Jamani tunaomba updates za ujenzi wa viwanda zikiwa pia na majibu ya maswali haya

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Wakati tukijiandaa kuwa nchi ya viwanda, ningependa kupata updates za ujenzi wa viwanda hivyo pamoja na majibu ya maswali yafuatayo:

1.Nini kinaendelea sasa kuhusu ujenzi wa viwanda na labda kiwanda cha kwanza kinatarajiwa kuanza kujengwa lini?

2.Mpaka sasa ni aina gani ya viwanda vinavyotarajiwa kujengwa?

3.Ni wawekezaji gani wameahidi kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta hii ya viwanda?

4.Kati ya hao, ni kina nani wameshawasili hapa nchi kwa ajili hiyo?

5.Ni wawekezaji wangapi wameshakabidhiwa hati za viwanja/ardhi ili waanze ujenzi wa viwanda hivyo?

6.Ni malighafi za aina gani zitatoka hapa nchini kwa ajili ya viwanda hivyo?

7.Mpaka sasa tunatarajia vijana wangapi wa kitanzania watapata ajira za muda katika ujenzi wa viwanda hivyo?

8.Ni meli ngapi zinazotarajia kuja, zilizoko njiani au zilizowasili hapa nchini zikiwa na shehena ya vifaa vya ujenzi wa viwanda hivyo?

9.Ni maeneo gani ambayo mpaka sasa yamefanyiwa au yanatarajiwa kufanyiwa Environmental Impact Assessment kwa ajili ya ujenzi wa viwanda?

10.Je, mpaka sasa ni vikao vingapi vimefanyika kati ya serikali,wadau wengine na wawekezaji kujadili utekelezaji wa azima ya ujenzi wa viwanda hapa nchini?

11.Mpaka sasa serikali imetenga au inakusudia kutenga ekari kiasi gani kwa ajili ya ujenzi wa viwanda hivyo?

12.Upatikanaji wa umeme umeboreshwa kwa kiasi gani kuipokea Tanzania ya viwanda?

13.Je,mpaka sasa kuna changamoto gani zimejitokeza katika kutekeleza kauli mbiu ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na hatua gani zimechukuliwa/zitachukuliwa kukabiliana na changamoto hizo?
 
Bado kwanza mchakato wa upembuzi yakinifu unafanyika na upo katika hatua za mwisho
 
Kwa sasa tuachie tushughulike na masuala ya msingi. 2020 ukiuliza maswali hayo tutakupa majibu mujarabu. Kwa sasa is too early
 
Mkuu Salary Slip

Ishu ya viwanda ilikuwa ni "Slogan" tu. Ni kama zile za "maisha bora kwa kila mtanzania". Je maisha bora tuliyaona?

Dawa na chanjo huko ma hospitalini zinawashinda ndio wataweza ku simamisha Integrated Plants?

Kwanza watu wenyewe wameshachanganyikiwa wamekosa direction. Akili zao zinawaambia kuwa UKAWA ndio wanakwamisha viwanda, kwa hiyo kutwa kucha ni kufikiria namna gani ya kupambana na UKAWA.
 
Maswali magumu hayo hayaitaji majibu mepesi
Hebu ngoja nitoe maoni yangu kuhusu Sera za uchumi zinazovutia ujenzi wa viwanda

Serikali kisera imeanza vibaya. Kuna concept moja ya Economics inasema Fiscal policy ndio Sera nzuri kujenga viwanda kuliko monetary policy. Fiscal policy inajumuisha tax and government expenditure. katika hii Sera kuna expansion and contractory fiscal policy. Kinachoonekana hivi ni contractory badala ya expansion yaan kuna utitili wa kodi kuanzia bandarini na uwekezaji wenyewe ambavyo havivutii watu kuwekeza ktk viwanda. Pia Serikali imebana matumizi ya fedha na kupunguza pesa kwenye mzunguko, so consumption ya products zinazotokana na viwanda itakuwa chini. Note that mtumiaji mkubwa ktk uchumi wetu ni Serikali.
 
Unajuwa hawa jamaa mwanzoni walidhani kazi ya serikali ni kujenga viwanda. Ndio akili zao zilivyokuwa zinawatuma.

Hawakujua kuwa kazi ya serikali ni kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji ili mimi, wewe na Yule tuwe attracted na kufanya uwekezaji.

Sasa yameharibu country economy both micro and macro levels.

Ni muwekezaji ambaye atakuwa ana matatizo kichwani mwake ndiye atakuja kuwekeza kati this current economic conditions.

People don't have anything in their pocket to spend. Ni muwekezaji gani anataka Payback period ya 30 years?
 
Maswali magumu hayo hayaitaji majibu mepesi
Hebu ngoja nitoe maoni yangu kuhusu Sera za uchumi zinazovutia ujenzi wa viwanda

Serikali kisera imeanza vibaya. Kuna concept moja ya Economics inasema Fiscal policy ndio Sera nzuri kujenga viwanda kuliko monetary policy. Fiscal policy inajumuisha tax and government expenditure. katika hii Sera kuna expansion and contractory fiscal policy. Kinachoonekana hivi ni contractory badala ya expansion yaan kuna utitili wa kodi kuanzia bandarini na uwekezaji wenyewe ambavyo havivutii watu kuwekeza ktk viwanda. Pia Serikali imebana matumizi ya fedha na kupunguza pesa kwenye mzunguko, so consumption ya products zinazotokana na viwanda itakuwa chini. Note that mtumiaji mkubwa ktk uchumi wetu ni Serikali.
Nadhani maoni haya yatawafikia wahusika.

Asante mkuu.
 
Bado kuna uhakiki wa watumishi hewa na mchakato wa kukabidhiwa ndege, ukiisha mchakato wa viwanda utaendelea.

Nawaza tu lakini..
Yaani utazani hao watumishi wanaohakikiwa ni kama maruhani hivi... yaani leo wanaonekana... kesho hawaonekani.

Inawezekana vipi zoezi lichukue miezi 10 kama sio kuleta Mambo ya kitoto?
 
Back
Top Bottom