Ndallo
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 7,619
- 4,292
Kweli nimeamini shukrani ya Punda ni mateke! Mama huyu amekitumikia chama chake cha CCM kwa miongo 18 akiwa kama Mkuu wa wilaya tofauti katika taifa hili! Akiwa kama kada muadilifu kwa chama chake lakini sipati picha aliwajibishwa na bosi wake JK kwa kosa gani! Alishawahi kuwa mkuu wa wilaya kadhaa kama vile Kinondoni/Bagamoyo na Kibaha. Sasa hivi jamani anaugulia kitandani na hakuna wa kumsaidia na hata chama chake cha CCM? Pole sana Mama Hawa Ngulume kwa yalio kukuta ni Mungu tu atakae kusaidia. Mama Hawa Ngulume subiri tuone serikali mpya kwa awamu ya pili kwa aliyekua bosi wako labda anaweza kua amesikia kilio chako natumaini hata hapa JF huwa anapitiaga akaona Post hii kuwa na subira hata Spika wa Bunge letu tukufu ni mwanamke Mama Anna Makinda natumaini atakakua ameshasikia kilio chako.:sad: