Jamani serikali, hivi kweli mbunge Lema yuko Lupango mpaka leo?!

Ivi huko jela aliko yupo v.i.p ama yupo pamoja na wale wezi wa kuku ?
 
Katika kutafuta haki fulani huwa ni lazima baadhi ya watu waumie kwa niaba ya wengine. kinachofanyika kwa Mh. Lema ni kudhihirisha kuwa yeye yuko tayari kutamka na kutenda kwa ajili ya wengine wasio na uwezo huo kwa sababu mbali mbali. Kitu ambacho watawala wa Africa wanatakiwa kujifunza ni kwamba siasa siyo vita wala ugomvi lakini siasa hiyo hiyo ikitumika vibaya inaleta vita na kusambaratisha jamii nzima. Katika hili mifano ni mingi na sihitaji kuitaja.

Daima, huwezi kuinua umaarufu wako au wa jamii yako kwa kukandamiza/kunyanyasa jamii nyingine. Umaarufu wa mtu au jamii huinuka kwa matendo yaliyomema na sifa huletwa na aliyetendewa mema na wala siyo aliyetenda kwani hajui alitendalo kama ni jema au la.
 
Duh! Hivi Mh. Lema kakosa nini kiasi cha kusota lupango mpaka leo? People's Power iwapi na viongozi mlituahidi kuja kwa wingi mahakamani kumtoa mbunge wetu, kama hataachiwa!

Kipi kimewarudisha nyuma makamanda wangu ? Halafu siwaoni viongozi wa kitaifa hata mmoja kuja mahakamani kumpa kampani!, mmemuacha mwenyewe na askari magereza!! Inaniuma sanaa!
USIWE NA SHAKA KILA KITU KINA WAKATI WAKE!!!!
 
Back
Top Bottom