Mimi ni mwanajamii mpya na hii ndo post yangu ya kwanza.
Mimi nasikitishwa na tatizo la kikatiba lililopo ambayo inampa rais madaraka kupita kiasi, kiasi kwamba nchi inakuwa kama kampuni binafsi ya mtu. Yaani atateua kila mtu amtakaye bila kuingiliwa na mtu yoyote. Mpaka watendaji wa tume ya uchaguzi anateua yeye kiasi kwamba wapinzani wanalalamikia uhuru wa tume kuweza kufanya haki katika chaguzi.
Matokeo yake ndo tunaona madudu ya ufisadi kila kona na tunaona watu wenye kashfa nzito nzito wanajitokeza hadharani kuomba uongozi bila aibu.
Kwa hiyo nashauri watanzania tubadilike kudai mambo ambayo yatatusaidia kama nchi na vizazi vijavyo kuliko hivi sasa ambapo utakuta kashfa nyingi za ubadhirifu wa mabilioni ya pesa za umma zinaibuliwa, kama EPA, richmond lakini watanzania tunakaa kimya tu utafikiri hakuna kitu kilichotokea. Let us be serious, tusiwe watumwa kwa kisingizio cha amani.