Jamani wananwake wengine tabu Tupu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani wananwake wengine tabu Tupu.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Akili Unazo!, Jul 16, 2009.

 1. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,790
  Likes Received: 2,452
  Trophy Points: 280
  Nina rafiki yangu tunafanya naye kazi;hivi karibu amebahatika kupata mtoto na mke wake wa ndoa lakini kwa kuwa wapo tu wawili na house girl ikabidi washauriane kuwa kwa kipindi chote cha siku arobaini aende kwao mpaka hapo atakapo malizi hiyo arobaini.

  Kwa kipindi chote hicho amekuwa akienda kumwona mtoto na mama yake huku akimchukua kumpeleka hospital kwa ajili ya kumaattend kwa kuwa alijifungua kwa operation.

  Kilichomshangaza na kinachomuuma huya ndugu ni kwamba baada ya arobain kuisha na yeye kuwa amesharicover kidonda chake alimwambia kuwa inabidi arudi nyumbani ili mtoto apazowe kabla ya kuanza kazi (maternity leave).Cha kushangaza jama alijibiwa kuwa walikubaliana na mama yake kuwa akae tena wiki nzima ndo aende.

  baada ya jama kuambiwa hivyo ikabidi amuulize swali nani unatakiwa kukubaliana naye juu ya uamuzi wa kuendelea kukaa huko mimi mumeo au mama yako?Mwanamke hakujibu.

  Siku mbili baada ya arobaini huku hako kamgogoro baridi kakiendelea kutotatuliwa jama alifanya tu surprize ya kwenda kumwona mtoto kama kawaida cha ajabu hakumkuta mkewe pale nyumbani na mtoto kamuachia housegirl wa mama yake na alipouliza alijibiwa kuwa amekwenda sokoni ambao pana umbali kama km 50 hivi.jama alipojaribu kumpigia simu simu yake ikawa haipatikani.

  Muda wa saa kumi hivi akapiga simu ikawa inaita jama akamuuliza ukuwa wapi muda wote huo jama akajibiwa kuwa alienda sokono kutafuta nguo za mtoto na zake.Hapo ndo mgogoro ukawa umewaka.jama akamuuliza kwa nini ulikuwa umezima simu?na kwanini hukuniambia kuwa unasafari ya kwenda huko?jama hakupata jibu.
  Mpaka hivi ninavyoongea mwanamke huyo anasema yeye haoni kama alifanya kosa na haombi msamaha.

  Wakuu naomba msaada huyu jamaa amefikia sehemu japo ni mapema mno kuanza kuwa na wasiwasi na uhalali wa yeye kuitwa baba wa mtoto huyo kwani anaona hapewi heshima kama baba na mume wa mtu.

  Cha ajabu kikubwa jama akamuuliza kama huoni umefanya kosa ulipomshikisha mam yako juu ya hili alikwambia kuwa siyo kosa,mke akamjibu kuwa alikaa kimya hakujibu kitu.
  Hivi hapo jamaa yupo right kwa kureact hivyo au???
  Au alichokifanya mkewe ni sawa?

  jamani mpeni ushauri huyu ndugu maake mhhhhhhh kumbe hata wanawake nao tumooo!!!!!!!
   
 2. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Mi naona huyo mke kafanya kosa...kwa sababu, kiutaratibu alitakiwa amsikilize mume wake kwanza, na pengine amwambia ni kwa nini ni MUHIMU kubaki huko kwa mama yeka kwa wiki moja zaidi.

  Kujichukuliz uamuzi tu bila kumwambia mumewe ni kumdharau na kutompa heshima stahili,


  Na akazidi kutia chumvi kwenye kidonda kwa kuondoka 50Km kwenda 'sokoni'...anazidi kujenga mazingiza ya KUTOAMINIWA na mumewe na hasa panapokuwa na sababu zisizo na msingi ni kwa nini afanye hivyo tena bila kumuaga mumewe.

  Huyo jamaa ana haki ya kudemand maelezo kutoka kwa mkewe, lakini pia kiutaratibu wasije kutengana mtoto ado mdogo. Kama ana wasi wasi na mtoto basi siku hizi tuna mashine za DNA...anaeza kwenda kupima kama ikiwepo sababu ya lazima

  Pole sana jamaa 'angu
   
 3. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Mkuu,

  hapo nilibo-bold/blue ulimaanisha mtoto sio?
   
 4. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,790
  Likes Received: 2,452
  Trophy Points: 280
  Sorry mkuu ni mtoto
   
 5. B

  Bint Member

  #5
  Jul 16, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani tangu mwanzo hawana mawasiliano mazuri. Sio jambo la ajabu mama akaomba kukaa na mwanae wiki zaidi tena ambapo amejifungua kwa operation. Ila huyo mke alitakiwa amueleze mumewe mapema na wakubaliane.
  Swala la kwenda sokoni mi naona huyo mume ame-react sana, simu yaweza kuzima kwa kuishiwa charge bila wewe kujua kama charge imebaki kidogo hasa pale unapokuwa unamhudumia mtoto mdogo.
  Tatizo watu tunapenda sana kufikiria to the extreme pale tu unapoona simu ya mtu haipatikani au ameenda mahali bila kukutaarifu, sioni kama kuna sababu ya kutomuamini mkeo kiasi hicho
  Ni hayo tu
   
 6. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,790
  Likes Received: 2,452
  Trophy Points: 280
  sababu aliyoitoa kwa jama ni kwamba anahisi kuwa nyumba kwake yaani kwa mumewe kuna uchafu yaani vumbi jingi kwa hiyo anasubiria jumamosi ili aje na wadogo zake waje msaidie kufanya usafi eti mtoto anaweza kuugua mafua.

  baada ya kusikia hivyo jamaa akamwambia hivi toak mwanzo nilikuwa mchafu au ulinikuta mchafu hapo ndo kazidi kumuudhi kabisa.na kuhusu suala la DNA alligusia baada ya kukosa maelezo ya kutosha yule mkewe akasema hata kesho nenda.
   
 7. B

  Bint Member

  #7
  Jul 16, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona hata mimi nilipojifungua ilibidi mume wangu na mdogo wake wafanye usafi nyumba nzima kila mahali ilikuondoa vumbi? Mtoto wa kwanza ana mambo mengi wandugu. Mwambie huyo jamaa yako kama kweli anampenda mkewe wakae chini waongee bila kushutumiana wamlee mtoto wao waache malumbano na mtoto anawahitaji
   
 8. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,790
  Likes Received: 2,452
  Trophy Points: 280
  Yaani jama na huyo mke wake wanamaelewano ya hali ya juu kilichokuja kumudhi nikule kutomshirikisha suala ambalo linawahusu wawili tu na kulazimisha kuwa mume akubaliane na maamuzi waliofikia yeye na mama yake bila hata kumsikiliza yeye ambaye ndo ana dhama kubwa la kuwalea na kuwatunza yeye na mtoto waliompata kwenye ndo takatifu.
   
 9. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280

  Hili nalo linahusu.


  Hapo ndo tatizo lilipo Binti,

  Kumbuka, ameamua kuongeza wiki bila sababu, ana operation, anaenda sokoni kilomita hamsini, mumewe hana habari, na simu haipatikani!

  sualando linaanzia hapo, kwa nini.....unajua maumivu ya kichwa huanza pole pole..sina nia ya kusema kuwa jamaa amepitiliza au vipi lakini ana haki ya kujua, si ndo na nyie mnapenda pia kujua tumeenda wapi? kama mawasiliano mazuri, kazi yake ni nini kama sio kuambiana kuwa naenda wapi, nk?
   
 10. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Chaku, nadhani ni suala la kukaa chini hao wawili wayaongee. Kama mawasiliano yakiwa mazuri nadhani hakuna tatizo

  nina wasi wasi huyo mke wake baada ya kujifungua, amekumbwa na yale mabadiliko ya kuwa mzazi, kulea mtoto nk na anaona mambo mengine hayana umuhimu. Ni vizuri asiingie kwenye huo mtego,, mtoto ni muhimu ila akumbuke siku zote mtoto wake wa kwanza ni Mumewe:)
   
 11. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #11
  Jul 16, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Inawezekana ni ulimbukeni wangu ila nijuavyo mie ni kuwa maamuzi kama hayo (ya ndoa) ni kati ya mume na mke! Tusiruhusu mama au baba akuamulie kwa sababu hata wao wana ndoa yao. Unless kuwe na sababu muhimu ambayo mume anaonekana kutoielewa ni vema akaeleweshwa ila mume ndie mwenye maamuzi hasa linapokuja suala la mkewe na mtoto!
   
 12. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  makosa yalitendeka tokea mwanzo, siwezi kuamini kwamba house girl na mke wa rafiki yako hawawezi kumuangalia mtoto
  hakukuwa na sababu yeyote ya msingi mke kwenda kukaa kwa mama yake wakati kuna house girl ndani ya nyumba
  watu wanakuja kazini wanatoa story za mtoto anavyolia usiku na experience ya siku za mwanzo za mtoto lakini huyo jamaa yako hajui kitu (hana hiyo experience ya mtoto ya siku za mwanzo) ni makosa hayo siku ingine mtoto akizaliwa akae nae
   
 13. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,790
  Likes Received: 2,452
  Trophy Points: 280
  Ok mkuu kwa ushauri wako.lakini huoni kuwa anachotaka sasa ni kumrudisha nyumbani ili aexperience hizo za kulia kwa mtoto usiku?lakini anakumbana na kipingamizi hicho mpaka anaogopa nini kulikoni mama mkwe kuingile mahusiano ya wawili badala ya kumruhusu arudi kwake tena siyo kwenye nymba ya kupanga yake.au ndo maadili ya kitchen party? Ndo maana kuna kipindi niliulizia umuhimu wa kitchen party ni baada ya huyu jamaa kuniambia majibu aliyoambiwa na mkewe kutoka kwa mama mkwee
   
 14. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Na hili nadhani mkuu ni angalizo la maana kabisa

  najua kuna wenzetu wana utamaduni eti mke akafikia kujifungua 'anaenda kujifungulia kwao'...binafsi kama ni mke na mume, sioni sababu ya hili....mmeapa kuishi kwa kusaidiana shida na raha, sasa hii kwenda kumtwika mzigo mama mkwe ya nini?
   
 15. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,790
  Likes Received: 2,452
  Trophy Points: 280
  Sasa mkuu hili linauhusioano gani na swali la msingi au hujaelewa?jamaa anataka arudi nyumabi yeye anakata eti mpaka wiki iishe makubaliano yalikuwa baada ya arobaini kuisha arudi kwake siyo intervention kwenye maamuzi.

  hapo mkuu napingana na wewe kabisaaaaaaaaaa.

  Kwa kuwa hakuna kilichopelekea haya mambo mengine kuvumbuka ndo aondoke kusikojulikana na kuzima simu?
   
 16. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Chaku, kama sijaelewa utanisamehe...mi nazungumzia context ya issue nzima hadi kufikia hapo, nikitilia maanani alichosema Semilong hapo juu.

  Kwa nini walikubaliana toka mwanzo kwenda kuishi kwao kwa siku arobaini ? kwa nini asingeenda nyumbani moja kwa moja? huoni kuwa kwa kwenda kwake kwa mama yake,, ndio chanzo mcha kuhisiana vibaya? angekuwa nyumbani na mumewe, hayo yote yangetoka wapi?

  Ndio maana nikahoji mantiki nzima ya mke kwenda kujifungulia nyumbani kwao badala ya kwake anakokaa na mumewe.

  Karibu, kupingana constructively huleta raha ya mjadala.
   
 17. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...siri ya mtungi, ukiona moshi unafuka ujue kuna moto chini yake...huyo mwanamke haiwezekani kazuka tu katika kipindi cha arobaini kufanya vitimbi hivyo.

  Huenda bwana mkubwa huyo tayari alishamtenda sana huyo mkewe kipindi fulani cha ujauzito kiasi kwamba mke kaamua kumtia jamaa adabu...

  Mshauri jamaa atulie tu, "what goes around comes around", kipindi alipokuwa naye hajulikani alipokwenda, mara anazima simu, mara simu inaita haijibiwi mkewe alikuwa mashakani hivyoi hivyo, ...avumilie tu!

  Mwisho, siku akizaliwa mtoto mwingine ni marufuku kumpeleka Mkewe kwao! Kama hawezi kumlea mkewe na mtoto, amuagize ma mkwe aje hapo nyumbani.
   
 18. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  This is perfect! Kumrudisha mwanamke nyumbani ni kukwepa majukumu na ndio maana mama mkwe anapata nguvu ya kuingilia maamuzi (si mnakaa kwake!).
   
 19. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,790
  Likes Received: 2,452
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli anakazi ya kufanya kama yupo quilty kwa hilo sijui anyaway nashuku kwa ushauri wote na michango yenu nitmueleza niliyoyapata yeye aamuwe cha kufanya.
  Lakini kwa hilo smu bado nina utata nalo kwa kuwa kabla hata jama hajampeleka huko walikuwa wote hospitalini kwa muda wa wiki tatu.akiendelea na uchunguzi wa maendeleo ya mtoto.

  jama hakutegemea wiki tatu tena za kukaa kwao kungefika hatua ya kumpa kiburi mama mkwe kuanza kuingilia mahusiano yao.na kwa mantiki hiyo inaweza fika sehemu mama mkwe akamwambia leo usimpe of which kwangu naona nikutofuata maadili waliyopewa kanisani na kwenye kitchen party enzi hizo.

  Pia jama hakumleta mama yake kwa kuwa yupo mbali pia alikuwa afya yake haikuwa nzuri kihivyo ndo maana ikabidi ampeleke huko kwa kipindi hicho cha muda mfupi.
  Mbaya zaiadi matumizi yote anampelekea nyumbani kulekule kwao sasa sioni umuhimu wa mama mkwe kuingia mahusiano yao.

  Yote hayo nashukuru kwa niaba yake kwa michango mizuri mlioitoa kwa kweli hata mimi nimejifunza kitu hapa inabidi niwe makini.
   
 20. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #20
  Jul 17, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...jambo mojawapo la kujifariji 'akumbuke' mama mtoto hajapona sawa sawa, kwahiyo wala asiwe na wasiwasi kuwa labda 'atasaidiwa' huko nje!

  Huenda hilo pia linamfanyisha mama mkwe kuwa makini na hao wazazi, wasije 'wakamkunja samaki' angali mbichi. Mwacheni bibie apumzishe kidonda kwanza... :)
   
Loading...