Jambo ambalo wengi hawalijui: Hakuna kiongozi wa kisiasa atakayeshitakiwa kipindi cha uongozi wake au baada ya uongozi wake, ilimradi awe mwanaCCM

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,701
36,120
Habari wapendwa!

Mimi si mwandishi mzuri na huwa ni mzito kuandika jumbe ndefu. Habari ni kwamba viongozi wa kisiasa chini ya serikali ya CCM hawawezi kushitakiwa kwa makosa yao waliyotenda kipindi cha uongozi wao.

Wanawaza kuwajibishwaa kwa namna tofauti ila sio kuwapandisha kizimbani. CCM ni kama wameapa kulindana.

Hamtakuja kusikia Sabaya , Kangi Lugola na wengine wamepandishwa kizimbani.
 
Kama hujalijua sakata la Manji ni heri ungeuliza watu wakuelezee kiundani nini kilipelekea akae ndani.
Manji issue yake ilianzia kipindi cha kuelekea kura za maoni CCM Julai 2015
Haya nijuze nakusikiliza
 
Haitawezekana sababu ya unafki wa watanzania hasa walioko mlengo wa upinzani.

Awamu ya 4
Kipindi kikwete yupo madarakani walitamani raisi atayefuata amshtaki kikwete pamoja na akina ridhiwani kwa kuwa wameifilisi nchi
Baada ya kuingia raisi mwingine baada ya mwaka wakabadilika na kuanza kuwa-miss, na hivyo kuanza kuonekana waliokuwa awamu ya nne ni malaika.

Awamo ya 5
Kipindi magu yupo madarakani wakatamani ashtakiwe pamoja na viongozi wake wote wa serikali(wakasahau kabisa awamu ya 4)
Ghafla waliopo awamu ya 5 mfano makamu wa raisi kageuka tena malaika, washasahau.

Na baada ya muda wataanza tena kuwa miss
Ndio tunaishi hivi, Wala usipate tabu. Baada ya muda watatamani tu mama Samia nae ashtakiwe na awamu itayomfata(watasahau awamu ya 5)
 
Haitawezekana sababu ya unafki wa watanzania hasa walioko mlengo wa upinzani....
Suala la kusahau hilo ninaliunga mkono.

Watanzania wakiletewa tukio moja husahau lililopita.

Utawala wa Magufuli unapaswa ushitakiwe kabisa from top to down.
 
Sahau hayo..
Trust me, CCM ni wajanja waliokubaliana kula pamoja .
Ukiwa na kashfa mzito wanakupumzisha pembeni ila hufungwi na wala hushtakiwi
Wanaofungwa ni watumishi wa chini wanaolamba za brush kumkuta ndani mtu kachukua elf 50,au laki ni kitu cha kawaida lkn sio kina sabaya au bashite sahau hilo.Hata uhujumu uchumi wengi ni waliokuwa na bifu nao au waliogoma kutii maagizo
 
Yes. Umenena vyema.
Mijizi inapumzishwa kwa muda kusubiria Watanzania wasahaulifu wasahau warudi ulingoni
 
Habari wapendwa!

Mimi si mwandishi mzuri na huwa ni mzito kuandika jumbe ndefu. Habari ni kwamba viongozi wa kisiasa chini ya serikali ya CCM hawawezi kushitakiwa kwa makosa yao waliyotenda kipindi cha uongozi wao.

Wanawaza kuwajibishwaa kwa namna tofauti ila sio kuwapandisha kizimbani. CCM ni kama wameapa kulindana.

Hamtakuja kusikia Sabaya , Kangi Lugola na wengine wamepandishwa kizimbani.

Mramba na Yona walikuwa viongozi wa NCCR?
 
Back
Top Bottom