Slave
JF-Expert Member
- Dec 6, 2010
- 5,314
- 2,635
Vodacom leo umenitumia ujumbe unaosema: umeshinda kiingilio bure katika droo ya samsung flat screen TV Leo na vodacom!tuma jina lako BILA GHARAMA kwenda 15015 sasa hatukutanii! vodacom mimi nimepata taabu kidogo kukuelewa ktk haya: 1 nimeshinda kiingilio!je unauhakika nilicheza mchezo wowote mpaka nishinde? 2 tuma kwenda 15015 sasa hatukutanii! Ina maana tangu nianze kutumia line yangu hii ya voda niliyo inunua kwa tsh 10,000 enzi hizo leo ndo umekuwa mkweli wakuniambia hunitanii?na je umewahi kunitania malangapi? Vodacom mbona unakosa hekima? Bado umenigeuza mimi bango la matangazo yako katika simu yangu mala ooh kazi ni kwako nk.au hujui kuwa hii hand set na sim card ni mali yangu? Vodacom punguza usanii utatumaliza.