Jamani, shubiri ya mapenzi! Ushauri wako ni wa muhimu sana

Mfalme Daud

Senior Member
Feb 3, 2012
166
109
Nipo Dodoma. Nina rafiki yangu (mwanamume) analo jambo linalomsumbua na amenifuata nimpe ushauri. Nimeona si vyema, nichanganye na yenu hapa jamvini. Huyu rafiki yangu ana miaka 32, tunasoma naye degree ya kwanza na tunamalizia mwakani. Ana mpenzi wake na ni mzuri kwa kweli, kakamilika kila idara. Kwa kweli ana sifa zote za kuwa mke. Wote ni watumishi wa serikali na wana salary. Kama nilivyoeleza hapo awali, umri wa jamaa unazidi kusonga na alipanga kuoa mwakani baada ya kugraduate.

Mpenzi wa rafiki yangu, hivi juzi akiwa ofisini kwake (Mbeya) alipatwa na Masahibu ya ajabu mapema mwezi huu. Alianguka ghafla mithiri ya mtu mwenye kifafa na kupoteza fahamu. Alibebwa na kupelekwa hospitali. Madaktari walimpima magonjwa yote wakakuta hana. IKABIDI APIGWE X RAY, NDIPO WAKABAINI ANA KOVU KTK UBONGO. ALISHAURIWA KWAMBA TATIZO LINATIBIKA JAPO LITACHUKUA MUDA WA MIAKA 5. Alipewa dozi ya kunywa kila siku kwa muda wa miaka 5. N.B alishauriwa asizae mtoto kwa muda wote huo I.E miaka 5. AKizaa, basi mtoto hatakuwa na akili timamu. Alimpatia mpenzi wake taarifa huku akiwa na hofu nzito KUTOKANA NA KIPINDI HICHO KIREFU. Rafiki, amekuja kuniomba ushauri afanyeje? Kama nilivyoeleza hapo awali, jamaa alichelewa kuoa, ana miaka 32 hana mtoto yeyote. MIAKA 32+MIAKA 5 JUMLA NI 37! JAMAA ANAMPENDA KWELI MPENZI WAKE, AKIMWAMBIA ANAMWACHA ANAOGOPA ANAWEZA CHUKUWA MAAMZI YOYOTE.

NA HILI TATIZO LA KUANGUKA LINAENDELEA KUTOKEA HATA BAADA YA KUANZA DOZI, RAFIKI YANGU ANAENDELEA KUMFARIJI KWAMBA BADO ANAMPENDA. JAPO KWA KINYWA CHAKE AMESEMA YUPO NJIAPANDA KUTOKANA NA UMRI WAKE KUWA MKUBWA I.E 32 YRS. NAOMBENI USHAURI WENU ILI NIWEZE KUMPATIA PLZ.

NAWASILISHA JAMVINI
 
Amsubirie, mbona yeye kasubiriwa. Anadhani huyo dada yeye ndio hana hofu ya kuwa mtu mzima sana wakati atakapoambiwa sasa anaweza kuzaaa?
 
Haya ndo matatizo ya kutokujua maana ya kupenda,huwezi kusema unampenda mtu halafu unajiuliza kwenye changamoto kama hii ufanyeje.Mwambie amuoe na asubiri muda ufike ndipo watafupe mtoto.Miaka 37 kitu gani bana?Watu wengine wamepata mtoto kwanza wakiwa 44 sembuse 37!!Mwambie aache kuwehuka!
 
Kwa mfano yeye ndio angekuwa na hilo tatizo angependa mwenzie achukue uamuzi gani? Hapo ndio anatakiwa aonyeshe upendo wa kweli!
 
Anasema anampenda at the same time yuko njia panda??hakuna upendo wa hivyo!
 
umri wa jamaa unazidi kusonga kwani wa binti umesimama? tusiimbe mapenzi mdomoni tu, let's walk the talk guys....
 
Mitihani ya maisha ni mingi kwa kweli! Anaweza kumuacha mpenziwe anaempenda, akakimbilia kuoa mwingine na wasibarikiwe mtoto. Na hakuna guarantee kuwa akioa ambae haanguki sasa hivi, hatopatwa na tatizo lolote la kiafya baadae. Amuoe mpenziwe kama walivyopanga, hayo ya watoto na afya njema yana Mungu mwenyewe.
 
hapo ndipo atakapobaini kiwango cha mapenzi ambacho moenzi wake anachojuu yake....
 
pole kw matatizo,kama anampenda kweli kwanza walishugulikie hilo tatizo la ubongo. kwa uoni wangu ameambiwa asizae bcoz dawa anazotumia ni teratojen( zinaweza kusoababisha madhara kwa mtoto) so anaweza kubadilisha dawa akanza zenye effect ndogo anaweza kupata mtoto salama.
ubongo ukipata tatizo km unahitaji kufanyiwa operartion hufanywa mapema, inakuwaje ambiwe asubiri miaka5!
ampeleke hospital nyengine kwa vipimo zaidi ya CT or MR.. x ray ni kipimo kidogo kwa kujua tatizo la ubongo
 
pole kw matatizo,kama anampenda kweli kwanza walishugulikie hilo tatizo la ubongo. kwa uoni wangu ameambiwa asizae bcoz dawa anazotumia ni teratojen( zinaweza kusoababisha madhara kwa mtoto) so anaweza kubadilisha dawa akanza zenye effect ndogo anaweza kupata mtoto salama.
ubongo ukipata tatizo km unahitaji kufanyiwa operartion hufanywa mapema, inakuwaje ambiwe asubiri miaka5!
ampeleke hospital nyengine kwa vipimo zaidi ya CT or MR.. x ray ni kipimo kidogo kwa kujua tatizo la ubongo

niushauri mzuri hebu akacheki hosp mbili tatu kama ni the sa e case ok
 
Huyu hajui ratiba za Mungu, anaweza kumuacha akidai anataka azae haraka umri unakwenda akajikuta anakoenda anakaa 20 years ndipo mtoto anakuja au asije kabisa...! kumtenga mtu kwa kisa cha tatizo lake sio vizuri na binadamu tujifunze na kusaidiana kwa shida na raha kwani kesho yetu sisi wazima wa afya hatuijui iko mikononi mwa muumba wetu tu.

Ninamshauri aubebe ujasiri amuombe Mungu na asimtenge huyu mpenziwe katika kipindi hiki kigumu, amuoe tu kwani yote anapanga Mungu
 
Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, na hustahimili yote....yeye ndio atamsaidia huyo mdada kupona haraka
 
"Kama kweli anampenda, huu ndiyo muda wa kuonesha kuwa yu moyoni mwake, asubirie mpaka mwisho".....Afunge kwa Maombi na kumwombea Mungu amponye kwani madaktari ni akina nani? GOD IS ABLE....Kuna rafiki yangu alivunjika miguu yote miwili madaktari walisema atakatwa miguu....lakini tulimpa moyo na ushirikiano wa karibu...ukimwona huwezi jua kama alivunjika kapona...Miaka 32 kitu gani? watu wanaoa wana miaka 40 na mambo yanakwenda.....
 
ndo maana nasemaga watu wakipata chance ya kuzaa kabla hawajafika 30 bora tu wafanye hivyo maana chelewa chelewa ona sasa!!
 
MWanaume mwenye umri wa miaka 37 anakuwa amechelewa kuoa au kuzaa??!! Dah sikujua kuwa huu ni umri mkubwa kwa mwanaume kuoa na kuwa na familia!
 
mi kuna mdada namfaham bf alipata ajali na akavunjika mguu 1 na mbavu kibao, sasa wenzake(mdada) wakawa wanamwambia kuwa jamaa kiwanda lazima kitakuwa kimeharibika so hatoweza kuzaa tena, ila dada alionyesha msimamo na hakumuasha mskaji mpaka alipopona baada ya miez kama 10 hv. Mwisho wa siku wameonana na wana mtoto 1,

so mi namshauri huyo jamaa asimwache huyo dada, hiki ndo kipimo cha upendo!!!
 
Back
Top Bottom