Jamani ya Loliondo yanatisha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani ya Loliondo yanatisha!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by hamidshaban, Mar 28, 2011.

 1. h

  hamidshaban JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  TBC jana imeonesha maiti zikiwa zimezagaa ovyo na nyingine vichakani! Foleni yenye urefu wa 50Km. Wastan wa w2 7 hufa kila siku
   
 2. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Nadhani Ungefanyika Utaratibu wa angalau wagonjwa mahututi wanaofika hapo wawe na 1st priority ili kunusuru ongezeko la vifo!!
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
  Ni kweli...maaana kuna wengine ni woga tu unawasumbua wala hawajapima kujua status zao. Ni LAZIMA sasa serikali ifanye wajibu wake.
   
 4. W

  WildCard JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Waliofanyiwa utaratibu maalum ni WANASIASA na VIONGOZI wetu tu. Tuwe wakweli tu, huduma ya mzee wa KKKT( Kunywa Kikombe Kimoja Tu) inahitajika kweli? Taifa limeingia mkenge. Tutatokaje? Usalama wa Taifa wanalionaje?
   
 5. GreedyKenyan

  GreedyKenyan Senior Member

  #5
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 136
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  You guys are so gullible!!! you actually believe that concoction works. Watu waende hospitali sio kutafuta madawa ya kienyeji.
   
 6. m

  msaragambo Senior Member

  #6
  Mar 28, 2011
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Watu wanawatoa wagonjwa mahutihuti hospitalini nanawapeleka loliondo,Sioni sababu ya kumlaumu mchungaji kwani alishaonya Kutokuwatoa wagonjwa Hospitalini

  Kwa hali ya kawaida kama mgonjwa ni mahututi halafu unampeleka kwenye mazingira magumu,hakuna chakula,hakuna sehemu ya kulala,hakuna maji kwa kifupi hakuna huduma muhimu ni kama unafanya advanture kwa hali hii ni lazima atakufa tu
   
 7. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Keep quiet, Dont call our govt leaders such a name!
   
 8. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #8
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,403
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  kama ni kweli basi hatua za haraka sana zichukuliwe.
   
 9. W

  WildCard JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Huyu mzee wa Loliondo atafutiwe mahala apumzike. Watakufa wengi.
   
 10. GreedyKenyan

  GreedyKenyan Senior Member

  #10
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 136
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  So let me get this straight, 52 people had died senselessly and you are busy defending the government? That's what makes the difference between kenya and tz. In kenya the pressure on the government from media, civil rights groups and general public would be so great someone would have to be fired especially the government administration in that particular area.
   
 11. I

  Inkognito Member

  #11
  Mar 28, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania tuache unafiki, hivi mnajua ni wagonjwa wangapi wanakufa kila siku mahospitalini kwa kukosa huduma za afya?taswira inayojionesha Loliondo kwa Babu ni mano tu wa namna watanzania walivyochoka kuteseka majumbani na mahospitalini kwa kukosa huduma bora za afya.
  Kama tunavyojua, tulizoea kuwasikia na kuwaona viongozi wetu wakikimbilia kutibiwa nje ya nchi jhata pale wanapoumwa mafua, wamesikia babu anatoa tiba bado wanaendelea kuziba nafasi za watanzania wenye matumaini ya kupona kupitia kikombe cha Miujiza kutoka Loliondo, huo nao ni aiana ya ubinafsi na uroho wa huduma,

  Kama kweli serikali ina nia thabiti ya kuwasaidia watanzania ni vema ingeboresha miundo mbinu ili watanzania waweze kumfikia babu kwa urahisi.
  Jana nilikuwa Loliondo katika kufanya utafiti, tatizo kubwa linalofanya wagonjwa kufariki wakiwa njiani kwenda kwa Babu ni miundombinu mibovu ya barabara kunakosababisha msongamano mkubwa wa foleni za magari.
  Katika utafiti wangu nimegundua kuwa Babu huudumia magari mia mbili kwa saa ambapo kwa siku nzima mpaka anapofunga huduma huudumia zaidi ya magari 3000.

  Katika hali ya kushangaza, pamoja na serikali kutambua uzito wa huduma inayotolewa na Babu kwa watanzania na mataifa ya nje lakini wameshindwa kuboresha hata huduma za choo kwa maelfu ya watu waliokusanyika Loliondo na badala yake wamekuwa wepesi wa kukusanya kodi kupitia ushuru wa magari ambapo gari moja hutozwa kiasi cha shilingi 2000 kila linapoingia.

  Loliondo hakuna huduma za kueleweka za chakula na malazi, watu wanajisaidia machakani, kuku mmoja anauzwa elfu thelathini za kitanzania, paja la mbuzi elfu ishirini na tano, maji madogo ya uhai yanauzwa elfu tanu, soda elfu moja na mia tano mpaka elfu mbili,kwa ujumla hali si shwari.

  Kimsingi, kuna haja ya serikali kuongeza jitihada zake katika kuboresha hali ya mazingira na huduma za kijamii Loliondo
   
 12. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  ukweli karibu utajulikana.

  mi naendelea na maombi ili roho hii ifunuliwe mapema, watanzania waijue ni roho gani iliyoleta huu ufunuo huko samunge

  utukufu ni wake Mungu
   
 13. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ni kweli watu wanakufa na watu hawasikii wanazidi kusafiri na kujaribu kwenda huko. Kwenda kule kwa kipindi hiki ni sawa na kuikabidhi roho yako kwa Lucifer. Kipindi cha mvua eneo lote la Lake Natron ni hatari sana. Mito hufurika tena sio kwa mvua zinyeshazo eneo hila ila hupokea mafuriko toka miinuko ya Ngorongoro. Mnaweza kuona Natron ni pakavu kabisa mara unaona mito imefurika! Hii sio barabara ya kutumainiwa kwa sasa kwenda Loliondo. Wanaambiwa wafuate utaratibu though gov yetu haijaweka utaratibu. Hatuihitaji elimu chuo kikuu kuweka utaratibu wa kwenda huko! The leaders have already gone there. They have seen the real situation! Wanasema wanakaa vikao and they of course sitting allowance! Serekali inaweza kuchukua hatua za dharura kwa kuweka kituo cha dharura kila mkoa na kuratibu wagonjwa wote wanaoenda Loliondo. Wakifika kujiandikisha watapewa tarehe na namba ya maalumu. Hizi namba na majina yatumwe Loliondo na tarehe wanazotegemewa kuweko kule. Kama huna namba na tarehe uliyopangiwa hupewi huduma!
  Tukianza kuratibu toka mjini tutaanza kuona watu wanapungua. Na hata huduma zitakuwa za haraka. Mbona KCMC wanatoa appointment na watu wanafuata! Inawezekana kabisa pia kudhibiti wageni toka nje ya nchi na tukawa na takwimu pia.
  Kwa mfano kwenda Loliondo kwa usalama lazima upite Ngorongoro then ukifika sehemu fulani maarufu Golini uaenda Loliondo then Digodigo halafu unaingia kwa Babu! ikilazimu sana utapitia Serenget to Cleins to Loliondo. Raia wa nchi ya kigeni atalipia entries kwa route zote hizi and with that our parks will earn some amount from Loliondo issue.
  Kule sasa ni vurugu! Kuna wasomali ambao wanatokea pande za Kenya. Idara ya uhamiaji wameweka kambi pale lakini hatusikii wakisema ni wangapi wamekiuka taratibu za nchi yetu. Kuna ndugu zetu Wakenya wamejenga mahema na vyoo vyao pale! Na raia wa nchi mbalimbali wako pale wanafanya biashara! Serikali inaendelea kusema tutatuma hiki mara kile lakini hakuna kinachofanyika.
  Tuanzie kuratibu kwa kupitia vituo vitakavyowekwa mjini na ikibidi watu wajulikane wanaenda kutibiwa nini! Sio kila mtu tu anaamua kujiendea!
   
 14. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Badilisha avatar yako kwanza ndo ufanye maombi
   
 15. Muro

  Muro Senior Member

  #15
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwanadamu kufa akitafuta tiba,vitani na mambo kama hayo hiyo ni amri ya mungu,kwani hata huko hospitalini bado wanaendelea kufa,kipi bora kufa ukiwa hospitali au ukiokoa uhai wako.Hata ukiwa mzima unaweza kufa tu kwa stroke n.k.tiba wanayoifuata ni ya kiimani zaidi. Serikali ya kijiji iweke utaratibu tu wa sehemu ya kuwazika maiti za watu waliokufa wakitafuta huduma ya babu hata mchango kidogo tu utolewe na wanaohitaji huduma ya babu
   
 16. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #16
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  ebo! acha porojo zako wewe,nenda kawazungumzie wakenya wenzako wa kule kibera.civil societies zipi?kwani kibera wanakufa watu wangapi kwa siku?
   
 17. Shakazulu

  Shakazulu JF-Expert Member

  #17
  Mar 28, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 940
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hah! hah! hah! Look who is talking. We Kenyans my *&s. The last time I checked Uhuru was still in office even though he have been accused of very serious crimes.
   
 18. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #18
  Mar 28, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,948
  Likes Received: 1,505
  Trophy Points: 280
  Naona mlipuko wa magonjwa hauko mbali hapo Semunge
   
 19. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #19
  Mar 28, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,931
  Trophy Points: 280
  Hivi KKKT wamefikia wapi kwenye ule utaratibu wao wa kuwapeleka wagonjwa wote waliolazwa KCMC kwenye hospitali ya rufaa ya Samunge?
   
 20. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #20
  Mar 28, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Hivi kati ya kwa 'babu' na muhimbili ni wapi kuna wagonjwa wengi? na watu wangapi wanafariki muhimbi kwa siku?
   
Loading...