Jamani, watawala jiepushe na umwagaji wa DAMU kisiasa, haulipii! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani, watawala jiepushe na umwagaji wa DAMU kisiasa, haulipii!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by theophilius, Apr 29, 2012.

 1. theophilius

  theophilius Senior Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa kadri taarifa zinavoendelea kujitokeza, inaelekea CCM na watawala, ama wanajihusisha au wanawalinda wanaojihusisha, aMA ndiyo wanaoendesha mauaji na umwagaji damu wa kisiasa, unaoendelea nchini, kwa sababu za ushindani wa kisiasa.

  Nashawishika kuamini hivyo kutokana na kutoona juhudi za maksudi (na hata za kisanii) za viongozi za kujitenganisha na uhalifu huu dhidi ya binadamu, kwa kulaani na kuhakikisha vyombo vya dola vinachukua hatua za kuridhisha ili haki itendeke na ionekane inatendeka.

  Matukio ninayazungumzia ambayo yananifikisha niifananishe CCM na MNRD ya marehemu Habyarimana wa Rwanda na wanamgambo wake wa Interahamwe, ni haya ya karibuni, miongoni mwa mengine yaliyo wazi na yanayotendeka kwa siri:

  1. Umwagazi damu wa wanachama (vijana wanne) wa chadema wilayani tarime siku chache kabla ya siku ya uchaguzi mdogo uliofanyika baada ya kifo cha 'ajali' ya Chacha Wangwe

  2.
  Umwagaji damu wakati wa uchaguzi mdogo wa Busanda Geita ambapo viongi wawili wa Chedema walikatwa mapanga katika kata ya Kamena ambao ni Basil Lema na Hemed Isabula

  3. Mwanachama wa Chadema aliyepotea/kuuwawa kwenye uchaguzi mdogo wa Igunga, kuwepo/kuonekana/ vitisho vya kundi la wanachama wa UVCCM ambao walikuwa na mapanga wakikimbiza wapinzani wao, tunaelezwa vilelezo na hata mapanga yalipelekwa Tume ya uchaguzi lakini hakuna hatua iliyochukuliwa.

  4. Umwagaji damu, siku moja kabla ya uchaguizi mdogo katika kata ya kirumba Mwanza ambao wabunge wawili wa Chadema walikatwa mapanga na wana-CCM mbele ya polisi, lakini hadi sasa hakuna hatua zilizochukuliwa badala yake polisi wanatisha wanajaribu kuhoji utendaji kazi wao.

  5. Mauaji ya arusha, wakati wa maandamano na mkutano wa amani na sasa mauaji ya mitaani ambapo watu wananyongwa na kuchinjwa kama kuku! ANGALIA PICHA HIZI HAPA

  Anayesema CCM na watawala hawahusiki, atueleze, waliohhusika na vitendo hivi wako wapi?, wamechukuliwa hatua gani! Hata kama kuna baadhi ya watuhumiwa walikamatwa, haitoshi kwa vyombo vya dola kukamata watu na kuwafikisha polisi au hata mahakamani, na kudhani wamemaliza jukumu lao.

  Ni juu yao kukusanya ushahidi unajitosheleza na kuhakikisha wauaji (attempt murderers) wanakamatwa na kuhukumiwa. Haiwezekani mtu anakatwa mapanga mbele ya kandamnasi, polisi wanasema hakuna ushahdi, ni kudhihilisha ukihiyo (unprofessionalism) kwa polisi na vyombo vingine vya dola, otherwise, kuna kundi (INTERAHAMWE) limeshatengenezwa na watawala (CCM = MNRD)kuwaua, wasiohitajika mpaka kuwamaliza, kama ilivyofanyika wakati wa utawala wa miaka 20 wa Habyarimana.

  Na kama hivi ndivyo , watu watakatwa shingo, watapigwa risasi, waandishi wataauawa kama alivyouwawa Masatu mwanza, watachinjwa na kukatwa kwa mashoka na ‘vifuni’ kama ilivyokuwa kabla na wakati wa mauaji ya Rwanda
  Ni vyema hata hivyo walio nyuma ya mpango huu wakajua, kwamba haki inapatikana hapa hapa duniani, vinginevyo wawaulize walioko ICTR Arusha, The Hague na kwingineko, ambako viongozi ambao leo wangekuwa wanacheza na wajukuu wao wakila pensheni kwa raha, wanasota katika vyumba vya mahakama na magereza kutokana na hujuma dhidi ya ki za binadamu zilizofanyika chini yao. WaMo Polisi, wanajeshi, viongozi serikali na wa vyama vya siasa, jumuhiza za vyama vya siasa na magenge na mashabiki wao.

  Kama hamhusiki, lazimisha vyombo vya dola vifanye kazi wanayolipwa kufanya, maana nyie ndiyo tuliowapa jukumu la kusimamia utekelezaji wa haki na utawala bora, uongozi wakulazimisha kwa kumwaga damu HAULIPI
   
 2. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kwakweli inabidi watubu na kuacha maaana wanalaanika sana kwa hizi damu za watu wanazomwaga. Wakumbuke kuwa, hizo damu hazitaenda bure
   
 3. j

  juni Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  viongozi chadema na wanaharakati, mnasubiri hali iwe mbaya kiasi gani! hakuna hatua mnazoweza kuchukua?
   
 4. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila ubaya utalipwa hapa hapa duniani nakuhakikishia waliohusika wote watalipwa uove wao kabla hawajafa tene kwa aibu kubwa,damu ya mtu humlilia Mungu ikidai haki daima!
   
 5. mchongameno

  mchongameno Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 6. theophilius

  theophilius Senior Member

  #6
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
 7. theophilius

  theophilius Senior Member

  #7
  May 2, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Na hizi zawadi ya mil. 10 wanayokuja nayo polis, ni changa la macho ni kutaka kuonesha mapema kwamba hawezi kuwakamata wauaji wa mwenyeketi Usa River
   
 8. j

  juni Member

  #8
  May 2, 2012
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  yetu macho
   
Loading...