Jamani washauri wa Kikwete wanalipwa na serikali?

Siao

Member
Jan 4, 2008
96
3
Nisaidieni tu, maana najiuliza wanashauri nini?

Ni akina nani hawa yawezekana wanakula kodi yetu hivihivi?

Nisameheni, nimeshapata jazba siwezi tena kuendelea?
 
Nisaidieni tu, maana najiuliza wanashauri nini?

Ni akina nani hawa yawezekana wanakula kodi yetu hivihivi?

Nisameheni, nimeshapata jazba siwezi tena kuendelea?

Mmoja wa washauri wa Kikwete ni fisadi, dikiteta, na muuaji ambaye ameingilia uchaguzi huru wa wanafunzi wa chuo kikuu kabla hajaleta FFU kupiga mabomu mwanamke mjamzito asiye na kosa lolote lile - Rwekaza Mukandala!

Analipwa indirect kwa kufuja mabilioni ya pesa za serikali yanayotolewa kwa uongozi wa chuo kikuu cha Dar es salaam
 
Nisaidieni tu, maana najiuliza wanashauri nini?

Ni akina nani hawa yawezekana wanakula kodi yetu hivihivi?

Nisameheni, nimeshapata jazba siwezi tena kuendelea?

Siao,

Kikawaida washauri hugawanyika sehemu mbili, wale waajiriwa na serikali, hawa huwa wanalipwa na serikali (sisi walipa kodi). Pia kuna washauri wengine kama akina Mwinyi, Kawawa, hata huyo Mukandala. Hawa huwa hawalipwi zaidi ya offers mbalimbali wanazoweza kama asante kwa ushauri wanaotoa.
 
Siku zote huwa nastaajabu jinsi Rais anavyochelewa ku-react kwa matukio mbalimbali hapa nchini.

Je,inakuwa hana majibu? Kama ni hivyo hao washauri wanafanya nini? Au ushauri wanaotoa ni kumwambia "mzee we kaa kimya yataisha with time"! Au JK hashauriki? Au anaona kila kitu kiko sawa nchini?

Matukio mbalimbali yamejitokeza nchini just to name a latest few of them-Richmond Development Plc, Zanzibar ni nchi au sio nchi? Tume ya uchaguzi, madai ya wafanyakazi, katiba, Dowans, mauaji ya waandamanaji wa CHADEMA Arusha,mauaji ya wananchi wanaodai haki ya malori yao kutumia barabara kama ya yule mwenye kituo cha mafuta Mbarali.

Hakuna kauli yake isipokuwa suala la katiba ambalo ameongea tofauti na matakwa ya wananchi. Anyway walau kaongea! Kukaa kwake kimya mara kwa mara kunaleta hisia kwamba hakuna kiongozi mkuu wa nchi. Yaani kuna ombwe la uongozi. Au nchi iko kwenye "autopilot"!

Nchini sasa kila waziri anaongea lake. Suala la Dowans-Ngeleja anasema nchi mekubali kulipa bilioni 94;Sitta anasema wametuzidi ujanja ila uamuzi utatolewa na baraza la mawaziri;Mwakyembe anasema hatuwezi kulipa wakati Mkulo anasema hakuna hela ya kulipa hata mpaka mwaka kesho kutwa labda Ngeleja atoe pesa kutoka kwenye bajeti ya Wizara yake!

Ukitazama nalo suala la katiba nalo utaona Kombani anasema hili na Werema lile. Ndio maana juzi Kombani pale ukumbini Nkrumah akasema eti "alikuwa anatingisha kibiriti akakuta kimejaa". Aibu tupu!

Maandamano ya Arusha ndio kituko kabisa! Wafuatao wameyaongelea hayo mauaji baadhi yao kwa ubabe:Membe,Wassira,Makamba,Mwema,Chagonja,OCD na RPC-Arusha kuwataja wachache tu.

Lakini yote haya ni ukosefu wa kauli ya rais pale hali inapokuwa tete kunakofanya kila waziri walau aseme akifikiri atakuwa ametatua jambo. Kumbe ndio ombwe lenyewe na kuparaganyika kwa Serikali! Hakuna official Gov't line siku hizi!

Mbona napata wasiwasi tutafika kweli huko tuendako?
 
Mkuu washauri wa Raisi ni
1 mwenyewe Raisi
2 makamba
3 salva-mwandishi wake wa habari
4 membe
5 mama
6watoto
7 ccm
7 ROSTAM AZIZ
8 MANJI
Unategemea nini HAPO:ban:
 
Nisaidieni tu, maana najiuliza wanashauri nini?

Ni akina nani hawa yawezekana wanakula kodi yetu hivihivi?

Nisameheni, nimeshapata jazba siwezi tena kuendelea?

Sielewi washauri general lakini wale wa karibu akina salma, januari, yusufu, ridhiwan na ngombale wapo kwenye payrol ya serikali. Wanalipwa kwa kazi nzuri ya kumshauri rais wetu kipenzi cha mafisadi. Mojawapo ya ushauri waliompatia ni 'kula bati' kwamba hata kelele zizidi vipi yeye asifunge kinywa chache mpaka zitapotea naturally.
 
Kuna haja ya kuwapima akili washauri wake na kuangalia afya zao.
Waangalie na milo wanayokula. Lol.
 
Mi hapa mtanisamehe lakini rais wetu hajatutendea haki kwenye swala la maisha bora na kukuza uchumi.
Marais wa nchi nyingine hua wakiona chini mwao hamna washauri wenye uwezo kiuchumi hua wananunua ma expert kutoka nje na kuwasaidia katika mambo mbalimbali kama vile hii dunia ya utandawazi ambayo formula ya uchumi ya mwaka 80's imebadilika sana kwa sasa.
Mkwere yeye kamleta kocha wa football na kumlipa mamilioni ya shilingi ambayo sidhani kama kuna hata mshauri wake mmoja anayelipwa hata nusu ya mshahara aliokua analipwa maximo. Hapa uchumi utakua wapi??

Mi nayasema haya kulingana na historia ya nchi zilizoendelea ambayo inaonyesha Britain ilikua ya kwanza ku industrialize kutokana na kua na wachumi maarufu na wanasayansi kama vile Adam Smith, David Ricardo, Thomas Malthus, John Stuart Mill, Alfred Marshal, John M. Keynes, Isac Newton, Charles Darwin etc. Huo ni mfano kwa britain only...ukifuatilia amerca is the samething..hakuna mshauri wa rais kwenye mambo ya nchi anayeajiriwa kisa eti ni ndugu au mjomba bila kuangalia uwezo wake.

Back to washauri wetu...well wanaweza kuchangia mambo kulingana na hali halisi ya uchumi wa nchi yetu lakini wengi ni walevi wa madaraka na hua hawasomi current issue na wala hawajui uchumi wa dunia kwa sasa unaelekea wapi!!
Phd holders mshauri wa rais ambaye hajawahi ku publish hata paper moja ya kiuchumi unatarajia wamshauri nini rais??
NO invention no clear advise!!

Presida ukiona mambo yamezidi unga unaruhusiwa kununua washauri kutoka nje wa maswala ya viwanda, uchumi, technolojia, power plant, and social welfare bila kuona aibu kama vile viongozi wa nchi nyingine wanavyofanya.
Hatutakaa tuendelee kwa kusubiria IMF, WB na WTO watengeneze policy then washauri wetu kazi yao ni kuangalia kama inafaa na ku recomend kwa rais!!....TUNAHITAJI WASHAURI WATAKAOTENGENEZA POLICY ZETU NDANI YA NCHI KULINGANA NA HALI HALISI, MAHITAJI NA MALENGO YA NCHI.
mwingine aendelee jamani iam tied with my own country.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom