Jambazi sugu ajisalimisha kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya baada ya kukoswa koswa na risasi za Polisi

Yaani kakoswa na risasi za Polisi halafu anajisalimisha na kupewa milioni pamoja na pongezi juu du!

I wish I could be IGP
 
... in short polisi waliokuwa wakimtafuta "kwa muda mrefu sana" sasa wameshajua yuko wapi wakamchukue otherwise ni usanii juu ya usanii.
 
Safi sana. Anaeomba husamehewa hata na Allah seuse sisi binadam.

Namshauri kijana ashike swalat na asiache na Allah atamsameh.

Nawaomba na wale wote aliowakosea wamsameh.
 
Aisee! yaani unakiri ulikuwa jambazi sugu, umefanya matukio mengi lakini unapewa hela badala ya kupelekwa polisi? Basi sawa. Sijui RC atampa ngapi na yeye? Hongera kwa kupata BIKO kijana.
 
Jambazi sugu aitwaye Ali Mtemi amejisalimisha katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya baada ya kukoswa koswa kuuwawa na Askari wa doria mara nne katika Wilaya ya Kigamboni huku baadhi ya wengine katika kikundi chake wakiuwawa na kukamatwa.

Polisi wamekuwa wakimsaka kwa muda mrefu ambapo amekuwa akijificha katika mikoa mbalimbali lakini hatimaye ameamua kujitokeza na kwenda kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni ili kuomba msamaha kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigamboni.

Ujasiri wake wa kujisalimisha umepongezwa na Kamati ya Ulinzi ya Ulinzi na Usalama, ambapo Mkuu wa Wilaya amemuahidi kumsaidia shilingi 1,000,0000 kama mtaji wa biashara baada ya kuahidi ameachana na ujambazi mbele ya wazazi wake na mjomba wake.

Mkuu wa Wilaya amemuomba akawe ni kioo kwa vijana wengine ambao bado wanafanya vitendo vya wizi na ujambazi katika Wilaya ya Kigamboni.

NB: Kumbe hata majambazi wanaogopa kifo!

Video ya jambazi sugu akijisalimisha kwa Mkuu wa Wilaya.






Movie
 
Mahakamani anapelekwa lini?au kiki za uchaguzi maana CCM mna vijimambo.
Nadhani hafikishwi mahakamani na sidhani kama ni kiki za Uchaguzi kwa sababu tunaambiwa ''CCM hawana haja ya kufanya kiki ili wachaguliwe kwa sababu wanaiba kura''!

Huwezi kusema wanafanya kiki kwa sababu ya chaguzi halafu hapo hapo unasema huwa wanaiba kura!
 
Nadhani hafikishwi mahakamani na sidhani kama ni kiki za Uchaguzi kwa sababu tunaambiwa ''CCM hawana haja ya kufanya kiki ili wachaguliwe kwa sababu wanaiba kura''!

Huwezi kusema wanafanya kiki kwa sababu ya chaguzi halafu hapo hapo unasema huwa wanaiba kura!
Sasa tutaaminije hawaibi kama hakuna maigizo na sanaa kama hizi?
 
Insanity! Sasa kama kajisalimisha si apelekwe rumande kusubiri kesi? Kosa halina expiry date, hadi ulilipe. Sasa na milioni 1 juu? Na hivyo vyombo vya habari vilijuaje ataenda kujisalimisha siku hiyo?

Maigizo mengine ya kitoto sana.
Wazee wa kupingaaa
 
Back
Top Bottom