Jamaniee, ni namba gani ya kuongea na Huduma kwa Wateja wa Airtel?

Ghosryder

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
10,381
4,355
Hilo ndio swali langu yaani mtu unapiga simu customer care zaidi ya saa nzima unaongea na computer tu, na hupati maelekezo ya ubonyeze namba ipi kuonge na mtoa Huduma! Hivi inakuwaje nyie watu wa Airtel!??
 
Sijui uwa Wanakua wanapika Vitumbua uko ofisini kwao... Bora tu ufunge safari nenda Kesho kituo cha huduma au subiria usiku kuanzia saa 5 uwa wanapokea haraka kidogo...
 
Kuna namba ambayo ukipiga wanapokea haraka sana ila unakatwa hela.

Hilo ndio swali langu yaani mtu unapiga simu customer care zaidi ya saa nzima unaongea na computer tu, na hupati maelekezo ya ubonyeze namba ipi kuonge na mtoa Huduma! Hivi inakuwaje nyie watu wa Airtel!??
 
Airtel,tigo,voda,halotel wote ni wale wale ukipiga sim hawapokei sim

Ova
 
Unaweza kuwapigia bure kwa namba 100 kwa kutumia namba yako ya airtel au ukawapigia kwa namba 0784 105 400 au 078 4 104 800 kwa kutumia namba ya mtandao wowote japo kwa kupiga namba hizo mbili utalazimika kulipia muda wa maongezi.
 
huu ni upuuzi...ukipiga 100 unaishia kusikiliza maelezo ya computet tu...hamna hata namna ya kuzungumza na mhudumu...grrrrr
 
Back
Top Bottom