananikeraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa mpaka leo.

1. Nilishawahi kuwa karibu sana na dadangu mmoja bhasi muda nikiwa free lazima nipitie shop kwake na lazima ataniacha na chochote mfukoni, bhasi kipind nipo form6 sikufanikiwa kurudi home na wazazi wakawa wamehamishiwa sehemu nyingine kikazi bhasi nimemaliza form 6 nimerudi home (makazi mapya ya wazazi) tukawa tunawasiliana kawaida tuu na sista mwezi wa nane binamu yangu(wakiume) akanipigia simu "OYA VIPI MWENZIO AMEJIFUNGUA" nani? "DADA AKO ....." Nikamkatia simu simu nukaruka kwa DADA vipi nasilia una mtoto? ,jibu lake "POLE KWANI HUJUI KUWA WEWE NDIO BABA MJOMBA? , KILA MTU ANASEMA ETI WEWE NDIO BABA MTOTO" bhasi kwa kuwa alikua sista angu sana nikachukulia poa ila mpaka mtoto amekua ndio watu wamekuja kujua sio mtoto wangu.

2.Katika makazi mapya tulikua na beki tatu anaimba kwaya bhasi akawa na mchizi wake yupo kwenye kwaya humohumo bhasi kuna siku usiku huyo jamaa akaja home na kademu, akamuomba beki tatu kale kademu kalale pale home beki tatu akaniita, Binafsi nikaona sio shida kwa usiku mmoja tuu kakalala na beki tatu kesho yake pia kakabaki pale home ila siku ya tatu kakaondoka bhasi kalipoondoka kumbe beki tatu alikapatia namba yangu kuwa wakitaka kuwasiliana kapige kwangu, Siku moja usiku nikaona call kupokea nikauliza nani? MIMI FULANI NATAKA KUONGEA NA ..... nikampelekea simu wakamalizana baada ya siku kadhaa tena kakapiga simu nikapeleka simu wakamalizana huko, baada ya simu kurudi nikatumiwa sms SIO KILA NIKIPIGA SIMU NATAKA NIONGEE NA .......(JINA LA BEKI TATU) nikajibu poa ila nilikua nimekapiga gepu sana nikikachukulia kama mdogo, BAADA YA SIKU KADHAA KAKANIPIGIA SIMU KUWA KAPO arusha kidogo tena kakaniomba hela ya nauli maana kanaumwa halafu kapo DAR nikakapotezea zikapita wiki tatu nikatuma sms WEWE MZIMA AU ULISHAKUFA? bhasi t6atzo lilianzia hapo kwnye hiyo sms, kumbe jamaa aliyeniombe kalale nyumbani siku moja alikapangia gesti na akaandika na mke wake jamaa kapiga show mpka demu kajaa mimi kisa sms NIKATUHUMIWA NIMEKAPA UJAUZITO, bhasi ishu ikavuma hadi kanisani kila mtu akawa ananinyoshea kidole ila mwaka jana jamaa amekaweka ndani na wanamtoto tayari, baada ya miaka mitano ukweli ndio unajulikana

3.Hili ndio limenifanya kuandika mimi sio mwandishi mzuri wala sio mchangiaji ila kuna madhira unapitia inakubdi tuu kutoa la moyoni, baada ya kupitia changamoto kadhaa za maisha niliamua kujichimbia bushi fulani ili kufanya kilimo bhsi mwanaume nikakomaa kwa kilichonipeleka, Nilipanga geto la nje kwnye nyumba yenye mabinti wawili bhasi kuna siku nimetoka shamba nikamkuta binti wa mwnye nyumba anatoka geto kwangu aliponiona akanikimbia sikutilia maanani sana maana nilishahisi kuna mtu huwa anaingia mle geto na tunashare nae mafuta ya kupakaa sikuona shida sanaaaa juu ya hilo ila siku nyingine asijue nipo ndani aliongea neno moja linaukakasi sana "kwa kilugha" na aliekua anazungumza nae akamtonya kumwambia kuwa unaemsema anaelewa hiyo lugha bhasi akamuuliza kwani yupo? akamjibu nilisikia mlango umefunguliwa bhasi dogo akaja kuthibitisha akasukuma mlango ukawa umefungwa kwa ndani, jion yake nikaenda kwa jamaa mmoja nikamuuliza hichi kijiji nasikia akija mgeni huwa haondoki kuna ukweli hapo? akaniambia usijaribu kumtaka binti yoyote hapa kjijini watakuloga utaishia hapahapa nikaonyweshwa na mifano ya watu waliokuja pale mwisho wa siku wakabaki kama walivyokuja baada ya kujichanganya na hizo ammbo, bhasi toka hapo nikawa najichunga sna hata kula nakula kwa mawenge labda nikipata time ndio napika mwenyew, siku moja sina huili wala lile nasikia binti wa yule mama ni mjamzito duuuh na tetesi inasemekana ni mimi ndio nimefanya hyo kazi kwamba huwa nawahi kutoka shamba ili nimlale hyo binti, Duuuuh hiyo kaul iliniumiza sana ukichanganya na maisha ninayopitia bahsi nikaunganisha dot na kauli aliyoongea kwa kilugha yule binti nikawa nimepata jibu nusu bhasi nikisubiri mazao yangu yakomae ndio nisepe kimyamya, siku moja nachukua boxer nikaoge nakuta mpangilio niliouweka sio ule na boxer zote zimefukiwa na kukunjwa vizuri kitu amabcho kilinifilisha sanaaaa, nikarudi kitaa kukusanya data jamaa wakaniambia wanawake wa hicho kijiji wanatumia sana nguo za ndani kuloga wanaume bhasi niatupa boxer zooooote nikavuna matitikiti niksepa mazima ila niliacha nyanya zangu sijavuna.

4.Huu wa mwisho ndio bado nipo nao, nipo maeneo fulani na kikubwa kilichonileta huku ni biashara bhasi nilikua naenda church kusali nitatoakea kuwa na mazoea na dada mmoja na nilikua nahitaji connection za vijiji fulani wanalima sana mpunga, bhasi yuile adada akaniambia poa tutakua pamoja, sikuwa najua kazi yake ila nilihisi ni mfanyabiashara kumbe ni beki tatu ila yupo huru kufanya mambo yake, katika mazoea na ukaribu kumbe demu alikua anajitangaza natoka nae na tunampango wakuoana ila alifanya bila mimi kujua, baadae nikawa simuelewi yaani analeta mapenzi m,engi afu nikimwambia anipe hizo connection anazingua utafikiri yeye ndio kanipa mtaji bhasi nikaona hatuendani nikaachana nae akipiga simu sipokei, demu mwngne wa mule church akanipa connection ila sababu ya ugeni na nilikua nimeshakaa muda mrefu hapa hela ikawa imepungua nikamuomba huyu dada anitafutie mkopo afu mimi nitakua narejesha taratibu kupitia yeye dili likafanikiwa bhasi ikabd niwe close na huyu dada ili kujenga uaminifu, Kumbe hili demu ambalo ni beki tatu linaujauzito na lengo l;ake linipakazie mimi niulee, bhasi mimi bilka kujua nashangaa siku naitwa na katibu wa kanisa AKANIULIZA KIJANA UNAMAHUSIANO NA HUYU BINTI ? "ambaye amenidhamini kwenye mkopo " nikajibu HAPANA NI UKARIBU TUU WA BIASHARA NIKAMUONESHA NA SMS ZA MAREJESHO YA HELA, AKANIULIZA TENA VIPI NA YULE BINTI ULIEMPA UJAUZITO MBONA UMEMTELEKEZA? ikabd nimuulize binti yupi tena akaniambia mliekua karibu siku za nyuma NILIKOSA JIBU MAANA NILIKUA SIJUI KAMA NII MJAMZITO, anyway tulipoachana na katibu wa kanisa nikampigia simu demu nikamzingua sana, kumbe bhasi mimba ni ya boss wake mume wa dada yake wanakaa naye na mimba ni kubwa hawezi kuitoa miezi6 ila alitaka kuitoa ikiwa na miezi mitano dadaake akamzingua, akaona suluhisho ni kujiua bhasi akanunua sumu kainywa halafu kanitumia sms mimi kuwa " UNAYACHUKUA MAISHA YA MTU HII DAMU ITAKULILIA MILELE" jioni napigiwa simu na huyo demu alienidhamini ananiambia kimbia ondoka kabisa hapa, ...... amekunywa sumu na sasa yupo ICU nadhani sms yake uliipata so wanakutafuta nikamwambia sikimbii wala siondoki wakitaka waje au hata mimi mwnyw nitawapigia simu, MUNGU NI MWEMA demu alipona hajafa na mimba haijatoka ila bado demu amebaki na msimamo wake kuwa mimba ni yangu na jamii inaniangalia kwa jicho baya eti nimekataa mimba na nimesababisha mtu atake kujiua, ANYWAY BIASHARA IMESIMAMA NA KESI IMEISHA IJUMAA ILIOPITA TUNASUBILI MTOTO TUPIME DNA THEN MENGINE YATAFUATA ILA KWA HILI LIMENIUMIZA KULIKO YOOOOOTE NA SIONI NAMNA YA KUMSAMEHE HUYU DEMU KUNA MUDA NATAMANI NIMNUNULIE SUMU INAYOUA MAPEMA ILI ATANGULIE TUU MAZIMA MAANA AMENICHAFUA NA AMESABABISHA UCHUMI WANGU UMEYUMBA NA DENI LIMEONGEZEKA. YAANI HAPA NI STRESS TUUU
 
Kuna demu apa kitaa kalikuwa kanatangaza maneno eti mimi natembea nako, ikabidi nikafate nikaulize kulikoni, akasema "oohn watu waongo mara sijui nini nami wameniambia" nikasema basi hamna tabu ok. Naomba tuwe wote kama hutojali mtoto kakubali haraka sana nami nikaenda kujilia tunda kimasihara
Lengo lake lilitimia kimasihara!
 
Pale mheshiwa alipo tangazia Tanzania na Dunia kuwa Mimi nina gonga wake za watu na alisha nikanya sikusikia wakati haikuwa kweli
Ile ni udhalilishaji mkubwa, na kwa mwenye akili timamu ni dhahiri yeye ndio anamfuatilia (anajaribu kujihusisha)kwa karibu mtumishi mmoja tu kupita kiasi.
 
Nilisigiziwa nimeiba laki 300000 kwenye pesa za kununulia mzigo nilikataa siyo mimi wakasema ni mimi na kazini nikasimamishwa nashukuru Mungu walikuja kujua kweli
Siyo mimi wakaomba msamaha na kazini nikarudi paka leo tupo vizuri
Hela nyingi sana hizi yaani 30,000,000,000, kwa kifupi bilioni 30!
 
Niliwai singiziwa nataka kuchoma shule bweni,nilichapwa parade na kufukuzwa shule form 2 ilikua,tokea hapo mambo hayakua sawa
 
Nasingiziwa sana kuwa mtu wa mademu wengi jambo ambalo sio kweli.
Hii inatokana na namna ninavyoongea nao.
Kuna wakati hili jambo linaniudhi sana sana kwani kila msichana ninayesema naye au kuwa na ukaribu watu hunihesabu kuwa nimekula.
Maybe una shobo sana
 
Nilisingiziwa kubaka mtoto (13) na jamaa (ndugu) kisa aliona wivu maendeleo yangu. Miaka 30 sio mchezo. Nililala polisi siku moja, ikaonekana ni uwongo nikaachiwa huru. Huyo jamaa kumsamehe ni mpaka Mungu amsamehe shetani.
OMG na hako katoto kalishiriki kukuchoma?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom