Jamani, shubiri ya mapenzi! Ushauri wako ni wa muhimu sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani, shubiri ya mapenzi! Ushauri wako ni wa muhimu sana

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mfalme Daud, May 29, 2012.

 1. Mfalme Daud

  Mfalme Daud Senior Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 168
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Nipo Dodoma. Nina rafiki yangu (mwanamume) analo jambo linalomsumbua na amenifuata nimpe ushauri. Nimeona si vyema, nichanganye na yenu hapa jamvini. Huyu rafiki yangu ana miaka 32, tunasoma naye degree ya kwanza na tunamalizia mwakani. Ana mpenzi wake na ni mzuri kwa kweli, kakamilika kila idara. Kwa kweli ana sifa zote za kuwa mke. Wote ni watumishi wa serikali na wana salary. Kama nilivyoeleza hapo awali, umri wa jamaa unazidi kusonga na alipanga kuoa mwakani baada ya kugraduate.

  Mpenzi wa rafiki yangu, hivi juzi akiwa ofisini kwake (Mbeya) alipatwa na Masahibu ya ajabu mapema mwezi huu. Alianguka ghafla mithiri ya mtu mwenye kifafa na kupoteza fahamu. Alibebwa na kupelekwa hospitali. Madaktari walimpima magonjwa yote wakakuta hana. IKABIDI APIGWE X RAY, NDIPO WAKABAINI ANA KOVU KTK UBONGO. ALISHAURIWA KWAMBA TATIZO LINATIBIKA JAPO LITACHUKUA MUDA WA MIAKA 5. Alipewa dozi ya kunywa kila siku kwa muda wa miaka 5. N.B alishauriwa asizae mtoto kwa muda wote huo I.E miaka 5. AKizaa, basi mtoto hatakuwa na akili timamu. Alimpatia mpenzi wake taarifa huku akiwa na hofu nzito KUTOKANA NA KIPINDI HICHO KIREFU. Rafiki, amekuja kuniomba ushauri afanyeje? Kama nilivyoeleza hapo awali, jamaa alichelewa kuoa, ana miaka 32 hana mtoto yeyote. MIAKA 32+MIAKA 5 JUMLA NI 37! JAMAA ANAMPENDA KWELI MPENZI WAKE, AKIMWAMBIA ANAMWACHA ANAOGOPA ANAWEZA CHUKUWA MAAMZI YOYOTE.

  NA HILI TATIZO LA KUANGUKA LINAENDELEA KUTOKEA HATA BAADA YA KUANZA DOZI, RAFIKI YANGU ANAENDELEA KUMFARIJI KWAMBA BADO ANAMPENDA. JAPO KWA KINYWA CHAKE AMESEMA YUPO NJIAPANDA KUTOKANA NA UMRI WAKE KUWA MKUBWA I.E 32 YRS. NAOMBENI USHAURI WENU ILI NIWEZE KUMPATIA PLZ.

  NAWASILISHA JAMVINI
   
 2. J

  JOJEETA Senior Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa tatizo liko wapi hapo/cha muhimu ni huyo rafiki yako kuwa mvumilivu kama ana mapenzi ya dhati kwa mchumba wake,image kama hali hiyo ingetokea akiwa ndani ya ndoa je angeacheat au angemuafha?..........jambo lingine mwambie kama anamwamini Mungu basi ampeleke kwenye maombi kwani Yesu anaweza yote
   
 3. JS

  JS JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2012
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Amvumilie tu mpenzi wake na kama kweli anampenda kwa dhati na angependa kuishi naye milele miaka mitano si kitu. asimwache huyo dada wa watu kisa huo ugonjwa. pia akumbuke kupata mtoto pia ni majaliwa hata kama una hamu ya kuwa na familia kiasi gani. matatizo ya kiafya hayaishi miilini mwetu. ikiwezekana dada akistabilize ugonjwa wake huku akiendelea na tiba bila ya kumsahau Mungu kwa kufanya maombi wafunge ndoa na jamaa atashangaa jinsi siku zinavyoenda. Pia kuanzisha familia ukiwa na miaka 37 si mbaya jamani ni umri mzuri tu sema kwa sababu huyo kaka ana hamu ya familia sana kipindi hii lakini atulize kidogo awe nguvu ya mwenzie.
   
 4. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Moja ya mitihani tuliopewa binadamu na Mwenyezi Mungu ni kiwango cha uvumilivu! Mwambie rafikio avumilie ktk parameters zote. Baada ya uvumilivu, kuna mambo mazuri mbele.
   
 5. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nina umri wa miaka 52 na nina mtoto wa umri wa miaka 5. Na afanye hesabu, ina maana nimezaa nikiwa na miaka 47. Sasa miaka 37 ndio iondowe mapenzi? Au rafiki yako hahitaji mapenzi bali anahitaji mtoto tu.
   
Loading...