‘Jambazi’ afa baada ya kuvuliwa hirizi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MTUHUMIWA wa ujambazi sugu ambaye amekuwa akisakwa kwa muda mrefu na Polisi mkoani Rukwa, amekufa ghafla baada ya kuvuliwa hirizi kubwa aliyokuwa ameivaa mkononi.

Akizungumzia mkasa huo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Isuto Mantage alisema mtuhumiwa huyo, Jelaz Mwananjela (44), alikamatwa na wananchi saa 11 juzi jioni pamoja na mwanawe, Galus Mwananjela (18) na kufikishwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Namanyere, wilayani Nkasi kwa mahojiano.

Baada ya kufikishwa kituoni hapo, Kamanda Mantage alisema, mtuhumiwa huyo alianza kulalamika kuwa wananchi walimnyang'anya hirizi yake aliyokuwa ameifunga kwenye mkono wake wa kushoto.

“Kwa mshangao wa wengi wetu, Mwananjela alianza kulalamika kuwa anaweza kufa wakati wowote kama hatarudishiwa hirizi yake na kweli muda mfupi baada ya kutoa kauli hiyo alipoteza fahamu,” alisema Kamanda Mantage.

Kwa mujibu wa Kamanda Mantage, Galus ambaye ni mtoto wa marehemu na pia anashikiliwa Polisi, alikiri kuwa baba yake alivaa hirizi hiyo kama kinga yake na ilikuwa inamsaidia asiumie wala kufa kama akipigwa katika matukio ya ujambazi.

Kamanda Mantage, alisema watuhumiwa hao walikamatwa na bunduki moja aina ya Shotgun yenye namba 065678 na risasi mbili, na walikuwa katika maandalizi ya kufanya unyang'anyi katika kijiji cha Ntalamila wilayani Nkasi.

Alisema, watuhumiwa hao walikamatwa baada ya wananchi wema kutoa taarifa za siri kuwa kuna watu wana silaha kijijini hapo, ndipo polisi, viongozi wa kijiji na wananchi wakashirikiana kuwakamata.

Mwananjela alikutwa pia na kisu kikubwa ambacho wananchi walikitumia kukata hirizi hiyo na kuichoma moto.

Kwa mujibu wa Kamanda Mantage, Gulus atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi wa awali kukamilika.
 
Siku zake zimefika akasubiri adhabu yake ahera!!!namuonea huruma mtoto wake maana sidhani kama ana future tena mzazi amemuharibu sana amemuacha sehemu ambayo ataijutia milele!!
 
Haya waandishi msingoje kuandika udaku tu, habari hizo za kutungia kitabu na kuingiza mifweza. Halafu hoo, mtaji hatuna, mitaji si hiyo.
 
Mada hii inapaswa kuangaliwa from the other side of the coin: isije ikawa marehemu amefariki kwa kipigo lakini wauaji wakadai amekufa bcos amenyanganywa hirizi. Pia tujue kuwa si kila mwenye siraha (hasa shortgun) ni jambazi. Kwa ufupi maelezo haja-justfy kuwa:
1. marehemu alikufa kwasababu kanyanganywa hirizi.
2. Marehemu+mwanaye walikuwa majambazi.
3. Kwa kuwa na shortgun+kisu kikubwa walikuwa wanaenda kufanya ujambazi.
 
Magazeti ya udaku ni kazi yao kuandika udaku, na magazeti mengine kwa watu makini yana andika habari makini, mfano raia mwema, mwanahalisi, kuhusu mitaji nina imani wana kopesheka bank
 
Ukiwa mfuatiliaji wa vituko vingi vinavyotokea Tanzania moja kwa moja utaamini pasi shaka kuwa ndio nchi pekee yenye technology ya hali ya juu sana duniani. Hebu ona vituko vifuatavyo.
1. Wakati wanasayansi wanahangaika duniani kupata dawa za kutibu Cancer, Ukwimwi na kisukari, Tanzania vinatibiwa kwa dozi moja ya kikombe cha dawa.
2. Kuna aina ya hirizi ambazo mtu akivaa hafi ...hata umpe kisago cha mbwa mwizi hafi mpaka aivue.
Ingekuwa na wananchi wa kawaida vijijini wenye hizi imani nisingeshangaa sana, lakini imani kama hizi "zinapokolezwa" na kuhalalishwa na vyombo vya dola/habari huwa nabaki mdomo wazi....
 
teheteheeeee hiyo hirizi ndo roho yake sio maskini weee
sasa dogo naye inabidi asake hirizi kama hiyohiyo imlinde
 
Back
Top Bottom