Jamani sekta ya madini Africa kwa ujumla mnaionaje?

Qastrap

Member
Nov 24, 2010
17
20
kheri wazeiya?
Nilidhani bongo kwetu ndo kunatatizo la maisha mabovu kwa wananchi ambao tena wanaishi katika miji ambayo inamadini ya kutosha...labda hii ni kwasababu wachimbaji wadogo wadogo hawana utaalamu wowote juu ya madini hayo na biashara yenyewe! Lakini, kwani wanatakiwa waifanyaje hii kazi? Naweza kujaribu kujitupa?
Kumbe hata people wa congo pamoja na utajiri wote ule wa madini wanasota kama kawa........
 

Neytemu

Member
Nov 7, 2010
83
0
mi naona secta ya madini inatuumiza wananchi na zaidi inatutafutia umasikini maradufu kwa vizazi vijavyo maana kwa sasa tu hata wananchi wanaoishi jirani na machimbo haya hawanufaiki na hata serikali inachotoza hakina uwiano na kinachopatikana katika sekta hii nyeti:angry:
 

mhandisi_1

Member
Nov 27, 2010
72
150
Tunatakiwa kuwa wajanja, tuunganishe uchumi wetu kwa uchumi wa makampuni ya madini, mfano tujipange kwa makusudi kuhakikisha tunaanza kutoa huduma (zile tunazoweza, kama vyakula, supplies of local produce n.k.) ili tuweze kulazimisha kiasi fulani cha pesa kibaki Africa - Tanzania kwa njia ya biashara na utoaji huduma. Inasikitisha kuona bidhaa kama maziwa yanaagizwa nje ili yatumike migodini wakati migodi yote iko kanda ya Ziwa - eneo linaloongoza kwa wingi wa Ngo'mbe!
 

Neytemu

Member
Nov 7, 2010
83
0
Tatizo mazingira hayo ya wenyeji kufanya supply migodini hayakuwekwa kama sehemu ya mikataba na inakua ngumu kulazimisha.Huenda hata samaki na nyama zinatoka nje.
 

Ndahani

Platinum Member
Jun 3, 2008
17,706
2,000
We have not tried to incoporate the issue of mining our resources into our mainstream tax base shrewdly. Tumefanya hivyo kwa kutumia njia za mkato kwa hiyo contribution yake ni kama haipo. Tatizo kubwa ni kukosa kujiamini kama tunaweza na tuna sababu ya kuwabana hawa wawekezaji.
On the other hand, uwezo wetu wa kuwabana wawekezaji utakuwa mkubwa kama tutafanikiwa kuzalisha nishati ya kutosha ya kuzalisha hayo madini, maji ya kutosha na kuwa na wataalamu wengi wenye uwezo wa kutoa mchango positive.
Kama tunataka kufanikiwa ni lazima tupanue uwigo wa namna tunavyofanya mambo yetu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom