Jambazi aliyeua polisi auawa kwa ‘sangoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jambazi aliyeua polisi auawa kwa ‘sangoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Jan 14, 2012.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Jan 14, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  [TABLE="width: 99%, align: left"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody, align: left"]JAMBAZI sugu Pokea Kaaya `Steven Kaunda’ aliyekuwa anasakwa na Polisi kwa kumpiga risasi na kumwua askari kanzu na kumjeruhi kwa risasi begani Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Arusha (OC-CID), ameuawa kwa kupigwa risasi.

  Kaaya amefikwa na mauti hayo kwa kumiminiwa risasi na polisi baada ya kugundulika akiwa kwa mganga wa kienyeji akitibiwa majeraha.

  Kifo cha jambazi huyo ambaye Januari 3 alimuua Kijanda Mwandu (35) na kumjeruhi Faustin Mafwele wakati wa tukio la kurushiana risasi eneo la Shangalai wilayani Arumeru mkoani hapa, limethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye.

  Kamanda Andengenye alisema jana kwamba Kaaya aliuawa jana saa 12.45 alfajiri akiwa kwenye boma la Anna Roshilari katika kijiji cha Orarashi, kitongoji cha Lengine wilayani
  Arumeru.

  Alisema baada ya kupata taarifa za jambazi huyo kuwa eneo hilo, walituma kikosi cha kuhakikisha wanamtia mbaroni.

  Alisema: “Askari wangu walizunguka boma hilo usiku kucha na ilipofika saa 6.45 walimwona
  akichomoza ndani ya boma na kukimbia, askari wakamfukuza umbali wa kilometa mbili na ghafla akamgeukia askari namba E. 9912 Konstebo Wito na kumng’ata vidole ili aachie silaha
  aliyokuwanayo.”

  Andengenye aliendelea kusema, kwamba baada ya kumng’ata vidole, askari huyo aliachia silaha, jambazi akaichukua, lakini wakati akijiandaa kuitumia, askari wengine walimwahi kwa kumpiga risasi akaanguka chini na baada ya muda mfupi akafa.

  Alisema jambazi huyo alifika nyumbani kwa Anna Roshirali kutibiwa kwa mganga wa kienyeji jeraha alilokuwanalo.

  Aidha, jeshi hilo linaendelea kuwatafuta washirika wa karibu wa jambazi huyo, akiwamo Augustine Shine ‘Baba Mzungu’, mkazi wa Sakina Juu, mjini hapa.

  Pia kuhusiana na tukio hilo, watu wanne wanahusishwa na Kaaya ambao ni Agnes Silasi (40) ambaye ni mke wa marehemu aliyekamatwa eneo la tukio, Josephat Haule (33) mkazi wa Shangarai, Juma Masamaki ‘Twalibu’ (46) wa Ngarenaro na Daines Masawe (19) wa Nambala.

  Hata hivyo, polisi wanaendelea kuwashikiliwa watoto wa marehemu ambao ni Alex Parumina
  (13) na Daines Masawe (9), waliokamatwa siku ya tukio la mauaji ya Polisi Shangarai.

  Mwingine anayeshikiliwa ni Rehema Ally ambaye siku ya tukio alikamatwa na silaha akiwa
  ameificha chooni.

  Kamanda huyo alisema kabla ya jambazi huyo kuuawa, polisi wakishirikiana na wananchi, Januari 6 saa 4 asubuhi, eneo la Moshono, mtaa wa Letera, walipata silaha za jambazi huyo alizotumia kumwua polisi na kumjeruhi askari mwingine.

  Silaha hizo ni bunduki SMG namba 1016188011 yenye risasi 20 na magazini mbili na shotgun moja aina ya Model namba 88-12GA yenye risasi nne.

  Alisema silaha hizo zilikuwa zimehifadhiwa ndani ya mfuko wa sandarusi, huku juu yake
  umefunikwa jaketi jeusi, na kufichwa kichakani.

  Mwili wa mrehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, ambako kabla ya kuhifadhiwa katika majokofu, uliwekwa nje ya jengo hilo, kwa saa nane ili
  wananchi waushuhudie.

  Hata hivyo, habari kutoka kwa baadhi ya askari waliokuwa kwenye tukio la mauaji ya jambazi huyo ambao hata hivyo hawakutaka kutajwa majina yao, walisema wanachoamini uchawi upo, kwani walipomwona jambazi huyo kwa karibu kabla ya kukimbia, walifyatua risasi
  ikagoma.

  “Yaani nakwambia tulifanya kazi kubwa, kila tukikoki wapi, mpaka tukaanza kuomba ila
  nikakumbuka jinsi babu yangu alivyonifundisha, ikabidi niwaelekeze wenzangu ndipo chuma
  kikaachia, vinginevyo tungemalizwana huyu jamaa,” alisema mmoja wa askari hao.

  Aliongeza kuwa pia jambazi huyo wangemwua mapema lakini, kila walipokuwa wakipata taarifa ya mahali alipo na wao kufika eneo hilo, lakini huwa tayari ameondoka kwa pikipiki.

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Text, align: left"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Jan 14, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Angeua raia wa kawaida sidhani kama angetafutwa kwa nguvu kubwa namna hii.

  Anyway, hongera sana Kamanda Andengenye, hongera Makamanda kwa kazi nzuri
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  "Baada ya kung'ata vitole askari akaachia siraha,hata hvyo aliuawa wakati akijiaandaa kuitumia"

  Napata vitu vi2 hapo::
  1.Polisi wa Arusha ni Legelege sana,ni vipi ung'atwe vidole uachie silaha kirahisi tena kwa jambazi??? Mmh hapa andengenye una kazi kubwa sana kwa hawa askari wako

  2.Nahisi ni changa la macho hili kuweka hali ya hatari kwao na kuhipa nguvu hoja yao ya kumuua jambazi maana hapa wanasema wasingemuua wangeuliwa wao haaaaa,wangemkamata mzima angewaumbua sana
   
 4. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,934
  Trophy Points: 280
  Katika red nakuunga mkono. Majambazi sugu hakuna anayeletwa kituoni mzima maana wana mengi yakusema ambayo Polisi hawapendi wayaseme.
   
Loading...