Jambazi aliyetuibia TV mwaka 1988 nimemuona leo akiwa mzee

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
12,417
30,927
Kweli milima haikutani jambazi lililotuibia tv mwaka 1988 Raskazone Tanga nimeliona leo limezeeka linaishi kwa mtoto wake pale Mabibo jeshini linaumwa figo miguu imevimba balaa.

Kilichofanya nimtambue ni kovu lake juu ya jicho na huyo mwanae anaeishi nae japo wao wamenisahau.

Moyo unaniambia nimfwate mshkaji nimueleze kwamba ujambazi wa baba yako ulituletea umaskini kipindi tv za kwanza ndio zinaingia Tanzania.

Jamaa hawezi kunifanya lolote am now powerful than them I may do anything to them and leave unharmed.

Lengo nimlipie kisasi marehemu baba yangu.

Sitarajii kuwadhuru ila hata nikikumkumbusha huyu mzee uhalifu wake moyo wangu utaridhika.
 
Kinachoniuma ni baba yangu kashafariki halafu ndio namuona huyu mbwa.

Chukulia kawaida tu mkuu maana muda ushapita na huwezi jua yule wa jana na leo ni watu tofauti na ninaamini pia hata wewe kuna vitu ulivifanya kutokana na situations ama umri ambavyo nina uhakika huwezi kuvifanya leo. Chukulia ni ubinadamu tu na cha msingi zaidi hakuwadhuru au kutoa uhai wa mtu maana ingekuwa issue ingine.
 
Kamshauri aandike kitabu cha maisha yake ya ujambazi. Hasara na mikosi na ubaya wa uovu wake
Kule mbeya kwenu wakati kasusura anakamatwa pale Soweto 3 in 1 Mimi nilikuwa kwenye kiuchochoro kinachoelekea gereza la watoto liko hapo Soweto ile muvi ya kasusura niliiona nusu tokea hapo majizi na mawezi nimeyagawa sehemu mbili wenye akili Hawa huiba bank na wajinga hawa hutuibia sisi maskini wenzao kama hili zee la hapa mabibo. Ni jizi jinga.
 
Back
Top Bottom