Jambazi dar latunguliwa toka juu ya paa kwa risasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jambazi dar latunguliwa toka juu ya paa kwa risasi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Pdidy, Jul 25, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  Ukisimuliwa sakata hili utazani sinema ya za kivita nchini china la hasha ni shurba iliotokea mjini dar es salaam hapo jana jambazi mmoja aitwae jumanne jana alipanda juu ya paa la nyumba ya mtu na kisha kuanza kumimina risasi bashasha..kwa polisi waliokuwa katika harakati za kupambanana majambazi hayo yaliyovamia hotel...

  .hata hivyo majibizano ya risasi yaliishia mtu huyo kutunguliwa juu na risasi na polisi....tukio hilo lililowavutia watu wengi lilitokea jana saa 9alasiri eneo la manzese madizini kwenye hotel ya bismark kamanda wapolisi wa kinondoni amesema

  akisimulia zaidi tukio hilo mesema majambazi manne yalifika kwenye hotel hiyo kwa nia ya kufanya uhalifu...lakini kabla ya kufanikisha azma yao hiyo polisi walipata taarifa na kwenda eneo ya tukio na kuyazingira.....
  Aidha amesema baada ya kuyazingira jambazi ambalo alikuweza kufahamika maramoja halisi..maarufu kama j4 liliamua kupanda juu ya paa ya nyumb ya jirani....akasema likaanza kumwaga risasi rashasha kwa polisi kama vile mastrling wa mikanda ya kivita wanavyofanya....hata hivyo walijibu kwa ustadi wa hali juu wakalitungua na kisha kuchukua bunduki hiyo smg iliyokuwa imebaki na risasi 22 na magazine 2

  polisi walifanikiwa kuyakamata majambazi mengine matatu ambayo majina yamehifadhiwa kwa sababu ya uchunguzi zaidi...

  Duh marehemu wameamua kumtaja j4..hawa walio hai yamehifadhiwa kazi kwenu polisi....msije wakawa mapolisi/wanajeshi wastafu mkashindwa kututajia...maana sasa hivi wanandugu majambazi wakiingia course wamepitia ama jeshini/polisi

  hongereni;tungeomba iwe hivi kila siku na si kwa wengine mnaulizia wameshaondoka ...wana muda gani...then ndio mnaingia...tutawatafsiri vingine
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ukiona wamewahi basi ujue dili iliharibika ,huenda mmoja hakuwemo kwenye mgawo.Maana sijawahi kusikia polisi kuwahi ila kutakuwa na kutokuelewana kwenye mipango nyeti. Hapo pamechomewa tu.

  Mimi ni mwenyeji wa Dar na naijua chini juu ,ninavyofahamu hawa majambazi wakuu wa kutumia silaha nzito nzito karibuni wote wanajulikana na polisi ,au wanajuwana ,na hawa wapo kwa makundi ,na ukitokea ujambazi mahali fulani inajulikana hao ni wa kundi gani na mkubwa gani au kigogo gani ndie watu wake ,sijui kama mtakumbuka kuna mke fulani au sijui ni mbunge yule alishambuliwa na majambazi ,na majambazi hao kutoweka ,ila haikufika asubuhi wote wamekamatwa.
  Kuna mkuu fulani alikwenda safari aliporudi akakuta nyumba yake imevunjwa na kuibiwa ,akampelekea habari mkuu wa kituo kuwa isifike siku ya pili vitu vyake vyote vimerudishwa ,kwa kweli hata haikutimia vitu vilivyoibiwa vilipatikana na kurudishwa lakini walioiba hawakupatikana.

  Amini usiamini hiyo ndio Tz ,polisi na majambazi wanajuwana ,sasa hapo lazima mambo yalikwenda hovyo tu ,akuna jingine.

  Kule mikoa ya kusini ukisafiri bila ya escort unakutana na majambazi lakini ukipata japo polisi mmoja hukuti hata abiria ,mtasemaje na hapo ? Kuna siku tulikuwa tunatoka kwenye kuwinda ,tukakutana na majambazi ,ila tulishituka mapema na kuweka bunduki zetu sawa wao walikuwa watatu sisi tulikuwa watu kama tisa na bunduki zetu za kupigia nyati ,ukubwa wa risasi kama keroti ,tukawahi kujipanga ,na walipoona tuna zana si za kawaida na tumeanza kutoa onyo waliingia mitini. Na kusema kweli tulikuwa hatujapoa kutoka porini na hivyo tukapandwa na jazba ya kupambana nao.
   
  Last edited: Jul 25, 2009
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  Ukiona wamewahi basi ujue dili iliharibika ,huenda mmoja hakuwemo kwenye mgawo.Maana sijawahi kusikia polisi kuwahi ila kutakuwa na kutokuelewana kwenye mipango nyeti. Hapo pamechomewa

  UMESOMEA HAVARD NINI???UR SUCH A GENIOUS...Personal nimeliona hili nikajua hawa hawakuelewana kwenye mgao hakuna jipya.....nilishawahi kutoa thread moja kuna wale vijana wawili walishikwa na magari ya wizi kilimanjaro wakaondoka usiku ...wakiwa wanakunywa pale kimara baruti huku wakipanga jinsi ya kuondoka....ndugu yangu mmoja alie chuo kikuu akanieleza yote ..baada ya siku jamaa wakakamatiwa pale PANAFRICA....nanilitoa kila uchafu...na hata baada ya kukamatwa waliletwa hapa dar...mmoja wa alie kwenye system yao akaenda mkono kwa mkono kwa kamanda mkuu wa mkoa wa dar es salaama ....siku wanaenda nikaiwasha hapa jamvini...cha kusikitisha wale vijana wanakula kuku kwa kwenda mbele uraiani.......so tusiwe blind tuwapongeze kwa sababu tu wamemuua jambazi na si kuokoa...hao wakikarabatiwa vyema kwenye mgao ndugu hata uite na ukunga hilo mpaka liishe ndio wanakuja.....majuzi walikuwepo majambazi pale kimara mwisho....ukiwa unapandisha kwenda bonyokwa...walipokuja gafla mmoja wa maaskari aliekuwepo pale wakinywa aliondoka ...wale waheshimiwa wakakaaa wakaigiza ulipofika muda wa kuwasambaratisha watu....kila mtu alilala chini ya meza akabaki kijana mmoja maskini huwa akilewaga anafanya kama wacheza kumfu...so walipomwambia lala chini akaanza kufanya hu ha ile anyooshe mikono wakapiga bastola kwenye kiganja.....akae vizuri wakampa ya utumbo...R.I.P TALL
  majirani wakatoataarifa kwa mapolisi..kituo cha polisi jamani kiko mita 15 toka sehemu ya tukio...wakauliza wamshaondoka au bado...wakaambiwa bado..kumbe ni sumu..wakaaa dk 30 wakaja wakamchukua yule jamaa walivyokuwa washenzi badala ya kumpeleka hospital watu wanawaomba jamanimpelekeni hosp wakenda chini walipoambiwa wamekimbilia huko....wakaaakaa zidi ya dk 25 wakarudi kufika hosp dk akasema amebleed sana sijui kama utamuwahi....akaishia kwa muumba..so ninachoweza kuwaambia hii michezo yote mapolisi wanajua..
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ni marufuku polisi kumpeleka mtu aliejeruhiwa kwa risasi hospitali ,aidha unatakiwa ummalize mkiwa ndani ya gari kuelekea kituoni au hospitali ndio mara nyingi unasikia amefariki alipokuwa akipelekwa kituono au hospitali.

  halafu jambo moja ambalo linanishangaza sana panapotokea mapigano ya risasi kati yapolisi na majambazi au inapotokea mtu kupigwa risasi ,huoni gari la wagonjwa ,maana mtu akiwa ana bleed halafu unampakia kwenye rover ,hiyo peke yake ni njia ya kummaliza kiurahisi ,na yote kwa sababu tunapopeleka mtu wa aina hiyo tunatakiwa kutoa ushahidi ambao si jambo dogo mara maguzo yanakuangukia ,hivyo tunauwa kazi na mapema ,nakumbuka nilipokuwa nikifanya kazi Arusha ,majambazi walikuwa haturudi nao wakiwa hai.

  Jambo moja la ajabu kwa nini katika vituo vya polisi hakuna ambulance karibuni dinia nzima polisi wanakuwa na ambulance zao ,sasa hapa kwetu ni mambo ya kimiujiza tu. Viongozi wetu wanasafiri wanaona lakini hawayasomi yale wanayoyaona huko wanakokwenda wanarudi hapa wakijikuna vichwa na kujichokora pua.
   
 5. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Taarifa rasmi katika tukio hilo mmoja ni mwanajeshi na kulikuwa na mwanamke
   
 6. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Na kama mlikuwa mmekosa kitoweo siku hiyo.. karoti(risasi) zenu zote zingeishia hapo. washukuru mungu walipata hilo wazo la kula kona.
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Jul 26, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hayo majambawazi hayakujuwa kuwa kuna komandoo mstaafu nini? Nahisi wana bahati sana kulala mbele... mzee mzima ungekumbushia za kule Arua, mbale, Mbarara na mtukula...!
   
 8. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Mkuu umemaliza kila kitu. Kila siku tunasema kuwa polisi wanajua kazi, na wanawafahamu mwajambazi karibu wote (isipokuwa vibaka). Nakumbuka kaka yangu mmoja aliibiwa Nissan Patrol moja mpya kabisa. Alikwenda polisi, kwa heshima mmoja akamwita pembeni akamuomba atoe shilingi milioni moja gari itakapatikana. Na kweli in three hours gari ikakamatwa ikiingia njia ya kwenda Arusha ikitokea bagamoyo, haijanyofolewa kitu. Mwizi alijulikana ni nani na wala hakukamatwa. Hiyo milioni moja waligawana watu watatu walifanikisha kazi hiyo kwa simu tu.

  Nina hakika polisi wakipewa mazingira mazuri na kama wakifanya kazi kwa moyo uhalifu utapungua sana.
   
 9. C

  Chief JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2009
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
   
 10. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Polisi Tanzania hawana jipya ishu kama hizo ndio wao wanaona dili na kutangaza kwenye vyombo vya habari wakati kuna mengi mabaya wanayofanyiwa raia wa Tanzania na hawayasemi wala kutangaza. Kikubwa hili jeshi ni la wenye pesa na CCM sie wengine tulie tuu!
   
Loading...