Jamani wachina mnatutafuta ubaya.

uporoto01

JF-Expert Member
May 23, 2008
4,700
1,415
Kuna picha kwenye magazeti ya leo ikionyesha transfoma ya umeme likiungua TBC na Wachina watatu kwenye ngazi wakijaribu kuuzima kwa fire extinguisher na maelezo 'wafanyakazi wa TBC wakijaribu kuudhibiti moto huo'.Hivi tumefikia hatua ya kuajiri Wachina kufanya kazi kama hizi ? au sasa hatuwezi tena kutumia fire extinguisher kuzima moto ?
 
Wabongo walikimbia na mfanyakazi mmoja wa tanesco yupo icu hospital ya tmj kutokana na kuungua wakati anaiwasha transfoma!
 
Itakua labda watu wote tz wana ajira ndo maana wameamua kwaimport wachina kwenye ajira kama hizo
 
na bado,watakuja mpaka kuwa makonda,wapiga debe wauza genge,chipsi yai,watapisha vyoo,watoa mimba hapo ndio mtamjua mchina nani
 
na bado,watakuja mpaka kuwa makonda,wapiga debe wauza genge,chipsi yai,watapisha vyoo,watoa mimba hapo ndio mtamjua mchina nani
katika ujenzi wa barabara mikoani niliona mmoja akichanganya zege na mwingine akielekeza magari yapite kushoto nikawaza jamani hata kazi hizi kweli tunahitaji wataalamu ?
 
wale wachina ni wafanyakazi wa Startimes ambayo ina ofisi ndani ya jengo moja na TBC..
Yes na imewamwaga nchi nzima kwenye kila ofisi za star time, wamewapangia nyumba maeneo ya prime areas na kwenye nyumba hizo hujazana kama utitiri, siamini wote wako nchini kwa ajili ya kuuza vingamuzi tuu, lazima wana lao jambo la ziada!.
 
Kuna picha kwenye magazeti ya leo ikionyesha transfoma ya umeme likiungua TBC na Wachina watatu kwenye ngazi wakijaribu kuuzima kwa fire extinguisher na maelezo 'wafanyakazi wa TBC wakijaribu kuudhibiti moto huo'.Hivi tumefikia hatua ya kuajiri Wachina kufanya kazi kama hizi ? au sasa hatuwezi tena kutumia fire extinguisher kuzima moto ?

Kazi hatari kama hizi za kuzima moto wa umeme waachieni watu wenye ELIMU ya Fizikia kama wachina, umeme ni moto mara moja! wabongo ukisikia kasomea informatics, ujue kasoma manual ya computer applicationa, na sio computer fabrication.
 
Kwani hawaruhusiwi hata kutoa msaada? hiyo chuki ni ya nini? mnawachukia kisa wanapiga kazi 24hrs na wabongo walivyo wavivu wanataka kufanya kazi masaa sita tu...na bado hata magereza watapewa.....
 
tehe..jamani transfoma iliyolipuka iko ndani ya uzio wa TBC1 jirani kabisa na Ofisi za Star Times zinazomilikiwa na wachina. Cheche za moto kutoka kwenye transfoma zimesababisha generator la Star Times ambalo liko jirani kabisa na transfoma kushika moto na kulipuka na hivyo kusababisha mto mkubwa. Hivyo wachina walipaniki na walikuwa wakijitahidi kuuzima mto huo kwa kutumia "Fire Extinguisher".
 
Back
Top Bottom