Jamani wanawake kwanini wanakuwa waongo sana na kutokuwa waaminifu

donaldson don

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
624
415
Habari wanajukwaa, Naombeni msaada wa ushauri toka kwenu, mimi nimekuwa katika uhusiano wakimapenzi na msichana mmoja hivi kwa takiribani 3years ivi but na nimekuwa nikumhudumia kama mke ninae ishi nae.

Lakini mwisho wa siku akawa anaignore hata kumeet na mimi akidai yuko busy ilihali yuko kwa dadaake amelala mda kwavile yeye anaishi kwa dadaake anasingizia yuko busy chakushangaza kwenye mizunguko yake hasemi kama yuko busy kwa simu ananipigia sana pamoja nakutuma txt isipokuwa swala lakumeet tu ndo anapiga chenga.

Akija nyumbani kwangu yupo kwenye period anakuta nishapika tunakula story za hapa na pale then anaondoka but mwisho wa siku nimechoka kuhudumia bila namimi kuhudumiwa nikamwambia adai niendelee tu kuvumilia nikamwambia basi naomba uniambie kama unamwingine nijue kama wewe sio wangu niwapishe wenzangu na sitoweza tena kuendelea kuwasiliana nawewe wala kushirikiana kwa lolote.

Akawa anadhani maskhara mpaka now ninakata week sasa sijawasiliana nae japo yeye alinipigia simu ananiplz eti kwa usumbufu wakunipigia simu lakini pia wakuu nimeumia sana maana nimemhudumia mpaka dadaake anashangaa pamoja na kakaake akija nashida namsaidia mwezi wa tano alifiwa na babaake nikampa zaidi ya laki mbili kwenda kwao mwanza pamoja na kakaake.

Nashida ndogo za elfu 20,30,40,50,60,70 kibao hata hazihesabiki maana from 2013 adi sasa nikitambo kdogo sasa wakuu naombeni ushauri niachane nae nitafute mwingine au nijilazimishe kuwa nae japo yeye inaonesha kapata mwingine.. plz jamani nina areji na MATUSI ukiona sio ignore it.. samahani japo kwa ufupi maana ni historia ndefu
 
Pole sana kwa yaliyokukuta,lakini kijana mwenzangu ulipata wapi ujasiri (nani alikushauli) kuhudumia kiasi hicho ili hali hujamchunguza vya kutosha any way mapenzi upofu wanasemaga .

Ila hapo inaonekana wewe ndo umemelewa sana ila yeye bado hajaona:p:p:p:p:p....... kwa jinsi ulivo mfanyia hayo siyo malipo yake kabsa.

Pia kukataa kukuhudumia haimaanishi hakupendi kwani baadhi ya dini hamtakiwi mfanye hivo hadi muoane(siyajua dini zenu) ila kwa hali ya sikuhizi andika umeliwa tu.Ushauri wangu kama bado unampenda na una malengo naye maamuzi uliyoyachukua ya kukaa kimya ni sahihi yatakupa picha halisi alikuwa anakuchukuliaje ni vigumu yeye kuigiza kwa mda mrefu kama hakupendi kweli,vinginevo atakutafuta muongee tatzo nini ,akikaa kimya imekulaaaaaa.
 
Endelea kukaa kimya hata kama nafsi bado inataka ili kujua rangi yake halisi kwako ni ipi?

Ukiona kimya kwake pia chukua maamuzi magumu hata kama bado yuko kwenye mtima.

Note. Think more than twice before you say goodbye.
 
Habari wanajukwaa, Naombeni msaada wa ushauri toka kwenu, mimi nimekuwa katika uhusiano wakimapenzi na msichana mmoja hivi kwa takiribani 3years ivi but na nimekuwa nikumhudumia kama mke ninae ishi nae.. lakini mwisho wa siku akawa anaignore hata kumeet na mimi akidai yuko busy ilihali yuko kwa dadaake amelala mda kwavile yeye anaishi kwa dadaake anasingizia yuko busy chakushangaza kwene mizunguko yake hasemi kama yuko busy kwa simu ananipigia sana pamoja nakutuma txt isipokuwa swala lakumeet tu ndo anapiga chenga... akija nyumbani kwangu yupo kwene period anakuta nishapika tunakula story za hapa na pale then anaondoka but mwisho wa siku nimechoka kuhudumia bila namimi kuhudumiwa nikamwambia adai niendelee tu kuvumilia nikamwambia basi naomba uniambie kama unamwingine nijue kama wewe sio wangu niwapishe wenzangu na sitoweza tena kuendelea kuwasiliana nawewe wala kushirikiana kwa lolote.. akawa anadhani maskhara mpaka now ninakata week sasa sijawasiliana nae japo yeye alinipigia simu ananiplz eti kwa usumbufu wakunipigia simu lakini pia wakuu nimeumia sana maana nimemhudumia mpaka dadaake anashangaa pamoja na kakaake akija nashida namsaidia mwezi wa tano alifiwa na babaake nikampa zaidi ya laki mbili kwenda kwao mwanza pamoja na kakaake... nashida ndogo za elfu 20,30,40,50,60,70 kibao hata hazihesabiki maana from 2013 adi sasa nikitambo kdogo sasa wakuu naombeni ushauri niachane nae nitafute mwingine au nijilazimishe kuwa nae japo yeye inaonesha kapata mwingine.. plz jamani nina areji na MATUSI ukiona sio ignore it.. samahani japo kwa ufupi maana ni historia ndefu
Mmmh utakuwa na shida ya kumbukumbu Mkuu kwa vioja vyote hivyo bado unauliza uwe nae, mwanamke kama huyo Wa kuja kupikiwa na kula halafu anaondoka na vibomu juu.. ..
 
Ndo tabu ya kutosoma kemia. You have to balance equation, kama unampa nae akupe.

Hataki, mwambie asepe atakuharibia mizani yako ya mapenzi.
 
Duuuh yaan siku zote wale waaminifu na wakweli wanakutana na mabomu jaman tuoneeni huruma jaman tunajitunza kwa ajili yenu kumbe wengine mko na mpango wa kando kama humpend mtu siumweke wazi tu maisha yenyew mafupi, khaaaaa! !!
Pole Kaka kwa yaliyokukuta mtu unajicomit kwa mtu kumbe hata kichwan kwake haupo jaman kuwen na hofu ya MUNGU
 
Ngoja nikushauri kama baba yako mzazi
"Mwanangu donaldson don , maisha ya siku hizi ni tofauti na ya zamani, enzi zile za mimi na mama yako, ambapo hatukuwahi kugusana wala kufinyiana macho hadi siku tunaoana. Mama yako hakuwahi kuniomba senti ya sabuni wala doti ya khanga, tulikuwa tukionana pale tu mama yangu yaani bibi yako aliponiomba nimsindikize nyumbani kwa mama yake na mama yako yaani bibi mzaa mama yako, hapo ndipo tulipoonana, tukatabasamu tukajua tunapendana.

Lakini siku hizi kabla hujaoa, gharama unazotumia kuhudumia msichana ni zaidi ya mahari. Nakusihi mwanangu, kama hujawahi kukutana na msichana wa namna hiyo, muombe Mungu asikukutanishe nae, ila kama unae, hutoweza kumbadilisha, achana nae.

Mpenzi hatafutwi, hivyo nawe usitafute. Mpenzi hujitokeza katika mazingira yoyote yale, ofisini, njiani, daladala, basi, supermarket, bank, hospital n.k Ukikutana nae, kuwa mchangamfu, jiamini, omba namba, anzisha mawasiliano ya urafiki, mchunguze tabia, mwanamke anaekupenda kwa dhati hakuombi hela ng'o, shida zake atapeleka kwa wazazi, ndugu na marafiki zake, ukiridhika na mengi, mtoe out siku moja na umwambie nafikiria kukuoa, unaonaje nikiwa baba wa watoto wako?

Atashtuka najua, lakini atakubali, piga goti na umvalishe pete ya uchumba.Kesho yake Unijulishe baba yako ili tuandaae safari ya kuja huko mjini kuleta posa ya mkeo mtarajiwa. Siku ya harusi nitavaa ile suti uliyoninunulia Norway, nitapendezaaa, hahahaaa na Mama yako atavaa lile gauni lake la kuwakawaka.
Kila la kheri mwanangu.
 
chaaa kwahiyo unasubiri kutamkiwa?? mtu kama hakutaki ni hakutaki tu hata kama unamuhudumia. ningekushauri usepe kuliko kuendelea kuumia na kujipotezea muda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom