Jamani WanaJF! Hili la CHANDARUA kukaa miaka 5 bila ya kuwekwa dawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani WanaJF! Hili la CHANDARUA kukaa miaka 5 bila ya kuwekwa dawa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by LiverpoolFC, Dec 13, 2011.

 1. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #1
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Ndg zanguni hebu tuliangalie hili kwa undani kwa anayejua na atujuze wenzake ambao haituingii hata kidogo. Chandalua kukaa miaka 5 bila ya kuwekwa dawa yeyote inakuja jamani? Mi inanitia shaka sana!
   
 2. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Kuna mengi yanayotokea kwenye sayansi na teknolojia ambayo ni kama viini macho, lakini ukweli ni kuwa 'ni sayansi tu'! Ndio sawa na chandarua chenye dawa inayoweza kududmu miaka mi5.

  Hapo awali wakati teknolojia ya vyandarua vyenye dawa inaanza, ilikuwa ni chandarua cha kawaida kinachovwa kwenye dawa (Ngao ya kidonge au maji)..hii ilikuwa rahisi kwa dawa kutoka wakati wa kukifua.

  Lakini sasa dawa inakuwa kwenye zile fibers zenyewe za kutengenezea chandarua, yaani dawa inakuwa incoporated humo wakati wanatengeneza hivzo fiber, then fibers zinaletwa Tanzania Arusha pale A-Z wanatengeneza vyandarua. Kwa sababu dawa iko ndani ya fibers zenyewe, basi haitoki kwa kufua, na ndio maana dawa inaweza dumu kwa miaka hiyo mi5!
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkubwa! Ngoja wadau waje kwn bado sijaridhia wazo lako.
   
 4. mysteryman

  mysteryman JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nini miaka mitano mbona vipo mpaka yakudumu....afu kwanza ukitumia hayo mavyandarua hakyanani ukiamka asubuhi upo hoi kama umekunywa dawa za malaria....hiyo dawa ni kali sana mpaka mtu unalewa na kuchoka....,
   
 5. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,027
  Likes Received: 3,220
  Trophy Points: 280
  Afu inawezekanaje kusiwe na madhara (side effect) wakati hata aspirini inamadhara?
   
 6. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,251
  Trophy Points: 280
  Wanpunguza watu katika bara la afrika!wewe jiulize miaka5 unadawa unalala humu unavuta hewa je wewe kwa kipindi hicho utakuwa umeathirika vipi??pili jiulize water guard kifuniko kimoja kwa galoni 10 za lita 20 watu wakaona inakuwaje??wakajaribu kufulia nguo kama Jik dah majibu waliyoyakuta wakakuta jik original ndo feki maana water guard inangalisha mpaka basi hata kuwepo na Doa sugu kwa waterguard lazima litoke!!Sasa jiulize ukinywa wewe utakuwa mgeni wa nani??mimi nilipiga marufuku kwangu mimi nikuziba njia za mbu na kuchemsha maji basi!!
   
 7. n

  najua JF-Expert Member

  #7
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kwanza dawa yenyewe haifanyi kazi daily nakuta mbu wazima wapo ndani ya chandarua na hakina hata mwaka tangu serikali wagawe
   
 8. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #8
  Dec 13, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hii issue ya vyandarua kiukweli kila mtu ana lake. Ila waliowengi wanavipinga kwa hoja nyepesi nyepesi tu. Sayansi ni uwanja mpana kila mtu anacheza sehemu yake na mwisho wa siku anaondoka bila kuumaliza. Huwezi kuifikiria sayansi kwa upeo mdogo kiasi hicho.

  Binafsi kinachonikera ni pale unakuta mtu mzima kashupalia jambo fulani, tena jambo lenyewe hata yeye mwenyewe halijui na hataki hata kujishughulisha kidogo kujua ukweli wake. Kwa mfano, kuna watu wanaamini kuwa hivi vyandarua vimewekwa dawa maalumu ya kupunguza nguvu za kiume. Lakini ukiwauliza wadhibitishe, wanabaki wametoa macho. Kuna mswahili mmoja humu ndani(JF) aliombwa kufanya utafiti ili kujua dawa yenyewe na pengine kuona kama side effects zinaweza kusababisha kupunguza nguvu za kiume. Jibu alilotoa ni kwamba hata internet (google) ni ya wazungu so hata yenyewe itadanganya!

  Historia inaonyesha kuwa magonjwa mengi yalianza kwa kuuwa watu wengi kabla tiba na chanjo kupatikana. Hata Wareno walishindwa kutawala Africa Mashariki kutokana na vifo vingi vya wanajeshi wao vilitokana na malaria. Siku hizi kuna magonjwa mengi yametoweka duniani kutokana na chanjo na tiba ambazo kwa kiasi kikubwa(if not all) zimetengenezwa na wazungu! Sasa hivi kuna kampeni kubwa ya kutokomeza ugojwa wa polio duniani. Na kwa kiasi kikubwa kuna mafanikio isipokuwa sehemu chache tu ambapo bado ugonjwa huu upo. Kwa Africa ni Nigeria ambapo ugonjwa huu bado upo kwa sababu kuna jamii fulani ilikataa watoto wao wasichanjwe eti kwa madai kwamba ni jama za wazungu wanataka kutokomeza jamii hiyo(hii ni issue ya kidini)

  Binafi mimi napenda watu wanaokataa kitu fulani kwa hoja zinazoeleweka. Hivi tunatambua kuwa malaria ndio ugonjwa unaouwa watu wengi zaidi magonjwa yote? Hivi tunafahamu watoto wangapi wanakufa kila baada ya saa moja kutokana na malaria? Naamini kama tungekuwa tunayajua haya asingepatikana mtu anyepinaga hapa tena kwa hoja nyepesi kiasi hiki.

  Lakini pia kwa wale wanaopinga mpango huu wa vyandarua vyenye dawa wabekuja basi na njia mbadala. Watuambie basi nini tutumie badala ya hivi vyandarua. Je, tutumie nia gani ya kuuwa/kuzuia kuumwa na mbu. Dawa kuulia mazalio ya mbu kama vile DDT nyingi zina madhara ya kimazingira(ingawa nazo pia zimetengenezwa na wazungu). Au basi tuwe tunasubiri hadi tuumwe ndio tutibiwe, lakini hizi dawa zenyewe tunaziamini vipi kama nazo hazijawekwa dawa ya kutuzuia kuzaa? Ni vingapi vinatoka ulaya nasi tunatumia bila kuhoji? Lakini pia hiyo dawa inakaa tu kwenye vyandarua haiwezi kuwekwa kwenye mitumba ya nguo tunayovaa kila siku? Hivi mbona hii ni hisabati rahisi tu, kwa nini watu hatutaki kufukiria? Mbona sioni watu wakipinga uvaaji wa nguo za mitumba? Wanaiamini vipi?

  Kwa wale tuliofiwa na wapendwa wetu kutokana na malaria tunajua machungu yake. Hoja sio vyandarua vya Bush au vinavyotengeneza arusha. Hoja ni namna gani tujikinge na malaria. Hizo hoja za mtu kuamka asubuhi yuko hoi kama aliyetumia dawa za malaria hazina msingi kwani, dawa za kuua mbu ni tofauti na zile zinazotumika kutibu malaria. Hapa mi naona watu wanakimbia vivuli vyao. Ukiamka asubuhi kama hujisikii vizuri jaribu kuonana na daktari akusaidie, usi condem chandarua.

  Kiukweli kama tutaendelea kuwa na watu wenye mawazo ya namna hii, kuitokomeza malaria itakuwa ni ndoto. Mimi naamini hata kama hao wazungu wana lengo la kurudi Afrika sio lazima kupuguza idadi yatu. Kwani wanarudi kufuata nini ambacho hawawezi kupata kutoka Afika ambacho hawawezi kukipata hata sasa hivi? Kwani wanashidwa vipi kuja kununua eneo lote la Afrika kwa bei ndogo tu. Kma ni madini wanamiliki wao, kama ni wanyama wanakuja wanawachukuwa wazima wanaondoka nao, kama ni mifumo ya uchumi wanamiliki wao, kama ni soka la marapurapu(bidhaa) yao wanauza Afika, yani kila kitu! Sasa sisi hapa tunabishana nini?

  Tufike mahali jamani tuwe serious. Malaria inatuuwa sisi, wenye nguvu wanatibiwa India.

  Tafakari.
   
 9. Ahmad Mussa

  Ahmad Mussa Member

  #9
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Chandaru balaa hizi, yaani mpaka inzi anapenya!
   
 10. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #10
  Dec 13, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,532
  Likes Received: 1,020
  Trophy Points: 280
  Inawezekana mkuu kama ulivyoelezwa na RIWA hapo juu we huoni
  matangazo ya Dawa za nguvu za kiume yanavyoongezeka maana lisemwalo
  lipo watu wanasema ile Dawa inaharibu OFISI yaani inafika hadi IKULU..........
   
 11. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #11
  Dec 13, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu vipi wewe unasemaje?
   
 12. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #12
  Dec 13, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Lakini hapa kwetu vipo vyenye quality nzuri unaweza ukatumia. Lakini kwa wale wasiokuwa na uwezo ni vema wakaendelea kutumia hivyo hivyo kuliko kuacha kabisa.
   
 13. Nyaluhusa87

  Nyaluhusa87 JF-Expert Member

  #13
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 1,288
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Mrimi,naomba uniambie madhara ya mazingira yanayosababishwa na DDT?
   
 14. Ahmad Mussa

  Ahmad Mussa Member

  #14
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Si vema mkuu hivi unajua balaa la mbu wakiingia ndani ya neti?
  Ukiamka asubuhi wanakuwa wakubwa kama Inzi halafu hawawezi
  kuruka ukiwagusa tu wanapasuka na kutoa damu yaani balaa!
   
 15. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #15
  Dec 13, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,532
  Likes Received: 1,020
  Trophy Points: 280
  Ninafahamu kuwa inaharibu kwa kuwa ni sumu lakini sinjui
  kama inaharibu ikulu. Sijawahi kutumia na sijawahi kupata tatizo
  kwenye ofisi yangu. Ngoja nitumie nihakikishe, yaani kutaste sumu
  kwa kuilamba.
   
 16. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #16
  Dec 13, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Nimeishaanza kupata wasiwasi maana si muda mrefu nitaambiwa na mimi nina fungu kwenye mradi huu!

  Mkuu mazingira ni pamoja na viumbe hai wengine wasio mbu. Hawa ni viumbe ambao wengine wana faida kwa binadamu.
  Kwa kawaida DDT ni nonselective inapokuwa imetumika inaua kila kitu. Lakini ukumbuke nimetoa mfano mmoja tu wa dawa ila zipo nyingi tu. Na mbaya zaidi zinadumu ktk mazingira kwa muda mrefu na ndivyo madhara yake yanavyodumu pia.

  Nimejitahidi kujibu swali lako boss. Na wewe naomba unijibu maswali yangu hayau haya hapa.

  1. Unazungumziaje nguo za mitumba tunazovaa kila siku kama vile underwear na socks?
  2. Vipi kuhusu dawa nyingi zinazotengenezwa na wazungu ambazo tunatumia kila siku?
   
 17. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #17
  Dec 13, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Unaonaje kama ukifanya utafiti angalau ukajua hiyo dawa hatari.
  Ili angalau tupate pa kusimamia tunapokuwa tunajadili hii issue kuliko kutegemea tu habari za midomo tu ya watu?
  Na watu wenyewe hata hawajulikani maana kila mtu anasema tu eti nimesikia watu watu wanasema. Lakini pia kwani watalamu wanasemaje? Wamedhibitisha hili?
   
 18. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #18
  Dec 13, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Lakini boss, unalinganishaje balaa la mbu wawili watatu waliofanikiwa kuingia kwenye net(kama kweli wamepenya yale matundu) na mziki mzima wa jeshi la mbu waliomo chumbani? Kiukweli sina hakika kama mbu wamefikia level hiyo ya maarifa ya kuweza kupinda mabawa na miguu yao kuweza kupenya yale matundu. Tunaweza kulalamikia ubora wa net kumbe ni net imezeeka au haichomekwi vizuri kitandani.

  Pamoja na hayo wewe unashauri mbinu gani mbadala kwa manufaa ya wengi?
   
 19. Nyaluhusa87

  Nyaluhusa87 JF-Expert Member

  #19
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 1,288
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Asante mkuu na majibu yako.Nadhani unaielewa vizuri hiyo dawa ya DDT.Kwenye hayo maswali uliyoniuliza cpingani sana na ww kwenye yale maelezo yako ya mwanzo.Tatizo liko hapo kwenye DDT...Hivi ukilinganisha wa2 wanaokufa na maralia kila cku na endapo utapulizia hiyo DDT,wapi wanakufa wengi?
   
 20. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #20
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  mkuu hapa umenena...najua wavivu wengi wa kufikiri hawatataka hata kusoma hii post yako na wao kuanza ku support maujinga tu bila sababu..kama ishu ya kuharibiwa ikulu au mambo mengine yoyote mabaya kuna njia nyingi sana zingeweza kutumika za siri kutumaliza ambazo ndio kimbilio kubwa sana kwa wabongo...mfano mitumba...maana kama wanaweza kuweka dawa ndani ya nyuzi kabisa kisha nyuzi zitumike kwa chandarua watashindwa vipi kutengeneza nguo kabisa zenye dawa ya kufanya hayo..na unajua wabogo wanavyopenda vya ulaya ulaya...halafu ni kweli hata kama wanataka kuja kutawala tena africa ili iweje...mbona kila wanachotaka saiz wanachukua tena mchana kweupeee.!?? kama ni kuja kuishi tu mbona wapo wengi wanaishi tena raha mstarehe bila kutumia taratibu zozote za nchi...!?? yaani tufunguke kwa kweli..
   
Loading...