Jambazi lapigwa risasi likienda kuiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jambazi lapigwa risasi likienda kuiba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 13, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  JESHI la Polisi wilayani Bunda linamshikilia jambazi mmoja, James Joseph (17) mkazi wa Kijiji cha Masanza Kona wilayani Magu, baada ya kupigwa risasi na mfanyabiashara mmoja wa Kijiji cha Kinyambwiga wilayani hapa ambako lilienda kuiba na wenzake.

  Akizungumza na Tanzania Daima jana katika Kituo cha Polisi Bunda, mfanya biashara huyo ambaye majambazi hao walienda kuiba kwake, Nyamhanga Sisa, alisema kuwa tukio hilo lilitokea hivi majuzi majira ya saa saba usiku nyumbani kwake katika Kijiji hicho cha Kinyambwiga.

  Alisema kuwa siku ya tukio majambzi hao ambao inasadikiwa walikuwa watano, wakiwa na silaha za jadi walivamia nyumbani kwake ambapo walivunja milango ya nyumba zaidi ya mbili na kuanza kuwapiga wake zake pamoja na watoto huku wakiwaomba pesa.

  Mfanyabiashara huyo alisema kuwa wakati wanafanya uporaji huo yeye alikuwa mjini Bunda na ndipo alipopigiwa simu na majirani zake, ambapo aliondoka usiku huo na kwenda na kwamba alipokaribia nyumbani kwake alisikia vurugu za watu wakilia.

  “Baada ya kufika pale nyumbani kwangu niliingia kwenye nyumba ya mke mkubwa ambapo nilichukua bunduki na kwa bahati nzuri hawa majambazi mmoja wao aliangusha kiatu na baada ya muda nilimuona akirudi, ndipo nilipompiga risasi pajani na akaanguka papo hapo.

  Polisi wamesema kuwa wanaendelea kumhoji jambazi huyo ili aweze kuwataja wenzake waliohusika katika tukio hilo ili waweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yao.
   
 2. E

  Elias Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Jul 11, 2009
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  dahh!! mbona kijana mdogo sana? anasitahili kunyongwa.
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Anastahili kunyongwa??Kwa lipi??
   
Loading...