Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 30,801
- 59,269
Kuwapenda ndugu wa mwenzio haina maana ufurahie wao kuhamia kwako(kuja kuja kila mara).Hiyo inabadilisha maana nzima ya ndoa aliyokua nayo anaeingia...familia ipo hata yake kaicha ili aje kuwa na mumewe na sio familia ya mumewe!Kama mama wa watu kajichokea badala ya kwenda kupumzika analazimika kukaa na wageni ambao unaweza kuta hata story nae hawana!Matumizi na maisha yanabadilika kwa muda maana kila anachofanya inabidi afikirie wageni!Wengine hua wanakuja na maneno basi tabu tupu...ukiwakuta wanaongea hao wananyamaza na kujifanya kukuchekea kinafiki!Kubadilisha mambo yanavyoenda nyumbani maana unaweza kuta mama kaacha maagizo ya lunch iwe wali maharage akirudi anaambiwa nyama jioni ilipikwa mchana kwasababu shangazi hapendi maharage...unadhani kama mambo ya aina hii yanaendelea dada wa watu ataacha kua alivyo?!Kuna watu hata ukiwachekea wanakwangalia tu!!
Muhimu huyo mume amuulize mwenzake nini tatizo...huwezi jua labda asipokuwepo ndugu wanambeza mke.
Alafu jamani nyie wanaume hata kama ndugu zenu wanawategemea mnashindwa nini kuwasaidia wakiwa mbali?!Epukeni matatizo yasiyo ya lazima kwakuwafikishia mahitaji yao walipo badala ya kuishi au kuwpo kwenu muda mwingi.Hao ndugu nao wajue kusalimia unakaa siku mbili unaondoka na sio kila mwezi unakuja!Simu zipo salimianeni kwenye simu maisha yaendelee!