Jamani wanaJf nisaidieni hili kutoka TRA na BANK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani wanaJf nisaidieni hili kutoka TRA na BANK

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mike 1234, Apr 10, 2010.

 1. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kunatabia imezuka katika hizo taasisi hapo juu tunapo tuma wake zetu kufuatilia masuala labda kulipia kodi au kuomba mkopo kutoka bank,inapotokea mke wako akapangiwa ofisa mikopo mwanaume au ofisa wa kodi mwanaume basi imekuwa ni kero ya ajabu kwa hawa watumishi kuwatongoza wake za watu!mfano mke wangu alikuwa anafuatilia TIN number yake mwenge TRA pamoja na kuwa ameshaipata TIN number jamaa bado anampigia simu za kumtaka pamoja na kumweleza kuwa ameolewa lkn jamaa hasikii,hivyo hivyo katika Bank moja hapo Makumbusho pamoja na kuwa mkopo ameshapata lakini yule ofisa mikopo bado anamsumbua kwa kumtaka kimapenzi, huyu yeye ananijua kwa sura na wakati wa kukagua vitu vya ndani alinikuta nyumbani na nikaweka saini katika zile form za uzamini kama mume,naongea haya kwa uchungu kwa sababu huyo wa bank jana kampigia simu anamuomba wakutane maana wkend hii free,Sasa nauliza wanaJf nifanye nini kukomesha hili? naomba kuwasilisha hoja
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  kaka pole sana hata mimi linanikuta daily. wife wangu anachukua mkopo nmb magomeni mwaka wa tano sasa kuna kiafisa mkopo kimoja kilimtongoza, akaja kuniambia jamaa ananifahamu, wife wake ananifahamu na mie namfahamu hata wife wangu anajuana na wife wa huyo afisa mkopo, wife akanieleza tulichofanya jamaa akimpigia simu tukutane kiti moto sehemu flani, basi tunaenda wote jamaa akifika anatukuta, akamtumia wife sms eti ndo umefanya nini sasa wife akamtishia namforwadia mr hii sms, jamaa wacha aombe msamaha, hakukoma, siku ya kumsainisha form akampigia simu tena wakutane kitimoto maeneo flani pale sinza, wife akanishtua nikamwambia mtumie mke wa jamaa mwaliko aje kwenye kitimoto. ikawa km picha huwezi amini jamaa kaja mpaka pale kamkuta wife akaagiza bia wife anakunywa soda, jamaa km kawaida akaanza upuuzi wake, wife akanitext nikajoin pale jamaa akashtuka kwa vile ananijua dah akapagawa akaanza story nyingi, wife akachomekea nipe form niweke sahihi, jamaa hakubisha akazitoa akajidai eti kesho sitakwepo kwa ofisi ndo maana kazileta usiku anadhani mie sijui. form zimesainiwa tu, wife akamtext mke wa jamaa aje fasta kitimoto tayari, lahaulaa mke wa jamaa kumbe aliambiwa na mmewe yupo class, alipomkuta pale akamuuliza baba nani hii hapa ndo darasani? jamaa kimyaa, mwanamke mstaarabu hakuleta fujo pale, ila waliporudi nyumbani kwao jamaa alibanwa sawasawa akakoma kuleta upuuzi, juzi hapa wife kenda pale nmb magomeni kakutana naye, jamaa anamwambia wife siku hizi nakuchukia kisa eti kamchoresha kwangu na kwa wife wake. so mkuu tafuta means ukutane naye ana kwa ana akiwa kamfuata wife wako halafu mpige mkwara sawasawa ataacha.
   
 3. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,807
  Likes Received: 1,975
  Trophy Points: 280
  Naomba nikuambie jambo moja kwa kifupi kama unaamini huyo mkeo umepewa na MUNGU kwa imani yako whatever, husiumize kichwa hata kidogo kwani hapa ndio wakati wa kuijenga au kuibomoa ndoa yako. Najua kama mwanamume inauma kwani una uhakika kama mkeo anakuzuga tu kuonyesha kuwa anakerwa na matongozo hayo kutoka kwa wanaume hao.
  Manake ukitaka kuumiza kichwa ndio utaanza kufikiria kuwa hao ni baadhi tu ambao mkeo amejaaliwa kukuambia ila kuna wengine amewaweka kapuni.

  So relax mwanaume mwenzangu na umpe MUNGU majukumu ya kuilinda ndoa yako isisalitiwe. Sali sana kwa imani yako na haya majaribu ni ya kitambo tu yatapita
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu, unawafahamu kiundani wanawake? Nakuhakikishia ukimsikia mwanamke anakusimulia kuwa fulani ananitongoza, basi ujue kuwa alishamkubali na alishampa vitu. Kama anakuja kwako kulalamika kuwa bwana mikopo au bwana kodi anamsumbua, basi ujue hiyo ni gia ya kujikinga usije kushtuka kwa sababu anajua simu zao zitakuwa nyingi kwa sababu ameshaanzisha uhusiano nao
   
 5. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  .........Hii kitu ipo sana katika jamii baadhi ya wanaume mwenye ndoa yake kutongoza mwanamke na anajua ana ndoa yake.Yaani sijui hata huwa wanafikiria nini wanaume wa jinsi hii, anajua kabisa kwamba umeolewa tena anaona hadi pete ya ndoa na uchumba zimeganda kidoleni lakini bado anamtaka mke wa mtu na wakati ana mkewe.

  Hapo ndugu akili ni kichwani kwa mke wako, sisi wanawake tunatongozwa sana na wanaume japo tumeolewa lakini inabidi kuwa na msimamo kama mwanamke unayejali, unajiheshimu na kuwa na hofu ya Mungu kutoka nje ya ndoa.Hivyo katika swala hili ni msimamo tu wa mke wako kujua kusema no na akimaanisha ni no kweli.
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Si kweli! Nasema si kweli! ebu tupe sababu kwa nini unataka tuamini mawazo yako mpita njia?
  Ninalodhani limefanya utoe mawazo haya ni kwa kuwa uenda mkeo aliwahi kuku victimize siyo?
  Basi kama ilikutokea wewe usiwafanye wanawake wote ni sawa. Wapo waaminifu 100% na wako wasio waaminifu kabisa. Pia wapo wanaume waaminifu 100% na wako wale ambao uaminifu wao ni 0%.
  Mimi nilisha acha kufuatilia habari za wale wanaotongoza mke wangu ambao ni wengi tu maana ni pretty woman, na hata mimi wako wanawake wananitongoza wala simwambii mke wangu. Nimeamua kuilinda heshima yangu, ndoa yangu na kumpa Mungu utukufu. Full stop.
   
 7. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,807
  Likes Received: 1,975
  Trophy Points: 280
  Maafisa Mikopo bana, vichefuchefu kweli

  Kwahiyo mawife wetu daily wanatongozwa halafu na nyumbani kama mume unamzingua fasta tu anapandisha nguo na mkopo husio na riba unapatikana! Damn shit! Tuwapende sana wake zetu ili wakikutana na mafedhuli wase.. hawa wakumbuke upendo wa home.
   
 8. M

  MJM JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Sawa umenena kama mchungaji, lakini jamaa katushirikisha tuone tabia chafu na ya kishenzi ya hawa wanaijiona wa maana kuliko wanaume wote duniani. Kwani mara ngapi watu hutongoza wasichana na kuwadanganya wako TRA au Bank? Ushenzi wanaofanya kwa wanawake wanaozuzuka wanauendeleza. Kwani kuna nini mpaka utumie kazi kumbuka uliomba kazi kwa ajili ya kuganga njaa na siyo kuitumia kwa manufaa ya uasherati. Shame on them
   
 9. M

  MJM JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Good trap! Achana na hao wanaodai ndiyo wanawake wako hivyo sijui anakuzuga na nini haya mambo lazima u take action. By the way generalization katika suala la tabia siyo sahihi. Hivi ukidharau baada ya kuambiwa jamaa ananisumbua mkeo atakuonane kwamba umehalalisha au. Tuache ushabiki wanaume wasumbufu wapo tena hawajali mke wa mtu au street vendor
   
 10. L

  Lufu lwa ndama New Member

  #10
  May 4, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana ndugu yangu. Unafahamu vijana wa siku hizi hata maadili hawana.Enzi zile wafanyakazi wa benki waliaminika sana na jamii inayowazunguka lakini sasa mabenki yamegeuka mapango ya wahuni(hasa hawa vijana wanaodeal na loans). Unaweza kunipatia namba yako nijue namna ya kukusaidia?
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yaaani wajukuu zangu mnanifurahisha sana ....yaani kama mkeo anakuja na kukuambie eti fulani ananitongoza ujue kishampakata....kwangu mimi ningempa talaka straight away..kama ananiambia waliomtongoza mbona anaowakubalia na kuwapa utamu haji kuniambia???
   
 12. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Siku hizi hata WACHUNGAJI wanatongoza
   
 13. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Wanawake wakisikia mtu yuko benki anajishaua shaua . Ni matatizo kweli kweli.Wanadhani hao jamaa wanazo za uhakika kumbe wapi.
   
 14. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Pole sana ndugu.

  Lakini pia hongera kwa kuwa na mke ambaye 'wengine' pia wanamkubali (Joke:bounce:!)

  Mimi naona kuna ishu tatu hapo. Moja ni mtoa huduma kutumia privileded information (namba ya simu) ya mteja kwa manufaa binafsi. Hili linaweza kushughulkikiwa na ofisi husika kwa kupeleka malalamiko/ushahidi rasmi kwa mkurugenzi/mkuu wa taasisi husika. Pili ni je mtoa huduma ameweka ngono kama pre condition yeye kutoa huduma? Kama ni yes, then hili pia linaweza kushughulikiwa na taasisi na hata kipolisi/mahakamani.

  Ishu ya tatu, kama hayo mawili hayapo ni kwa mkeo kujifunza namna nzuri na effective ya kusema NO. Kwa maoni yangu wanawake wengi hata walioolewa inawawia vigumu sana kusema NO kwa maneno, vitendo na hata sura, mara nyingi wanaishia kutoa visababu kama hiyo ulioyoitaja (eti 'nimeolewa' au 'mimi mke wa mtu') huku sura zao hazioneshi kama kweli wanasema NO. Sababu kama hizi haziwezi kumzuia mwanaume mkware kuendelea kumfuatilia. Mwanamke anapoto sababu eti ameolewa, mwanaume anachofanya ni kujaribu kumshawishi kuwa mumewe hatajua hayo mahusiano (akifanikiwa hapa, tayari mwanamke hana tena ujanja!).

  Mimi binafsi sitarajii kujipa kazi ya kuanza kumsaidia mke wangu kusema No kila anapotongozwa. Nategemea yeye mwenye awe responsible and bold enough kusema NO ambayo anaiamini na anaweza kuisimamia. Otherwise utaumiza kichwa chako bure kwani watongozaji hawaishi kamwe.
   
 15. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #15
  May 4, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,495
  Likes Received: 1,052
  Trophy Points: 280
  Kamwone Shigongo amuwekee mtego,......ndiyo kazi yake hiyo kuumbua watu, tena akimpata kwenye anga zake (Shigongo)anakulipa na vihela kwa taarifa hizo...
  Pole sana........watu nao kwa kujaribujaribu.....kuwa makini, wakijaribu kama ishirini kuna uwezejano mmoja au wawili wakapata..so mpunguzie nafasi za kujaribiwa.
   
 16. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,495
  Likes Received: 1,052
  Trophy Points: 280
  Kamwone Shigongo amuwekee mtego,......ndiyo kazi yake hiyo kuumbua watu, tena akimpata kwenye anga zake (Shigongo)anakulipa na vihela kwa taarifa hizo...
  Pole sana........watu nao kwa kujaribujaribu.....kuwa makini, wakijaribu kama ishirini kuna uwezejano mmoja au wawili wakapata..so mpunguzie nafasi za kujaribiwa.
   
 17. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #17
  May 4, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kaka uwe makini saana !
   
 18. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #18
  May 5, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  muue
   
Loading...