Jambazi Lasalimisha Silaha Kigoma, Laachiwa Huru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jambazi Lasalimisha Silaha Kigoma, Laachiwa Huru

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gudboy, Jan 28, 2010.

 1. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Jeshi la polisi mkoani Kigoma limemwachia huru kwa msamaha maalumu mkazi mmoja wa kijiji cha Nyamidaho wilayani Kasulu aliyesalimisha kwa serikali ya kijiji, silaha ya kivita aliyokuwa akiitumia kwa ujambazi.</SPAN>
  Kamanda wa polisi mkoani Kigoma kamishina msaidizi wa polisi George Mayunga amemtaja mtu huyo kuwa ni Nathan Morton aliyekuwa akitajwa kuimiliki silaha hiyo kinyume cha sheria.

  Kamanda Mayunga ameeleza kuwa, Morton amejisalimisha kwa mwenyekiti wa kijiji Bw. Henriko Kimorimori baada ya ushawishi mkubwa uliomtaka kujisalimisha kabla ya jeshi la polisi kufanya msako.

  Amebainisha kuwa bunduki iliyokamatwa ni SMG yenye namba za usajili 109484 na kwamba jeshi la polisi kwa kutambua umuhimu wa mtu kusalimisha mwenyewe limempa msamaha na kipindi cha matazamio.

  Aidha katika tukio hilo lililotokea ijumaa iliyopita, serikali ya kata ya Nyamidaho imeagizwa kuunda timu maalumu itakayofuatilia mwenendo wa maisha ya Bw. Nathan Morton ili kuhakiki kama hajihusishi na uharifu zaidi.

  Kufuatia tukio hilo mkuu wa polisi mkoa wa Kigoma George Mayunga ametangaza rasmi kutoa msamaha kwa jambazi atakayesalimisha silaha kwa hiyari katika kipindi cha mwezi mmoja.

  Amesema endapo mmiliki haramu wa silaha atajisalimisha jeshi la polisi halitamchukulia hatua yoyote zaidi ya kumpa ushauri nasaha wa kubadili tabia na kuacha uhalifu.

  Hata hivyo kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma amesisitiza kuwa operesheni kamambe inaendelea ili kuhakikisha wamiliki wa silaha na watekelezaji wa vitendo vya ujambazi wanakamatwa na kufikishwa katika mkondo wa sheria.

  Na katika tukio jingine lisilo la kawaida, mkazi mmoja wa manspaa ya kigoma Ujiji Bw. Hassan Baguma anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kukamatwa wakati akifanya shambulio la hatari kwa kuwakata kwa panga mkewe, shemejiwe na mama mkwe wake.

  Tukio hilo limetokea jumanne wiki hii katika mtaa wa hali ya hewa mjini Kigoma umbali wa mita 200 toka makao makuu ya polisi Kigoma wakati Bw. Hassan alipofika ukweni kwake na kuanza kuwashambulia wana ndugu hao kwa mapanga na kuwajeruhi vibaya.

  Kamanda George Mayunga amewataja waliojeruhiwa kuwa ni mke wa mtuhumiwa Bi.Mwamini Francis, Shemejie aliyetambuliwa kwa jina la Emanuel Baguma na mama mkwe wake ajulikanaye kwa jina la Asia Francis.

  Majeruhi wote wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Kigoma Maweni ambako wanaendelea kupata matibabu.

  Chanzo cha Bw. Hassan kuwacharanga mapanga wanandugu hao kinatajwa kuwa ugomvi wa ndoa baina yake na mkewe Bi. Mwamini ambaye mumewe anamtuhumu kumfilisi na kisha kumkimbia na kuambatana na wanaume wengine kwa ushawishi wa mama yake na ndugu wengine.
   
 2. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  upuuzi wa jeshi la polisi!!
  sawasawa na kuona wanapongezwa kwa kuuwa watu wanaoshukiwa kuwa majambazi!!!

  Hii ni sawa na kumpa ushindi Zombe
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,000
  Trophy Points: 280
  Jamaa kasalimisha bunduki moja tu wakati anazo kibao ghalani mwake.
  Kweli jeshi letu lina mbinu za kisasa za kupambana na ujambazi.
   
 4. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Lakini jamani tuseme ukweli. Huyu jamaa anaangaliwa na watu wote nyendo zake sio na polisi tu. Kama kweli alikuwa jambazi atakuwa msaada sana kuwafichua majambazi wenzake wenye viburi. Sema tu yeye mwenyewe yuko katika hatari ya kusiginwa na wenzake kwa hofu ya kuanikwa mambo yao. KIla kazi ina kustaafu, huyu bwana kastaafu ujambazi ni budi aheshimiwe na jamii angalau kuliona hilo.

  Leka
   
 5. Power to the People

  Power to the People JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2010
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 1,193
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Hawawezi wakawaacha wakati polisi ndio washirika wao wakuu. lazima wawamalizie mbali wasije kuwataja kwenye interrogation. we haujui?
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Mamlaka ya kusamehe wahalifu kayapata wapi kisheria, tunaomba atueleze. Vile vile na criteria ya kumsamehe huyo mtu maana kukutwa na bunduki bila kibali ni kosa la jinai.

  SMG ni silaha zinazopatikana polisi na kwenye majeshi amecheki na maghala mengine ya silaha ili kubaini silaha yenye namba hiyo ilikuwa wapi na ilitokaje kwenye ghala la silaha kable ya kumuachia. Kwani kama iliibiwa basi hilo ni kosa kwa aliyeiba na aliyepewa wote ni watuhumiwa.
   
Loading...