Jambazi sugu ajisalimisha kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya baada ya kukoswa koswa na risasi za Polisi

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,041
2,000
Jambazi sugu aitwaye Ali Mtemi amejisalimisha katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya baada ya kukoswa koswa kuuwawa na Askari wa doria mara nne katika Wilaya ya Kigamboni huku baadhi ya wengine katika kikundi chake wakiuwawa na kukamatwa.

Polisi wamekuwa wakimsaka kwa muda mrefu ambapo amekuwa akijificha katika mikoa mbalimbali lakini hatimaye ameamua kujitokeza na kwenda kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni ili kuomba msamaha kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigamboni.

Ujasiri wake wa kujisalimisha umepongezwa na Kamati ya Ulinzi ya Ulinzi na Usalama, ambapo Mkuu wa Wilaya amemuahidi kumsaidia shilingi 1,000,0000 kama mtaji wa biashara baada ya kuahidi ameachana na ujambazi mbele ya wazazi wake na mjomba wake.

Mkuu wa Wilaya amemuomba akawe ni kioo kwa vijana wengine ambao bado wanafanya vitendo vya wizi na ujambazi katika Wilaya ya Kigamboni.

NB: Kumbe hata majambazi wanaogopa kifo!

Video ya jambazi sugu akijisalimisha kwa Mkuu wa Wilaya.

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
19,697
2,000
Insanity! Sasa kama kajisalimisha si apelekwe rumande kusubiri kesi? Kosa halina expiry date, hadi ulilipe. Sasa na milioni 1 juu? Na hivyo vyombo vya habari vilijuaje ataenda kujisalimisha siku hiyo?

Maigizo mengine ya kitoto sana.
_______________________________________
IG: @marble_na_granite
 
MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,041
2,000
Insanity! Sasa kama kajisalimisha si apelekwe rumande kusubiri kesi? Kosa halina expiry date, hadi ulilipe. Sasa na milioni 1 juu??! Na hivyo vyombo vya habari vilijuaje ataenda kujisalimisha siku hiyo? Maigizo mengine ya kitoto sana..
Mkuu;
Tumia hata akili ya kawaida kama unayo kutambua kuwa baada ya Jambazi kujisalimisha kwa DC, vyombo vya habari viliitwa.

Vyombo vya habari Dar es Salaam havina habari, hata wewe ukiviita kwenye tukio lolote vinakuja kwa wingi.

Kuhusiana na makosa aliyofanya, hapo ndipo tunaweza kufanya mjadala kama anatakiwa apelekwe rumande au apewe onyo kama njia ya kuwafanya majambazi wengine wajisalimishe na kuahidi kuacha ujambazi.

Kuna wengine watasema anatakiwa kupelekwa mahakamani na kuna wengine watasema njia iliyotumika ni nzuri ili kutoa fursa kwa wezi na majambazi wengine kuiga mbinu aliyotumia ya kujisalimisha.
 
FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
19,697
2,000
Mkuu;
Tumia hata akili ya kawaida kama unayo kutambua kuwa baada ya Jambazi kujisalimisha kwa DC, vyombo vya habari viliitwa.

Vyombo vya habari Dar Es Salaam havina habari, hata wewe ukiviita kwenye tukio lolote vinakuja kwa wingi.
Kwahiyo wameitwa kwenye igizo sio? Basi sawa..
 
Baba Watoto

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
390
500
Kujisalimisha ni tofautina kukiri kosa/ makosa na kueleza namna ulivyohusika. I stand to be corrected.
 
FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
19,697
2,000
Kujisalimisha ni tofautina kukiri kosa / makosa na kueleza namna ulivyohusika. I stand to be corrected.
Kujisalimisha maana umetafuta usalama kwa kujipeleka mwenyewe kabla hawajakukamata wao, sasa kama kajisalimisha basi apelekwe mahakamani
 
Kertel

JF-Expert Member
May 11, 2012
3,826
2,000
Duh,jambazi sugu anayetafutwa sana na polisi(means wanazo taarifa zake za ujambazi)amejisalimisha na kuachwa akawe kioo kwa jamii(amesamehewa) bila kupelekwa mahakamani.
 
Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
14,593
2,000
Jambazi sugu aitwaye Ali Mtemi amejisalimisha katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya baada ya kukoswa koswa kuuwawa na Askari wa doria mara nne katika Wilaya ya Kigamboni huku baadhi ya wengine katika kikundi chake wakiuwawa na kukamatwa.

Polisi wamekuwa wakimsaka kwa muda mrefu ambapo amekuwa akijificha katika mikoa mbalimbali lakini hatimaye ameamua kujitokeza na kwenda kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni ili kuomba msamaha kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigamboni.

Ujasiri wake wa kujisalimisha umepongezwa na Kamati ya Ulinzi ya Ulinzi na Usalama, ambapo Mkuu wa Wilaya amemuahidi kumsaidia shilingi 1,000,0000 kama mtaji wa biashara baada ya kuahidi ameachana na ujambazi mbele ya wazazi wake na mjomba wake.

Mkuu wa Wilaya amemuomba akawe ni kioo kwa vijana wengine ambao bado wanafanya vitendo vya wizi na ujambazi katika Wilaya ya Kigamboni.

NB: Kumbe hata majambazi wanaogopa kifo!

Video ya jambazi sugu akijisalimisha kwa Mkuu wa Wilaya.

Tumezoea movi za magufuli aki ekti kumsaidia mama mnyonge pesa ya matibabu, hii movi actor ni nani? DC au jambazi?
 
kedekede

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
3,983
2,000
Je uhakika wa kwamba hatarudia vitendo hivyo unapatikanaje?awaonyeshe wenzake walipo maana ni mtandao,coz anawajua kisha tumsamehe.Katika ujambazi wake amedhuru watu wangapi?ameua watu wangapi?amepora watu wangapi?Fidia ya hao watu itatolewaje ili waridhike?Utawazuiaje watu walioumizwa na huyu mtu kwa njia yoyote ile ili wasije kumdhuru baada ya mkuu wa wilaya kumsamehe?Sijapendezewa!
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
46,884
2,000
Mkuu;
Tumia hata akili ya kawaida kama unayo kutambua kuwa baada ya Jambazi kujisalimisha kwa DC, vyombo vya habari viliitwa.

Vyombo vya habari Dar es Salaam havina habari, hata wewe ukiviita kwenye tukio lolote vinakuja kwa wingi.
Wanarudiaga Hawa........

Ova
 
Top Bottom