Jamani WanaJF! Hili la CHANDARUA kukaa miaka 5 bila ya kuwekwa dawa

Nilikuwa naangalia BBC, wikiLeaks Director "Julian Assange" alikuwa akieleza HUKU AKILIA , jinsi wamarekani walivo polute MTO " RIVER" ambao unatumiwa ku destibute maji eneo moja kule Iraq wali polute kwa sumu mto ule na watu wakanywa , kilichotokea hiroshima ndio kinachotokea huko! watoto wanazaliwa vilema dah! siwezi kuendelea nataka kulia!
 
Itaisha vp Mkubwa? Ina maana hauonei huruma Watanzania wenzetu? Jamani kazi kweli kweli!

Huruma nawaonea sasa maana hata mimi ni mtanzania. Shida ninayoona hapa ni kwamba kwa kadiri watu wanavyojadili, ndivyo wanavyo divert kutoka kwenye kufikia hitimisho na suluhu ya jambo hili.

Wengi wanatoa tu lawama tu na kuonesha wasi wasi juu ya matumizi ya net hizi. Lakini hawatoi njia mbadala ya kutumia ili kudhibiti malaria. Nadhani sasa tuache kulalama ila watu watoe mawazo yao juu ya njia mbadala ambayo haitakuwa na madhara kwa jamii na mazingira.
 
Njia mbadala ni kuhakikisha ndoo za maji sehemu ambazo maji hayatoki zinafunikwa zote, yaani kujaribu kuondoa sehemu ambazo kuna mazalia ya mbu, ikiwezekana waweke mafuta ili mayai yasiweze kutotolewa ! Tanzania bila Malaria inawezekana mbona India wameweza hiyo kwa silimia fulani ?!
 
Asili ya marekani ni hawa "Red Indians" ..sasa soma kisa cha chini hapo

How Red Indians disappeared in America ? ( I need very serious ansers please)?

  • 5 years ago
by xxxxxMember since:May 09, 2006Total points:21,438 (Level 6)
Best Answer - Chosen by Asker

There are several reasons that the native Americans are not as prevalent as they used to be:

1. 470 something treaties that our government made with the tribes and broke.

2. Disease infected blankets were intentionally traded to the native Americans to kill them off.

3. When we traded arms to the native Americans, we only gave them guns with no rifling in the barrels making the weapons very inaccurate.

4. We forced marched the tribes across the country along what is now called the trail of tears in which almost every elderly and most youth did not survive.

5. When a few of the tribes finally got fed up with this treatment and started fighting back we slaughtered them.

This was every bit as much of an act of genocide as Nazi Germany committed. We just committed the genocide, slowly over a long period of time.

Sasa hivi vyandarua tutapona kweli? kweli mtu ambae ana weza kufikiri kwa kina, chandura kinakaa kwa miaka mitano hakitiwi dawa na mbu akigusa tu anakufa je yule anaelalia inakuwa vipi pale,

Juzi nimesoma kwenye gazeti wa asia wa Mwanza wanagoma kupeleka watoto wao kwenye chanjo ya polio! serikali imesema itawatia ndani ! tunashangaa sana enzi zetu sisi chanjo ukimaliza basi lakini leo kila wakati chanjo mtu unajiuliza ni chanjo au ?? tumeshuhudia jinsi watoto wa Libya ambao hawna hatia yeyote wakidungwa sindano za kuambukizwa virusi jamani tuwe makini na hii misaada ! Mungu ibariki Tanzania Mungu vibariki vizazi vetu Amin.

Mimi nadhani hilo wazo la waasia kukwepa chanjo si la kujivunia.

Kabla ya kuwaza hivyo ungefikiria kwanza magojwa yaliyowahi kuwepo na sasa hayapo ambayo yalitokomezwa kutokana na chanjo kama hii ya polio. Na hivi sasa kuna harakati za kuitokomeza polio, je tuache kuchanja watoto wetu? Inawezekana labda ni uongo hakuna kitu kinaitwa polio? Mbona tuna hofu hata ktk mambo ya msingi kabisa jamani.

Mkuu najua wewe ni mtaalam naomba unihakikishie yafuatayo:
1. Usalama wa nguo za mituma zinazotoka ulaya ambazo tunavaa kila siku bila kuhoji.
2. Usalama wa dawa za binadamu zinazotoka ulaya tunazotumia hospitalini kila siku- nyingine tunanunua kwa bei ghali sana.
3. Vyakula na vinywaji vinavyotoka ulaya tunavyonunua kila siku supermarkets.

Inawezekana hivyo hapo havina madhara ndio maana hatuhoji. Kama dawa inaweza kuwekwa kwenye net, inashindikana vipi kuwekwa katika nguo za mitumba? Kulikuwa na haja gani kuingia gharama ya kutengeneza net mpya badala ya kuweka ktk nguo used na kuzisafirisha huku kwa gharama ndogo tu? Inawezenanaje kutumia AK47 badala ya kutumia mtego wa panya uliozoeleka kuuwa panya?! Mbona tunakwepa mambo mengine? Tuhoji na hili.

Hapo kwenye kijani mimi nina shaka kwa sabaubu sio mpango wa mungu wazazi kukataa watoto wao kupata tiba. Siamini kama mungu anapenda mtu aumwe akae tu bila kutafuta tiba. Hata kama ni kuomba uponyaji, lazima uoneshe interest kama kweli unahitaji huo uponyaji. Sioni logic ya kumhusisha mungu katika mambo ambayo mengine tunajitakia tu wenyewe.
 
Njia mbadala ni kuhakikisha ndoo za maji sehemu ambazo maji hayatoki zinafunikwa zote, yaani kujaribu kuondoa sehemu ambazo kuna mazalia ya mbu, ikiwezekana waweke mafuta ili mayai yasiweze kutotolewa ! Tanzania bila Malaria inawezekana mbona India wameweza hiyo kwa silimia fulani ?!

mkuu sasa kinachotushinda kutumia hizi njia mbadalia ni nini? Maana sote tumezaliwa tukakuta ujumbe kama huu, na mpaka leo tunaendelea na ujumbe huu hadi kwa wajukuu zetu, na kibaya zaidi, tatizo ndio limezidi hata zaidi ya zamani. Siku hizi kuna mbu kila mahali. Hata maeneo ambayo zamani hakukuwa na mbu, siku hizi wapo wa kutosha tu.

Naona umegusia mafuta, sina hakika kama mafuta haya yanatoka hapa kwetu. Vipi, yenyewe hawawezi kutia kitu, maana naona hawa wazungu wamedhamiria kutumaliza kabisa?! Jaribu nja ambazo asili yake haina mkono wa mzungu.
 
Mimi nadhani hilo wazo la waasia kukwepa chanjo si la kujivunia.

Kabla ya kuwaza hivyo ungefikiria kwanza magojwa yaliyowahi kuwepo na sasa hayapo ambayo yalitokomezwa kutokana na chanjo kama hii ya polio. Na hivi sasa kuna harakati za kuitokomeza polio, je tuache kuchanja watoto wetu? Inawezekana labda ni uongo hakuna kitu kinaitwa polio? Mbona tuna hofu hata ktk mambo ya msingi kabisa jamani.

Mkuu najua wewe ni mtaalam naomba unihakikishie yafuatayo:
1. Usalama wa nguo za mituma zinazotoka ulaya ambazo tunavaa kila siku bila kuhoji.
2. Usalama wa dawa za binadamu zinazotoka ulaya tunazotumia hospitalini kila siku- nyingine tunanunua kwa bei ghali sana.
3. Vyakula na vinywaji vinavyotoka ulaya tunavyonunua kila siku supermarkets.

Inawezekana hivyo hapo havina madhara ndio maana hatuhoji. Kama dawa inaweza kuwekwa kwenye net, inashindikana vipi kuwekwa katika nguo za mitumba? Kulikuwa na haja gani kuingia gharama ya kutengeneza net mpya badala ya kuweka ktk nguo used na kuzisafirisha huku kwa gharama ndogo tu? Inawezenanaje kutumia AK47 badala ya kutumia mtego wa panya uliozoeleka kuuwa panya?! Mbona tunakwepa mambo mengine? Tuhoji na hili.

Hapo kwenye kijani mimi nina shaka kwa sabaubu sio mpango wa mungu wazazi kukataa watoto wao kupata tiba. Siamini kama mungu anapenda mtu aumwe akae tu bila kutafuta tiba. Hata kama ni kuomba uponyaji, lazima uoneshe interest kama kweli unahitaji huo uponyaji. Sioni logic ya kumhusisha mungu katika mambo ambayo mengine tunajitakia tu wenyewe.

Watu kamwe hawakatai kupata tiba, kinachotisha ni hawa wenzetu mambo wanayoyafanya katika za wenzetu, kuna usemi usemao "ukiona mwenzio ananyolewa na wewe tia maji " .

Binafsi sipingi kinga wala dawa yeyote, lakini sisi tulipozaliwa tulikuwa tukipewa chanjo wakati tupo wadogo na baada ya hapo hakuna kilichoendelea labda kama kuna mlipuko wa maradhi umetokea.

Hivi mkuu wangu nikuulize, huoni kama CANCER ni nyingi sana sasa hivi ukilinganisha na miaka ya nyuma??? unajua kwanini? hivo vyakula unavoviongelea ndio sababu kubwa ya maradhi hayo,! watu wameacha kula vyakula vya asili na kibaya zaidi hata hicho chakula cha asili nacho kinatiwa mbolea za kila aina ili kinone!

Hivi umeshatembelea ward za watoto wanaougua cancer pale Muhimbili? nenda kaangalie! umeshapata habari ya maziwa ya china yalokuwa yanatiwa "melamine" unga mfano wa maziwa, je unejua kemikali ambazo zinatiwa katika vyakula siku hizi?..nenda tembelea MUHIMBILI KAONE WATOTO WANAVONYOFOLEWA MAFIGO !! aisee inatisha wewe!

hakuna anaepinga chanjo tatizo watu tumeingia wasiwasi kutokana na masimulizi yaliyopita na jinsi historia ya hawa wenzetu inavosema. wana mazuri na mabaya yao!

Nikuulize, zamani ulikuwa ukitibiwa na Chloroquine, sasa hivi unaambiwa haitibu na madawa ya kila aina yameanzshwa sidhani kama ni kwa imani bali NI KIBIASHARA ZAIDI! ...

Kama wao wana imani sana ya kutuletea chandarua , kwanini wasitumie pesa hizo KUTUTAFUTIA CHANJO AMBAYO MTU AKICHOMWA itakuwa ni once and for all .. na Malaria hupati tena kama walivofanya kwenye hayo mambo mengine.

Hapa Ndugu yangu sikuungi mkono! hali inatisha ! some trend ya cancer inavokuwa siku hadi siku ....naendela kusema MUNGU IBARIKI TANZANIA .. NA VIZAZI VETU! ndugu zetu wa "Ifakara Heath Institute" wanajipinda kutafuta chanjo ya MAlari ipo Siku Mwenye Ez Mungu atafunua na itapatikana kwani kwa imani yetu ya kiislamu tunasema hakuna ugonjwa usio na dawa ..ipo siku ...
 
mkuu sasa kinachotushinda kutumia hizi njia mbadalia ni nini? Maana sote tumezaliwa tukakuta ujumbe kama huu, na mpaka leo tunaendelea na ujumbe huu hadi kwa wajukuu zetu, na kibaya zaidi, tatizo ndio limezidi hata zaidi ya zamani. Siku hizi kuna mbu kila mahali. Hata maeneo ambayo zamani hakukuwa na mbu, siku hizi wapo wa kutosha tu.

Naona umegusia mafuta, sina hakika kama mafuta haya yanatoka hapa kwetu. Vipi, yenyewe hawawezi kutia kitu, maana naona hawa wazungu wamedhamiria kutumaliza kabisa?! Jaribu nja ambazo asili yake haina mkono wa mzungu.

Ndugu yangu kama ulisoma Tanzania, sayansi kimu, kuna wakati tulifundishwa jinsi ya kuondoa masalia ya Mbu, na moja wapo ni kumwagia mafuta katika mabwawa yaliyo karibu na makazi ili kuua mazalia ya mbu, iwe mafuta ya uto, karanga, alizeti hata ya wanyama kama ngo'mbe, nina imani kubwa mafuta yote haya yanatengenezwa hapa hapa nchini ,au mkuu wangu haupo Tanzania? kinachotakiwa ni serikali kujikita zaidi kutoa elimu kama zamani tulikuwa tunasikia "MBIU YA MGAMBO IKILIA INA JAMBO" kule vijijini, tena kizuri kabisa siku hizi kuna vipaza sauti ambavyo vinaweza kutumika vema tu . mtaa mpaka mtaa! wakuu wa serikali za Mtaa wawezeshwe ili wahamasishe wakazi wa eneo lao kufanya hima kuua mazalio ya Mbu! imma kwa kufukia mashimo yanayoweka maji, kuzibua mifereji yote inayoweka maji na kuweka mafuta hayo nilokutajia ili kuzuia mayai kupata "Oxygen" na kwisha kufa kabisa.. Narudia "Tanzania Bila Malari inawezekana" kama kauli mbiu hii itafanyiwa kazi kikamilifu MTAA KWA MTAA basi sidhani kama tutahitaji vyandarua vya bush!
 
Mh. Mkomatembo, nimekuelewa.
Naamini umeanzia mwanzo wa thread hii, nilionyesha hofu ya kuhusishwa na mradi huu. Ila kinachonisukuma kuendelea kujadili hii mada ni hoja za wachangiaji. Kimsingi mimi sina tatizo na wasiwasi wetu juu ya hivi vyandarua, ila kinachonitia shaka ni kwamba watu wengi wanaangalia zaidi hivi vyandarua pasipokukubali kwamba kuna mianya mingi inayoweza kutumiwa na hawa jamaa kutuhujumu. Na ambayo kimsingi kama wana lengo hilo, walishaanza zamani na pengine watakuwa wameishafanikiwa. Sijawahi kusikia watu(+you) wakihoji wala kujadili kuhusu nguo za mitumba na vitu vingine vya aina hiyo.

Umesema lisemwalo lipo kama halipo......, tatizo hapa ni namna watu wanavyolisema. Kwa mfano, maziwa ya China yalileta madhara tukaona-hakuna anayepinaga.Unaweza kusema madhara yanaweza kuwa imediate au late consequences, sikatai ila unapokuja na hoja kwamba chandarua kina dawa ya kupunguza nguvu za kiume ndipo naona kuna ukakasi. Ukifuatilia mchango ya watu mbalimbali humu utakuta kila mtu anatoa sababu zake; huyu atasema vyandarua vina matobo makubwa havifai, huyu anasema vina dawa ya kupunguza nguvu za kiume, mwingine yeye akiamka yuko hoi. Je, ndugu mkomatembo wewe unagundua nini hapo? Je, lisemwalo lipo.... ndio hilo? Kwa haraka haraka unapata jibu kwamba watu wanapinaga matumizi ya hivi vyandarua kwa sababu nyepesi tu.

Binafsi mimi si muumini wa misaada ya wazungu.Sio kwamba ninaamini kuwa hivi vyandarua ndiyo suluhu ya tatizo la malaria, ila kama kitu kinaonekana kusaidia sina sababu ya kuweka vikwazo tena bila sababu yoyote yenye mashiko. Kwa mfano,kama njia nyingine ambazo ni salama zimeshindikana kwanini nisitumie hizi neti. Je, nilale tu bila net kwa sababu tu watu wanasema tena bila udhibitisho. Ni mangapi yamesemwa ya uongo? So, nife na malaria? Hapana, nitakuwa wa mwisho kuedesha maisha yangu kwa kufuata maneno ya watu ambayo hayana udhibitisho wowote zaidi ya lisemwalo lipo...

Kimsingi nakubaliana na wewe juu ya mbinu chafu wanazotumia wazungu kutawala. Pia nakubaliana na wewe kwamba kuna madhara mengi yanayotokana na vyakula vinavyotoka ulaya. Naongeza hapa pia kwamba ni imani yangu kuwa wazungu si jamaa zetu. Ila napingana na wewe kwenye kuhamasisha jamii iache kutumia vyandarua bila sababu yoyote ya msingi huku tukiacha kujadili njia nyigine ambazo zinaweza (na pengine zimeishatumika) kutuhujumu, mfano nguo za mitumba, vipodozi, dawa za kawaida za hospitali nk.
 
Hizo chandarua ukilala uwa zinauma usoni na kenye ngozi iwapo zitakugusa. maumivu yake inakuwa kama upo makambako hizi zake au umeingia frijini.
 
Hizo chandarua ukilala uwa zinauma usoni na kenye ngozi iwapo zitakugusa. maumivu yake inakuwa kama upo makambako hizi zake au umeingia frijini.

Ni kama sijakuelewa vile. Hebu fafanua kidogo.
 
Back
Top Bottom