Jamani PCCB/takururu imetukifu kabisa...!

Siao

Member
Jan 4, 2008
96
3
Mwenye hoja na athibitishe kama hiki kitengo sio kinaonyesha mazingaumbwe nchini. Wakati ule tukiwa watoto wa primary tuliona vitu kama hivi vinavyofanywa na pccb. Hawana jambo lolote serious zeidi ya warsha na makombano, ofcourse nani yule amesema wanachunguza rushwa za ngono... maana yake mambo ya mepenzi. The organ is very vey poor in approaches, perspectives and methodologies.

Inaudhi mno kusikia eti wamemkamata mtendaji wa kijiji na hongo ya gongo... na mafisadi wakiwepo ma vijisenti.

Ukisikia kic
 
Wameapa...kukabana koo na kuwakimbiza kuwatishia amani watumishi...wale wa chini chini..na virushwa vyao mbuzi..ila si rushwa nono nono,sheria haiwahusu kama ambavyo DG wao alivyotanabaisha kuwa wao "si kazi yao"......nahisi kazi yao ni "research bila combating"...huko wilayani wanaogopwa kweli kweli ila si huku ngazi juu.........nawakilisha
 
It is appalling kuona anaeyongoza TAKURURU ni Dk lakini anachemka hakuna mfano. anaongea kama mwanasiasa mwerevu! Mambo ya Rushwa iliyokithiri amaayo huwezi kuitenganisha na UFISADI Uliozagaa Tanzania still anasema kesi 10 ZITATAJWA MWAKA HUU!! He makes me feel sick.

hebu soma hii hapa chini. Sioni mantiki Mpaka apikiwe na apewe allowance ya seminar ndiyo ayaseme haya hapa chini.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuizua Rushwa Nchini, (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea, amesema uchunguzi wa kesi kubwa 10 za rushwa utatangazwa mwaka huu.

Alisema kuwa kati ya kesi tano matokeo yake yanatarajiwa kutangazwa baada ya mwaka wa fedha wa serikali ambao unamalizika Juni 30, na zingine ifikapo Desemba, mwaka huu.

Hayo alisema jana wakati akifunga semina ya siku mbili iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la African International Group of Political Risk Analysis (PORIS) kuhusu maboresho ya Utawala Bora dhidi ya kupambana na rushwa iliyofanyika, Bagamoyo mkoani Pwani.

Dk. Hosea alisema uchunguzi wa kesi zimefikia katika hatua nzuri ya kukamilika na matokeo ya kwanza yanatarajia kutangazwa mwishoni mwa mwaka wa fedha.

Alisema PCCB itachunguza kesi zote ambazo zinawakabili baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu serikalini ambao wanahusika na kuingia mikataba mibovu ya serikali ambayo inadaiwa rushwa ilitumika katika kupitisha mikataba hiyo.

Dk. Hosea alisema taasisi hiyo haijalala usingizi kuhusiana na tuhuma za rushwa ambazo zinawakabili viongozi ambazo zingine zimeibuliwa na wabunge.

Aidha alisema kuwa, wananchi wasifikiri hawafanyi lolote dhidi ya tuhuma za rushwa na kuongeza kwamba jamii inatakiwa kushirikiana na chombo hicho ili kuweza kutoa taarifa za rushwa.

Dk. Hosea alisema kuwa baada ya uchunguzi wao watapeleka uchunguzi wao mbele ya vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.

Hata hivyo, aliushukuru Ubalozi wa Ubelgiji kwa ufadhili wa fedha kutoka PORIS katika kuenzi utawala bora nchini Tanzania.

Mkurugenzi wa PORIS, Bw. Prince Bagenda, alisema kuwa semina hiyo inafuatia matokeo ya Brussels yaliyofanyika Machi 14-15 mwaka jana nchini Ubelgiji kuhusiana na maboresho ya Utawala bora na jinsi ya kupiga vita rushwa.
 
Taasisi ya kuruhusu na kuwalinda wala rushwa (TAKUKURU)
 
Taasisi ya kuruhusu na kuwalinda wala rushwa (TAKUKURU)

Mimi sina la kusema .Maana kumbe matokeo yanatangazwa kwa nyakati maalumu.Yaani uchunguzi unachukua mwaka mzima .Kwa nini iwe wakati wa kipingi cha mwisho cha mwaka wa fedha ?
 
Kama kawaida hiyo ni mbwembwe za ninara. Ukweli ni kuwa Viongozi wetu waliowengi whether ni wa kuteuliwa ama kuchaguliwa wote lengo na macho yao ni KUFISADI. Sioni msafi hata kidogo. wanalindana, wnapeana janja, wnapeana mikakati. Je unajua Leaders club?? na vigenge vingine? kamam wewe ni kapuku ukutuhumiwa tu kesho kazi huna na next uko makahamania na vyombo vya habari kila kona, tena utbatizwa kigogo. kumbe Tarishi!! Nilishawahi kuandika Humu kuihusu balali kuwa moto utaisha na itakuwa hivihivi. siju ni ushahidi gani unatafutwa!! Mawili KULINDANA ama they are not competent. au yote. Uwoga wa kupoteza kazi.
 
Simply put PCCB is useless and hopeless, yenyewe pia ni ufisadi, inatumia pesa nyingi kuwepo lakini haifanyi kazi yoyote. Chenge ana shahidi mzuri, amewasifu SFO lakini hakusema PCCB, kwa sababu anajua ni bogus!
 
Kwa nini iwe wakati wa kipingi cha mwisho cha mwaka wa fedha ?
Lunyungu, yani sijui tumepigwa na kipapai gani Mtanzania mwenzangu. Kukamilika kwa uchunguzi na mambo ya bajeti wapi na wapi? Hivi sisi tuna akili kweli jamani?

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuizua Rushwa Nchini, Dk. Edward Hosea ...alisema kuwa kati ya kesi tano matokeo yake yanatarajiwa kutangazwa baada ya mwaka wa fedha wa serikali ambao unamalizika Juni 30, na zingine ifikapo Desemba, mwaka huu.

...aliushukuru Ubalozi wa Ubelgiji kwa ufadhili wa fedha kutoka PORIS katika kuenzi utawala bora nchini Tanzania.


Katikati ya maskandali ya rushwa na uozo wa Serikali, huyu bin Adam anathubutu kusema tumepewa tuzo ya utawala bora! Mchana mchana kweli? Hawa ndio wanasababisha dunia iseme 'Dr. Watson was Right.'

Roho inaniuma ile mbaya, natetemeka!
 
Sie wengine pesa zatu zinaishia kwenye mambo kama haya

1209502595.jpg
 
Back
Top Bottom